NGARA: Mwanamke aua mke mwenza na kumzika shambani

Ngara. Mwanamke mkazi wa Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara anatuhumiwa kumuua mke mwenza na kumzika shambani.

Kifo hicho kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi kimetokea katika Kata ya Kibimba mkoani Kagera ambako aliyeuawa alizikwa kwenye shamba la viazi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mayenzi, Philipo Rutumbanya amesema Edina Joseph (28) anatuhumiwa kumuua Noelina Joseph (24).

Wawili hao ni wake wa Joseph Laurean (33), mkazi wa Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara.

Rutumbanya amesema mauaji hayo yalifanyika jana Jumatano Desemba 13,2017 saa 7:30 mchana na kwamba mtuhumiwa amefikishwa polisi.

Amesema Edina alihisiwa kuhusika na mauaji baada ya mumewe kumkuta akiwa na damu mwilini shambani.

Mwenyekiti huyo wa kijiji amesema Laurean alipomhoji mkewe hakujibu lolote na alipofuatilia shambani aliona nguo za mkewe mdogo lakini yeye hakuwepo.

Amesema Laurian alitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ndipo mtuhumiwa Edina alipohojiwa na alieleza alikuwa na chuki na mke mwenzake aliyeolewa miezi miwili iliyopita.

Mwenyekiti huyo amesema walimweka Edina chini ya ulinzi na aliwapeleka kwenye shamba la mume wake ambalo ni mali ya binamu yake John Shimimana alikoonyesha alikomzika mwenzake kwenye tuta la viazi.

Akizungumzia tukio hilo, mume wa wake hao, Laurian amesema ameishi na Edina kwa miaka 12 na wamejaliwa watoto watano; wa kike mmoja na wa kiume wanne. Pia ni mjamzito.

Laurian amesema mkewe mdogo alimpangia nyumba katika Kijiji cha Kanazi umbali wa kilomita sita kutoka Kijiji cha Mayenzi na alimpatia shamba ambalo alipewa na binamu yake Shimimana, ambaye ni diwani wa Kata ya Kibimba.

Amesema alipotoka matembezi kijijini alifika nyumbani kwa Edina alikokuwa amelala Jumanne Desemba 12,2017 lakini hakumkuta.

Laurian amesema alikwenda kumuona mkewe mdogo Noelina aliyekuwa shambani ambako alimkuta Edina akiwa na jembe na mwili ukiwa na damu.

Amesema alipomhoji kuhusu damu alitetemeka na alipofuatilia alikuta nguo za Noelina lakini yeye hakuonekana.

"Tangu nioe mke wa pili kumekuwa na malumbano na malalamiko lakini niliona kawaida sikutarajia kama angechukua uamuzi wa kumuua mwenzake," amesema Laurian.

Polisi wilayani Ngara imefika eneo la tukio ambako Edina amekamatwa na baada ya kupata kibali cha Mahakama ya Wilaya ya Ngara mwili wa Noelina umefukuliwa.

Akizungumza wakati wa kufukua mwili ofisa upelelezi wa Polisi wilayani Ngara, Edward Masunga amewataka wananchi wakiwemo wanandoa kufuata utaratibu wa kufikisha malalamiko kwa viongozi wa vijiji badala ya kujichukulia sheria mkononi.


Mwananchi
Umalaya haujawahi kumuacha mtu salama,hili liwe fundisho kwa wanaume wote wenye tabia ya umalaya.Ni vema tukaridhika na wenzi wetu.
 
Mme kushindwa kumdhibiti mke anaamua kuleta mwingine apunguze dharau. Kuua mtu ni uamuzi mbaya!
 
Apumzike kwa Amani. Ila Bi Mkubwa ana moyo, kuchukua maamuzi kama hayo.
 
Alafu mtuhumiwa ana mimba huyo mtoto atazaliwa jela na hatapata nafasi ya kuinjoy maisha ya familia
 
Binti wa miaka 28 ana watoto WATANO na mimba juu na bado kijeba kimeongeza mke!! Aliyesema ukielimisha mwanamke umeelimisha jamii bila shaka alipata PhD, ukombozi pekee wa hawa mabinti ni ELIMU PEKEE. Kwa hesabu hizo aliolewa at 16 na hana tegemeo jingine la maisha isipokuwa MUMEWE na ndio maana kachukua maamuzi magumu maslahi yake yalipoguswa!
 
Halafu kwa uwezo alionao huyo jamaa lakini bado kuna mtu humu ndani kaweka uzi wake ananyegeka kila wakati sasa amekuja kuulizia dawa na kasema kabisa ameshamchiti mme wake sana ila nafuu hakuna,nampa ushari bure kuwa jamaa huko Ngara hana mke yuko single aende tu kwahuyo dawa ataipata.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP), Augusine Ollomi amesema picha zinazoendelea kusambaa mtandaoni zikionyesha askari Polisi wilayani Ngara Mkoani Kagera wakishirikiana na wananchi kufukua mwili ni za kweli.

Picha hizo zinazoonesha Maaskari wakifukua mwili wa Noelina aliyeuliwa na mke mwenza wa marehemu Noelina Joseph mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa kijiji cha mayenzi wilayani humo ni tukio la kweli.

Noelina Joseph (24) mkazi wa kijiji cha Mayenzi wilayani humo aliyeuawa na mke mwenza jana na kuzikwa kwenye shamba la viazi kutokana na wivu wa kimapenzi baada ya kuolewa na mume mmoja kijijini humo.

“Ni kweli tukio hilo limetokea huko Ngara na tayari maafisa wetu wapo eneo la tukio ila bado uchunguzi zaidi haujafanyika ndio tunaendelea nao” ,amesema kamanda Ollomi.
 
Akili nyingine mweh!
Kutoa roho ya binadamu mwenzio kisa binadamu mwingine. Na wanaume wote hawa duniani..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom