Street Hustler
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 2,268
- 4,490
Kama ilvyoandikwa
1π Kama vile inzi waliokufa huacha harufu mbaya kwenye manukato,
ndivyo upumbavu kidogo huzidi nguvu hekima na heshima.
2 π Moyo wa mwenye hekima huelekea kuume,
lakini moyo wa mpumbavu huelekea kushoto.
3π Hata anapotembea barabarani, mpumbavu hukosa ufahamu na kudhihirisha kwa kila mmoja
jinsi alivyo mpumbavu.
4π Kama hasira ya mtawala ikiwaka dhidi yako, usiache mahali pako, utulivu huweza kuzuia makosa mengi.
5π Kuna ubaya niliouona chini ya jua, aina ya kosa litokalo kwa mtawala:
6π Wapumbavu kuwekwa kwenye nafasi nyingi za utawala, hali matajiri wanashika nafasi za chini.
7π Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, wakati wakuu wakitembea
kwa miguu kama watumwa.
8π Yeye achimbaye shimo
aweza kutumbukia ndani yake,
yeyote abomoaye ukuta
anaweza kuumwa na nyoka.
9π Yeyote apasuaye mawe
inawezekana yakamuumiza,
yeyote apasuaye magogo
inawezekana yakamuumiza.
10π Kama shoka ni butu
na halikunolewa,
nguvu nyingi zinahitajika,
lakini ustadi utaleta mafanikio.
11π Nyoka akiuma kabla ya kuchezeshwa,
mchezeshaji hatahitajika tena.
12π Maneno yanayotoka kinywani mwa mtu mwenye hekima yana neema,
bali mpumbavu huangamizwa
na midomo yake mwenyewe.
13π Mwanzoni maneno yake ni upumbavu,
mwishoni ni wazimu mbaya,
14π naye mpumbavu huzidisha maneno.
Hakuna yeyote ajuaye linalokuja,
ni nani awezaye kueleza ni jambo gani
litakalotokea baada yake?
15π Kazi ya mpumbavu humchosha mwenyewe,
hajui njia iendayo mjini.
16π Ole wako, ee nchi ambayo mfalme wako alikuwa mtumwa
na ambayo wakuu wako hufanya karamu asubuhi.
17π Heri wewe, ee nchi ambayo mfalme wako ni wa uzao wenye kuheshimika,
na ambayo wakuu wako hula chakula kwa wakati unaofaa:
wao hula ili kupata nguvu na si kwa ajili ya ulevi.
18π Kama mtu ni mvivu, paa la nyumba huinama;
kutokana na mikono milegevu, nyumba huvuja.
19π Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko,
nao mvinyo hufurahisha maisha,
lakini fedha ni jawabu la mambo yote.
20π Usimshutumu mfalme hata ikiwa ni katika mawazo yako,
au kumlaani tajiri katika chumba chako cha kulala,
kwa sababu ndege wa angani wanaweza kuchukua maneno yako,
naye ndege anayeruka anaweza kutoa taarifa ya yale uliyosema.