Neno 'shangingi' ni kiswahili fasaha?

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
shangingi nnavyojua ni mwanamke-flamboyant, mmbeya na msengenyaji!(sina uhakika kama ni kiswahili fasaha), ikaja kwamba aina fulani ya magari yakaitwa mashangingi, sasa imekuwa kama ni neno oficial mpaka bungeni linatumika na bila shaka linaingia kwenye hansard za bunge, wataalam wa lugha tunaomba mtuelimishe!
 
so long as limekubaliwa na jamii basi litumika tu kama magari makubwa ya kifahari.

Enzi ztu huko Tanzania ile pegeot 404 ilikuwa iaitwa Guruwe.
 
ndiyo neno "shangingi" ni kiswahili sanifu kabisa lenye maana ya Mwanamke anayependa starehe sana na pili ni gari la kifahari.
 
Kama nakumbuka vizuri neno hili limetohorewa kutoka kabila la masai, masi wakisema "Sangiki" ikiwa na maana ya mwanamke mnene!
 
Shangingi lilitokana na nengo "Shangigi" la Kimasai likiwa na maana ya mwanamke ambaye hajaolewa; hivyo yuko kwenye soko la wanaume. Lilipoingizwa kwenye lugha ya kiswahili lilikuwa na maana hiyo hiyo ya mwanamke ambaye "yuko huru" kwenye soko la wanaume, lakini likawa limelenga zaidi wale wanaotembea na wanaume mbalimbali. Kwa wanawake wa namna hiyo walikuwa na tabia ya kuwa na ma-ta-ko manene, basi yale magari ya Nissan Patrol yaliyotoka mwanozni mwa miaka ya tisini nayo yaliitwa shangingi kwa sababu ya muundo wake ambapo fenders zake katika maeneo ya matairi zilikuwa kubw kama ma-ta-ko ya mwanamke wa ina ya shangingi wakati huo. Ni kutokana na hiyo extension ya kwenye Nissan Patrol baadaye magari ya Toyota Landcriuiser nayo yakajumuishwa kuitwa mashangingi. Leo huenda linatumika kwa hayo ma-Landcruiser tu, kwani nadhani umaarufu wa Nissan Patrol umefifia sana.
 
mh! historia ya jina hilo sikuifahamu kabla, huenda ni kweli
 
Back
Top Bottom