Neno la mwisho la Kanumba kwa mama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno la mwisho la Kanumba kwa mama!

Discussion in 'Entertainment' started by Independent Voter, Apr 8, 2012.

 1. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maneno Ya Mwisho Ya Kanumba Kwa Mama Yake Mzazi

  [​IMG]
  Pichani ni Mama Kanumba anayeitwa Flora Mtegoa
  Wakati Taifa la Tanzania likiwa katika majonzi mara baada ya kupoteza moja kati ya vijana wake walio peperusha vyema ndani na nje ya mipaka pendera yake kupitia tasnia ya Filamu STEVEN KANUMBA, yafuatayo ni mahojiano kati ya mdau wa blog ya G. Sengo mkoani Kagera mwandishi wa habari anayeitwa Nicolaus Ngaiza, aliyoyafanya na Mama Kanumba (Flora Mtegoa).  Katika mahojiano yaliyofanyika leo majira ya saa nane mchana katika uwanja wa ndege Bukoba katika harakati za safari kuelekea jijini Dar es salaam ILIKUWA HIVI:-
  Nicolaus Ngaiza:- Mama unamwelezeaje Steven Kanumba katika kipindi cha uhai wake?
  MAMA:- Kanumba mtoto wangu mtiifu, rafiki yangu, mpendwa wangu, mtotowangu wa karibu na jana niliongea naye kwenye simu na alfajiri naambiwa kafa.

  Nicolaus Ngaiza:- Pengine alizaliwa sehemu gani mwaka gani?
  MAMA:- Kanumba alizaliwa tarehe 8/1/1984 mkoani Shinyanga, katika hospitali ya Government Shy.

  Nicolaus Ngaiza:- Baba yake yuko hai?
  MAMA:- Baba yake yuko hai yuko Shinyanga anaitwa Charles Kanumba

  Nicolaus Ngaiza:- Katika kipindi hiki kigumu unawambiaje watu wa Bukoba?
  MAMA:- Naomba waniombee kwani hali yangu siyo nzuri kwani niko katika kipindi hiki kigumu.

  Nicolaus Ngaiza:- Labda mama kijijini kwenu ni wapi?
  MAMA:- Mimi natoka Wilayani Muleba, kata ya Izigo, kijiji cha Itojo.

  Nicolaus Ngaiza:- Steven Kanumba sisi tunamjua kwa jina hilo jeh! hakuwa na jina la kinyumbani?
  MAMA:- Hakuwa na jina lolote la kinyumbani zaidi ya hilo Kanumba la Kisukuma yeye ni msukuma.

  Nicolaus Ngaiza:- Tungependa kujuwa neno la mwisho mlio weza kuzungumza pamoja.
  MAMA:- Aliniambia mama natuma nauli uje tuagane naondoka naenda Marekani, akiwa mwenye furaha, tunataniana...

  Nicolaus Ngaiza:- Labda aliwahi kukwambia ndoto zake katika maisha kwamba analenga kufanya nini?
  MAMA:- Yeye ndoto zake ni kuendeleza sanaa yake na ninashukuru alikuwa amefika mbali kisanaa.

  Nicolaus Ngaiza:- Labda kifamilia alikuwa ameoa au alikuwa na mtoto?
  MAMA:- Hajawahi kuoa na hakuwa na mtoto...
   
 2. L

  Lady G JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 517
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  jamani inasikitisha sana. pole mama kanumba, Mungu akupe faraja ktk kipindi hiki kigumu.
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hilo la hakua na mtoto ndio linauma zaidi.
   
 4. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Too sad!
   
 5. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  linauma nini? Acha mambo ya kiujima...kuwa na mtoto sio lazima kwa kipindi hiki kazi angefanya sa ngapi? Ndio maana mnazeek aharaka nyie wamama
   
 6. M

  Mabelana JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Lah! kila kitu kina wakati wake na mahali pake.
   
 7. M

  Mabelana JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
 8. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pole na mama kanumba ndio mipango ya mungu hiyo
   
 9. atubariki

  atubariki JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Inasikitisha sana kwa kuwa hakuwa na mke wala mtoto jamanii pole sana familia ya Steven Kanumba
   
 10. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Pole mama Kanumba ni kipindi kigumu katika maisha mungu mwenye rehema atakupa nguvu na kukufariji yeye ndie muweza wa kila kitu tumtegemee yeye. Amina
   
 11. T

  Twinky Senior Member

  #11
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 10, 2010
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mama Mungu akupe faraja kuu itokayo kwake. Ni kipindi kigumu sana
   
 12. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Uko sawa wewe? Au machungu ya msiba hayo.
   
 13. Wabogojo

  Wabogojo JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 355
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ama kwa hakika kifo cha kijana S.Kanumba si kwa familia ya Kanumba bali kwa Taifa la Tanzania kwa ujumla na itachukua muda mrefu kuziba pengo lake. Tulimpenda lakini kumbe MUNGU amempenda zaidi, Roho ya Marehemu SK ilale mahali mahali peponi. Amina!
   
 14. idea

  idea Senior Member

  #14
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 120
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ndugu hujui thamani ya mtoto! bora ungekaa kimya!
   
 15. newMbishi

  newMbishi Senior Member

  #15
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mtoto ana thamani kubwa sn ww, angekuwepo ingekua faraja kubwa kw mama Kanumba
   
 16. H

  Hilwa Halawa New Member

  #16
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah! inauma sana pole sana mama kanumba the Great. May his soul rest in peace.. My condolences 2 all.
   
 17. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Dah..ngoja tusubiri kidogo maana yule binti lulu kama mjamzito vile!!!!..
   
Loading...