Wakati fulani nilikua natafuta kifaa au mfumo ambao utanirahisishia kuchapisha kitu chochote bila kukimbizana na computer. Hii ilitokea hasa wakati nillipokuwa naandika hadithi fulani kwa ajili ya kipindi cha redio. Mwanzo nilikua natumia keyboard ya bluetooth pamoja na simu yenye bluetooth na application za simu zinazoruhusu kuandika text ndefu, (Nitaelezea hii zaidi ktk post nyingine). Nilikua naandika hadi kurasa 14 ndio nahamishia kwenye computer na inaonekana ningeweza kuandika hata zaidi.
Baadae niligundua kumbe simu yangu inaruhusu pia OTG (On The Go) cable fulani ambao unakua na Jike la USB kubwa kwa upande mmoja na micro USB kwa upande mwingine
hivyo nikaweza kutumia keyboard kubwa na mouse kwenye simu, kisha kuhamishia kwenye computer (nitaelezea pia zaidi ktk post nyingine)
Kuna wakati nilikua naangazaangaza kwenye mtandao nikaona kifaa kinachotwa NEO inayotengenezwa na kampuni inayoitwa ALPHASMART.
Nilijaribu kuiagiza Amazon pamoja na rafiki yangu. Bei ilikua poa sana maana ni used, tukaagiza mbili. Tulipitishia MyUs zikaja kwa FedEx. Kwa bahati mbaya zilipofika Bongo, zikashikiliwa customs kwa ajili ya kodi. Kwanza taratibu za kutoa customs na mambo ya kodi zikachukua muda mrefu, na gharama ikawa karibu mara mbili ya bei tuliyo nunulia (HOVYO KABISA).
Yenyewe ni kitu gani
Ni mashine ndogo ipo simpo, word processor ina full keyboard, screen ndogo na inatumia battery 3 za size AA. Unachapisha bila formatting kisha unahamishia kwenye computer kwa cable ya usb. Inaonekana mashine za mtindo huu zilianza kutengenezwa mwaka 2004 na mwaka 2013, zilisitishwa kutengenezwa. Awali ilitumika kwa matumizi ya shule za watoto wa shule za msingi kwa wenzetu mbele.
Baada ya kusitishwa kutengenezwa zimekua zikitafutwa na waandishi kwa matumizi yao ya kila siku. Waandishi na watumiaji wengine wananunua kama mtumba kwa bei inayoanzia dolari 29 na kuendelea kwenye masoko ya Amazon na Ebay, na watumiaji wengi wamekua wakitoa maoni chanya kuhusu kifaa hicho. Angalia video you tube. Au Pia video. Pia unaweza ku-search kwa neno Neo Alphasmart kwenye youtube na kuangalia.
Kwa kweli nimeipenda na nimetamani ningekua nayo tayari tangu wakati naandika hadithi. Hi ni kwasabau

- Baada ya kuchapisha naweza kuhamishia moja kwa moja kwenye computer, kwamba kazi inakwenda moja kwa moja kwenye computer na hivyo unapunguza muda ambao ningeutumia kwa kuanza kuandika kwenye karatasi au kuzubaa kwenye computer.
- Ina njia rahisi sana ya kuhamishia yale yaliyochapwa kwenda kwenye computer au kifaa kingine kwa kutumia waya wa usb, aina A-B nambao unapatikana kwenye printers nyingi. Niliipata yangu bila cable hiyo. Pia kwa kutumia cable ya OTG nimefaulu kuhamishia niliyochapa kwenye simu bila shida. Ikiwa imeunganishwa na computer kwa usb inaweza kutumika kama keyboard, na ni nzuri maana keyboard yake ni nzuri sana.
- Ina uwezo wa kuhifadhi kurasa 25 kwa kila file na ina jumla ya mafile 8 hivyo huweza kushikilia kurasa 200 bila wasiwasi
- Naweza kuhama mara moja kuhama toka file moja kwenda jingine kwa kubofya kitufe kimoja tu. Hivyo naweza kupanga kazi moja katika sehemu sehemu na kuzishughulikia sehemu hizo bila kuwa na mahangaiko sana.
