Nikupe kisa kimoja. Wakati nipo shule pale New Delhi, nikawa nimezoena na wahindi wengi, wanachuo na lecturers.
Siku moja chuoni pale nikakutanishwa na Mhindi, ndg wa lecturer wangu. Mhindi yule katika maongezi yetu, alikuwa anatumia baadhi ya maneno ya Kiswahili.
Kumbe yule bwana amekaa Tanzania miaka mi4! Alikaa sana Arusha. Wacha ataje mitaa. Vitongoji. Hotel. Mabasi. Vyote vya Arusha.
Yule Mhindi akawa analazimisha urafiki, ukaribu na Mimi. Akafika point akanambia kwa shida yoyote ile, nimuambie yeye, na yeye atahakikisha sipati tabu yoyote ndani ya New Delhi. Nikaogopa.
Nikaogopa kwamba kwa maisha yetu Bongo, Mwanaume kumuambia Mwanaume mwenzie maneno kama hayo sio kitu kidogo. Ikabidi nianze kumkwepa. Nae akazidi kunfata fata. Nikimuuliza anachokitaka kwangu, anasema no, just friendship. Mmmh.
Ikabidi nimuambie wifi yako wa Kinaminibia niliekuwa nae class moja. Akanishauri turipot kwa uongozi wa chuo. Kituko. Kumbe bwana yule alizingua Tanzania ktk kampuni ya wahindi wenzie Arusha. Wakampiga chini. Viza sijui vibali vikaexpire. Akarudi India. Maisha India magumu. Analia usiku. Analia mchana. Kinachomliza ni Tanzania. Nimuunganishie mchongo wa kumrudisha Tanzania. Yaani alikuwa lazima arudi Tanzania.