Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,874
Neno la Nyongeza: Watanzania wapo kati yetu wenye tabia za ubaguzi; upo ubaguzi wa rangi, wa kidini na hata wa kihali. Ukitaka kuona ni kwa kiasi gani watu wetu wapo wabaguzi waulize wanafikiria nini kuhusu Wahindi wa Tanzania! Au nikumbushie kilichomkuta Richa Adhia? Wakati ule sikuona watu wengi wakisimama kumtetea kwa sababu ya kubaguliwa kwake. Au kuna watu wamesahau jinsi gani Wachagga wanatajwa tena wengine wanasema hivyo wakiamini wanasema kwa nia njema kabisa? Au nikumbushie mijadala yetu ya 2006-2007 wakati wengine tuliposimama kupinga ubaguzi dhidi ya Wachagga? Au nichokoze kwa kuulizia ubaguzi wa kidini? Au tumeshasahau mara moa hii kuwa hata wapo wanasiasa wadini wakubwa kabisa?
Ubaguzi ni ubaguzi; usije kulia ubaguzi kwa sababu wa karibu kabaguliwa! Pinga ubaguzi kwa sababu ubaguzi ni ubaguzi. Kwa sisi Nyerereist kilichotokea jana Zanzibar si kigeni; tayari kulikuwa na Uzanzibari na Uzanzibara.. hili mbona Baba wa Taifa alishalitabiri. Ukishasema fulani washughulikie wabaguzi wake na wale wa kwenu nao washughulikiwe! Ukishaamua kupinga ubaguzi kila unapojitokeza usiamue kupinga zaidi kule lakini siyo huku?
Au waliokuwa wanawaita wenzao "Fisiemu" walikuwa wanatumia lugha nzuri? Na nina uhakika wenyewe wanaamini wako sahihi!
Napiga vita ubaguzi - na nimefanya hivyo hata wengine walipokuwa kimya - lakini napinga zaidi ubaguzi wanaobagua wabaguzi wazuri na wabaya! Wanaoongozwa na kanuni ya "akibagua wa kwetu mbaya akibagua wa kwao mzuri".
MMM