- Katika kuiwasha na kuizima, inawaka na kuzima kwa haraka sio kama zilivyo computer ambazo zinatumia muda mrefu kuwaka. Inakaribia kama unavyowasha na kuzima calculator ya kawaida
- Matumizi yake ni rahisi kabisa, maana kuna vitufe vya kubonyeza tu kwa kufanikisha shughuli fulani ya pekee kama vile kufanya spell check, kuzima na kuwasha, kuhamia file jingine kuhamishia kazi kwenye computer au kifaa kingine, nk.
- Ninapoiwasha na kuendelea, kuandika inanipeleka moja kwa moja pale nilipoachia kwa haraka sana.
- Ni nyepesi, Ina uzito wa gram 815 Ni ngumu kabisa imetengenezwa kwa material isiyoruhusu kuharibika kwa urahisi. Ni portable inaniwezesa kwenda kufanya kazi kwenye mazingira mengine mbali na meza ya kazi.
- Screen yake ingawa ni ndogo sana na huwa inaonyesha wastani wa mistari minne 4 kwa mara moja, hata hivyo, inaniwezesha kuandika bila wasiwasi. Screen yake pia haitoi mwanga, na haina uakisi na hivvyo inamruhusu mtumiaji kutumika kwenye mazingira mbalimbali, isipokua katika giza.
- Screen yake ni rafiki wa macho. Sio hasa kwa kufanyia editting lakini kwa kuandikia. Ninapopata wazo fulani au ninaposoma kitu fulani unachohitaji kuongeza kwenye kazi yangu, nawasha Neo na kuchapisha moja kwa moja.
- Inatumia betri ndogo tatu za size ya AA na hizo hutumika kwa muda unaokadiriwa kuwa mwaka mmoja. Hivyo nina uhakika wa kwenda hata mahali ambapo hakuna umeme na kuendelea na kazi. Hata bila kuwa nca chembe ya wasiwasi kwamba betri itakata.
- Haina mambo mengine ya pembeni pembeni, kama yale tunavyoweza kuyafikia kwa kwenye computer na kwenye simu kama vile facebook, twitter, instagram, youtube ambazo mara nyingi huleta kishawishi na kupoteza utulivu wa kazi.
- Wakati wa kuhamishia kwenye computer, inafanya kazi kama keyboard ya kawaida. Kinachotokea ni kwamba inaonekana na chombo chochote ninachotumia kama keyboard ya kawaida. Hivyo nafungua program ambayo nataka kuhamishia maandishi yangu, kisha naclick pale ninapotaka maandishi yangu yaanzie, halafu nabonyeza kitufe cha send kisha yenyewe inaanza kuhamishia kama vile mtu anatype kwa kasi kubwa. Baada ya muda mfupi kazi yote imeshachapwa, ninachofanya sasa ni kusave na kuendelea na editting kwa kwenye computer.
- Ukubwa wake sio wa kuenea kwenye kabegi kadogo sana. Upana wa juu kabisa ni cm 19 Baada ya cm 10 kutoka juu unafika juu ya keyboard na upana hapo unakua cm 29. Na upana wa chini ni kama cm 30 hivi. Urefu ni cm 23.7. Keyboard peke yake ina urefu wa cm 11.1 na upana wa cm 27.7. Screen ni ndogo ina urefu wa cm 4 na upana wa cm 15 na ipo cm 3.5 kutoka juu. Unaweza kuona ni kubwa kidogo. Ina uzito wa Gram 825 sawa na kilo 0.825. Hatahivyo nimelinganisha na laptop ni zaidi ya kilo 3 na kuendelea nikaona uzito huo si kitu.
- Screen yake ni ndogo, kwa maandishi size ya kati inaweza kuonyesha hadi mistari 4
- Huwezi kufanya mambo mengi sana zaidi ya kuchapisha. Pia inaweza kufanya hesabu za kawaida pamoja vitu vingine vichache.
- Utaratibu wake wa kuhamishia kazi kwenye computer ni manual sana. Pengine ingefaa kuhamisha kwa mtindo wa file ingekua safi zaidi