NGARA: Basi kampuni ya Emirates lapata ajali na kuua watu 15 baada ya kupinduka

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
May 3, 2020
2,416
3,911
Watu 10 Wamefariki dunia na Wengine watano kujeruhiwa na kupelekwa hospital teule ya Nyamiaga wilayani Ngara, baada ya gari la abiria mali ya kampuni ya Emirates kuanguka likitokea Ngara kwenda Bukoba.

Mganga mfawidhi wa hospital hiyo, David Mapunda amethibitisha.

1.jpg
2.jpg

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumamosi Oktoba 24, 2020 ametuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya basi iliyosababisha vifo vya watu 15.

Ajali hiyo imetokea leo wilayani Ngara Mkoa wa Kagera baada ya basi la kampuni ya Emirates lililokuwa likitokea Ngara kwenda Bukoba kupinduka katika mteremko wa Kumnyange wilayani Ngara Mkoa wa Kagera. Katika ajali hiyo watu 18 wamejeruhiwa.

Taarifa iliyotolewa leo na mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa Magufuli amemtumia salamu za rambirambi mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti na amemtaka kufikisha salamu za rambirambi kwa familia na wote walioguswa na vifo hivyo na kuwatakia majeruhi wapone haraka.

“Nimesikitishwa na vifo vya Watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika ajali hii, nawapa pole wafiwa wote na nawaomba wawe na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi,” amesema Magufuli.

Taarifa hiyo imesema Rais amewataka watumiaji wa barabara hasa madereva wa magari kuzingatia sheria zote za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

“Pia amevitaka vyombo vinavyosimamia usalama barabarani kuchukua hatua dhidi ya watumiaji barabara wanaokiuka sheria za barabarani,” imeeleza taarifa hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Inahuzunisha sana.
RIP ndugu zetu.
Pole kwa ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu.

#AJALI HUTOKEA.

#TUTUMIE VYOMBO VYA MOTO KWA UMAKINI.
 
Pole sana majeruhi na wote walio poteza wapendwa wao.

Je, kuna mwenye majina ya marehemu au majeruhi?
 
Mungu azilaze roho za marehemu pema peponi, hakika maisha ya mwanadamu ni mafupi sana.
 
Mwendokasi wa mabasi sasaivi ni hatar sana.. kuna kuingia studio sikuizi yani mtu anakuondolea kengele hapo LATRa.

Nikiwa naenda mikoani mabas ni mwendo wa Mia alafu overtake ni popote.

Simbachawene umewasahau sana hawa watu.
 
Watu waliokuwa wakisafiri kutoka Ngara kwenda Bukoba na bus la Emirates

Wamepata ajari na watu 15 kufariki na wengine 20 kujeruhiwa

Kamanda wa police mkoa wa Kagera amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo pia wanamshikilia dereva wa bus la Emirates

Ambaye naye ni miongozi mwa watu waliojeruhiwa na anaongea kwa tabu sana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ametuma salaam za rambirambi kwa mkuu wa mkoa wa Kagera, huku akisisitiza watumiaji wa barabara wafuate sheria
 
Back
Top Bottom