New Habari 2006 Ltd ya Rostam haipeleki michango mifuko ya Jamii

Coloneli

Member
Aug 24, 2020
26
100
Salama wakuu,

Mimi ni mmoja wa waandishi wa zamani wa New Habari 2006 Ltd inayomilikiwa na Rostam Aziz. Nimefuatilia mafao yangu PPF kwa zaidi ya miaka saba sasa.

Lakini kila siku ninaambiwa bado michango haijapelekwa. Nikienda ofisini, watu wa utawala wanasema kampuni haina fedha, sasa najiuliza, hizi zinazokatwa
.
kwenye mishahara zinaenda wapi? Kuna watu hawajawekewa hela kwenye hii mifuko ya jamii tangu mwaka 2007 hadi leo.

Hii kampuni inaongozwa na Naibu Wazirii Hussein Bashe. Tunamuona Rostam anajisogezasogeza karibu na namba moja.

Tunamuomba namba moja amuambie atulipe fedha zetu, hata kama amesitisha uchapishaji wa magazeti kwa sasa, hilo halituhusu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom