Neno nakupenda

Neno nakupenda

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,631
Reaction score
89,393
Kiuhalisia mwanamke na mwanaume ni watu waliotengana kimwili endapo hutakiana kimwili!

Mapenzi ni muunganiko wa kimhemko(kihisia) wa kimahaba baina ya mwanamke na mwanaume na ndio huwaunganisha wawili hao.
ktk neno nakupenda ni neno lenye nguvu ambalo huleta hali ya furaha,hukata huzuni na pia huleta faraja.. hulka ya mwanadamu hupenda kupendwa,hivyo anapoambiwa kuwa anapendwa hujisikia furaha hasa neno hilo anapolipata kwa mtu anaempenda.
neno hilo huamsha hali ama upendo uliokuwa umelala ama kufubaa hasa pale utakapomuonyesha mapenzi kwa vitendo yule umpendae!..

Ili kuendelea kuitunza afya ya mapenzi yenu neno "nakupenda" lisitoke ktk peo zenu za ubongo,sambamba na matendo.
Sekta ya mapenzi hujitegemea,mtafaruku hujitokeza pale utakapo mix na sekta nyengine..
Penda na pendwa kwa furaha na faraja ya maisha yako lkn usiutumie upendo wa mwenzako kuwa fimbo kwake,mheshimu anaekupenda maana amekuridhia.
 
'Wengi hupenda kulitamka kwa kiinglish☺☺☺
 
Stress za maisha zinafanya tusahau neno hili. Mjini kwenyewe mmepanga chumba na sebule, mna watoto wawili na dada wa kazi.
Wifi ameomba mkae na kijana wake amechaguliwa kidato cha tano hana uwezo wa kulipa hosteli.
Neno hili litakua la mwisho kwenye akili yako.
 
Stress za maisha zinafanya Tussaud’s maneno hili. Mjini kwenyewe mmepanga chumba na senile, mna watoto wawili na dada wa kazi.
Wifi ameomba mkae na kijana wake amechaguliwa kidato cha tano hana uwezo wa kulipa hosteli.
Neno hili litanies la mwisho kwenye akili yako.
Dr, inamaana leo simu yako imepata kigugumizi, au bado umelala?! Sijakupata kabisa.
 
Wengi hushindwa kulitamka kwa wapenzi wao kutokana na dhana kwamba ataona unamtania tu, na hasa kama anajua kuwa una mchepuko, hivyo njia pekee huona bora awe kimya. Atajuaje mpenzi wako kuwa unampenda? matendo yako mbele yake, yawe mazuri.
 
Back
Top Bottom