NGARA: Mwanamke aua mke mwenza na kumzika shambani

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,409
20,766
index.jpeg
Ngara. Mwanamke mkazi wa Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara anatuhumiwa kumuua mke mwenza na kumzika shambani.

Kifo hicho kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi kimetokea katika Kata ya Kibimba mkoani Kagera ambako aliyeuawa alizikwa kwenye shamba la viazi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mayenzi, Philipo Rutumbanya amesema Edina Joseph (28) anatuhumiwa kumuua Noelina Joseph (24).

Wawili hao ni wake wa Joseph Laurean (33), mkazi wa Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara.

Rutumbanya amesema mauaji hayo yalifanyika jana Jumatano Desemba 13,2017 saa 7:30 mchana na kwamba mtuhumiwa amefikishwa polisi.

Amesema Edina alihisiwa kuhusika na mauaji baada ya mumewe kumkuta akiwa na damu mwilini shambani.

Mwenyekiti huyo wa kijiji amesema Laurean alipomhoji mkewe hakujibu lolote na alipofuatilia shambani aliona nguo za mkewe mdogo lakini yeye hakuwepo.

Amesema Laurian alitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ndipo mtuhumiwa Edina alipohojiwa na alieleza alikuwa na chuki na mke mwenzake aliyeolewa miezi miwili iliyopita.

Mwenyekiti huyo amesema walimweka Edina chini ya ulinzi na aliwapeleka kwenye shamba la mume wake ambalo ni mali ya binamu yake John Shimimana alikoonyesha alikomzika mwenzake kwenye tuta la viazi.

Akizungumzia tukio hilo, mume wa wake hao, Laurian amesema ameishi na Edina kwa miaka 12 na wamejaliwa watoto watano; wa kike mmoja na wa kiume wanne. Pia ni mjamzito.

Laurian amesema mkewe mdogo alimpangia nyumba katika Kijiji cha Kanazi umbali wa kilomita sita kutoka Kijiji cha Mayenzi na alimpatia shamba ambalo alipewa na binamu yake Shimimana, ambaye ni diwani wa Kata ya Kibimba.

Amesema alipotoka matembezi kijijini alifika nyumbani kwa Edina alikokuwa amelala Jumanne Desemba 12,2017 lakini hakumkuta.

Laurian amesema alikwenda kumuona mkewe mdogo Noelina aliyekuwa shambani ambako alimkuta Edina akiwa na jembe na mwili ukiwa na damu.

Amesema alipomhoji kuhusu damu alitetemeka na alipofuatilia alikuta nguo za Noelina lakini yeye hakuonekana.

"Tangu nioe mke wa pili kumekuwa na malumbano na malalamiko lakini niliona kawaida sikutarajia kama angechukua uamuzi wa kumuua mwenzake," amesema Laurian.

Polisi wilayani Ngara imefika eneo la tukio ambako Edina amekamatwa na baada ya kupata kibali cha Mahakama ya Wilaya ya Ngara mwili wa Noelina umefukuliwa.

Akizungumza wakati wa kufukua mwili ofisa upelelezi wa Polisi wilayani Ngara, Edward Masunga amewataka wananchi wakiwemo wanandoa kufuata utaratibu wa kufikisha malalamiko kwa viongozi wa vijiji badala ya kujichukulia sheria mkononi.


Mwananchi
 
Wanaume upendo haugawanyiki ndio mjue hivyo..
Hao wanawake hawakulazimishwa lakini. Sasa hapa tatizo linakuwa kwa mwanaume au mwanamke? Sasa mwanamke anaona mume ana mke halafu anakubali mwenyewe kuolewa kuwa mke mwenza.
 
Acha na kitu kutoa uhai wa mtu wewe, sikia tu, kachanganyikiwa, damu kwenye nguo anaziona ila akili haipo anaona ni rangi, nguo za marehemu zipo pembeni ila akili haijui cha kufanya. Yan akili zote zilihamia kwenye nguvu ya kuchimbia shimo.
 
aisee kweli haya ni makubwa kutoa roho ya mtu kisa nini jamani mwisho wa dunia kuna mambo
 
Mara nyingi Migogoro inayohusiana na Mapenzi ndiyo huwa na madhara makubwa pale busara isipotumika ama suluhu isipopatikana mapema!!
 
Apumzike kwa amani.....
Bi mkubwa si angeaga tu shindano, sasa ataacha watoto masikini akakae gerezani pole zake.
 
RIP mke mwenza.

Kunyongwa hadi kufa mke mkubwa.

BONGO MOVIE, CHUKUENI STORY HIYO FANYENI YENU. ITAKUWA KALI MNO.
 
Acha izo wewe,
Mbona babu zetu waliweza kuishi hadi na wake 5
Na mapenzi yaligawanyika km kawa.
Yaani witu tu ndio umtoe mtu roho
Sasa acha akafie magereza akose mume na mke mweza
Huyo ana roho mbaya hataki mwenzake aolewe apate mume. Ni ndoto ya kila mwanamke kua na mume au kuitwa mke wa fulani..

Wanaume wenyewe tuko wachache sasa tusipooa wanawake wengi nani atawaoa?

Kwanza hata asili na sayansi havikubaliani na mwanaume kua na mke mmoja.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom