Neno La Leo: Ngeleja's Last Dance!

Ndugu zangu,

Leo nilipata tabu sana hata kunyanyuka kitini kwenda haja ndogo wakati mjadala wa ripoti ya Kamati Teule ya Nishati na Madini ukiendelea. Niliufuatilia tangu mwanzo hadi mwisho.

Na mchana huu nikawachukua wanangu kwenda kupata mahitaji sokoni. Njiani nilisimama kununua karanga za kukaanga. Mwuuza karanga ni msichana asiyezidi miaka 16. Nilimwona akiwa amekaa juani anauza karanga zake.

Pakiti ya karanga ni shilingi mia. Nikatoa noti ya shilingi mia tano kununua paketi tatu za karanga. Nilimwangalia msichana yule akihangaika na chenji ya shilingi mia mbili.

" Hapana, acha tu!" Nilimwambia.

Mmoja wa watoto wangu akaniambia; " Baba, nina shilingi mia mbili nyingine mfukoni, ngoja nimwongezee."

Msichana yule ikamchanganya. Akachukua karanga nyingine paketi nne anipe. Alidhani, kuwa nimebadili mawazo, kuwa ile mia mbili niliyomwachia na hii ya sasa tunataka karanga nyingine.

Akashangaa na kushukuru alipofahamu kuwa tumenunua karanga za shilingi mia tatu na tumemwachia shilingi mia nne abaki nazo.

Niliondoka mahali pale nikitafakari sana juu ya umasikini wa watu wetu huku bado kumbukumbu ya mjadala wa bungeni leo Jumamosi ungali kichwani mwangu.

Nawafikria akina Ngeleja na Malima na ujasiri wao wa kifisadi wa kusaini malipo ya shilingi milioni nne kila mmoja kama ' Posho ya kukarimisha'. Nawafikiria akina Jairo na Luhanjo na ufisadi wa Wizara kuchangisha mamilioni ya shilingi na kupeleka watumishi zaidi ya mia mbili Dodoma kufanikisha uwasilishaji wa bajeti ya Wizara.

Maneno ya Mheshimiwa Lembeli yananijia; " Ndugu yangu Ngeleja jiuzuru!". Na hakika, wabunge wengi niliowasikia leo wamezungumza kwa uchungu juu ya kashfa na aibu hii kwa taifa akina akina Ngeleja na wenzake wametuletea.

Nawapongeza sana wabunge wetu kwa ujasiri waliouonyesha leo. Nami kama raia tu nasema; walichofanya akina Ngeleja na wenzake ni uhalifu na hakuna kingine cha wao kufanya sasa bali kuachia ngazi ili kulinda heshima zao, ya Rais na nchi yetu. Na juu ya hapo wafikishwe mahakamani.

Na kwa mtani wangu Ngeleja kama ni disco leo awe amecheza ' Last Dance!'. Kumwona Ngeleja Bunge lijalo akiwa kama Waziri si kingine bali ni matusi kwa WaTanzania.

Nahitimisha.

Maggid Mjengwa,
Iringa,
Yote uloandika mkuu wangu yanaweza tafsriwa vyovyote.. Sasa turudi kwenye karanga, mimi nikisema zile fedha ulompa yule msichana zilikuwa na maana ya kumhonga utakubali au?.. Binafsi, hili swala la Ngeleja na Jairo ni la kisiasa zaidi kwa sababu fedha humwagwa bungeni na sii jambo geni isipokuwa limeletwa kama lile la Richmond.
Mikataba feki nchini ni mingi mno kiasi kwamba huo wa Richmond ulikuwa tu siku za Lowassa zimewadia na they wanted him out. Unataka kukomesha Ufisadi na mikataba feki unapitia mikataba yote kujua ipi ilofanana na ile ya Richmond na hapa pia tunatakiwa kutazama matumizi ya wizara zote ktk ufisadi kama huu ku lobby wabunge, ndio tutapata suluhu na sio kufukuza watu kazi hali mchezo ulikuwepo na unaendelea.

Kwa mjumla wa yote haya ni mapambano ya mafisadi kwa sababu uwanja wa kufisadi umekuwa mdogo na hata kama Ngeleja ataondolewa madarakani lakini bado Papa wapo baharini (list of shame). Tunachokifanya ni kumwondoa pool hili na kumwamishia pool jingine..

Ushauri wangu usipende kutoa msaada wa fedha kwa watoto wa kike, Mpeleke shule utamsaidia zaidi..
 
Maggid umeanza vyema kabisa lakini umemalizia kwa ushabik na hoja imekuwa ni dhaifu x 2 (mara mbili).

Kwanza, huwa hatutowi sadaka ya shillingi 200 halafu tukatangaza, halafu umeshajiuliza? ikiwa wewe uweze kutoa mia 200 na mwanao (ambae nadhani bado ni mwanafunzi) katika vi "pocket money" vyake nae aweze kutowa 200 na uje humu kumtangazia kuwa anazo za kutumia kama zako, jee ulikuwa unatuonesha kuwa unazo za ziada au kuwa wewe na mwanao ni wakarim sana?

Pili, huyo uliyemkuta anauza karanga ni bora mara elfu kuliko wale ambao ukipita Ohio utawakuta wakijiuza, au wale wanaosimama "traffic lights" wakiomba omba na wazee wao pembeni wanawachombeza.

Kwa mimi, ningekuona wa maana sana ungeleta hoja nyingne kabisa kwa uliyoyasikia bungeni na si kwa kumbeza au kumuonea simanzi uliyemkuta anauza karanga, huyo ni mfanya biashara, vyovyote ilivyo alikuwa kazini na hapo ni pakusifia na ungekuwa na huruma nae sana ungemkirim kwa kumpeleka chuo cha ujasiriamali au kumuongeza mtaji na si kumpa viji mia mbili vyako na vya mwanao kisha uvitolee mfano humu JF, hiyo ni kutokuwa na nadharia ndefu.

"Give a man a fish and you feed him for a day. Teach a man to fish and you feed him for a lifetime." Chinese Proverb.

Wasio nacho si vyema kuwatumia kwa kuwatolea mifano wapo wengi sana na wanahitaji msaada zaidi ya 200 za "keep change".

Naomba tumia kalamu yako vizuri "Pen is mightier than the sword".

Qur'an 68:1 Nun. By the Pen and the (Record) which (men) write,-
"Noon waalqalami wama yasturoona
"

Hilo neno la mwisho "yasturoona" si kuandika tu, na vipi wanastiri katika maandiko yao.

Kupokea Ngeleja (Waziri) pesa za dhifa million 4 kama zilikuwepo kwenye bajeti, ziliombwa na kupitishwa kihalali bungeni, sioni kuwa ni kosa, kinyume cha hapo (ubadhirifu) ni kosa tena kubwa sana. Millioni nne si kubwa hivyo kwa wadhifa na dhifa za Waziri. Ni kubwa sana pale tu zitakapotumika kujinufaisha binafsi au kinyume na zilivyoombwa.

Naomba nielewe vizuri, sitetei makosa nachelea ukiitumia vibaya kalamu utajikuta unafanya kosa katika kujenga hoja za kukosowa.

maneno mengi umeandika, ila yote ni Pumba tena mbichi.
 
Mkuu, kwenye hii thread hujaona sehemu yeyote palipoandikwa noti ya shilingi mia tano,
Unauliza au unatoa positive statement? Matokeo ya mfumo mbovu wa elimu yetu. Hakuna anaeweza kubisha kwamba ukimwachia mtu 400/= "abaki nazo," ukachukua karanga zenye thamani ya 300/= maana yake umetoa bakhshish ya 100/= tu.

tumenunua karanga za shilingi mia tatu na tumemwachia shilingi mia nne abaki nazo.

Unauliza au unatoa positive statement? Matokeo ya mfumo mbovu wa elimu yetu. Hakuna anaeweza kubisha kwamba ukimwachia mtu 400/= "abaki nazo," ukachukua karanga zenye thamani ya 300/= maana yake umetoa bakhshish ya 100/= tu.

Ubishi uko wapi jamani? Majjid kasema alitoa noti ya Tsh 500 akanunua karanga za mia 300, akamwachia chenji na mwanaye akamuongezea binti yule 200.. Sasa kinachowashinda kuelewa aliacha 400 ni kipi?
 
Dawa pekee ya hawa watu ni kuwanyima kura kuanzia Udiwani, UBUNGE na hata Urasi. Maana kwa njia nyingine wanaendelea kutetewa na kulindwa na Viongozi wenye madaraka makubwa katika nchi hii. Mgao mpaka leo Upo na walitudanganya kuwaumeisha.
 
Ndugu zangu,

Leo nilipata tabu sana hata kunyanyuka kitini kwenda haja ndogo wakati mjadala wa ripoti ya Kamati Teule ya Nishati na Madini ukiendelea. Niliufuatilia tangu mwanzo hadi mwisho.

Na mchana huu nikawachukua wanangu kwenda kupata mahitaji sokoni. Njiani nilisimama kununua karanga za kukaanga. Mwuuza karanga ni msichana asiyezidi miaka 16. Nilimwona akiwa amekaa juani anauza karanga zake.

Pakiti ya karanga ni shilingi mia. Nikatoa noti ya shilingi mia tano kununua paketi tatu za karanga. Nilimwangalia msichana yule akihangaika na chenji ya shilingi mia mbili.

” Hapana, acha tu!” Nilimwambia.

Mmoja wa watoto wangu akaniambia; ” Baba, nina shilingi mia mbili nyingine mfukoni, ngoja nimwongezee.”

Msichana yule ikamchanganya. Akachukua karanga nyingine paketi nne anipe. Alidhani, kuwa nimebadili mawazo, kuwa ile mia mbili niliyomwachia na hii ya sasa tunataka karanga nyingine.

Akashangaa na kushukuru alipofahamu kuwa tumenunua karanga za shilingi mia tatu na tumemwachia shilingi mia nne abaki nazo.

Niliondoka mahali pale nikitafakari sana juu ya umasikini wa watu wetu huku bado kumbukumbu ya mjadala wa bungeni leo Jumamosi ungali kichwani mwangu.

Nawafikria akina Ngeleja na Malima na ujasiri wao wa kifisadi wa kusaini malipo ya shilingi milioni nne kila mmoja kama ’ Posho ya kukarimisha’. Nawafikiria akina Jairo na Luhanjo na ufisadi wa Wizara kuchangisha mamilioni ya shilingi na kupeleka watumishi zaidi ya mia mbili Dodoma kufanikisha uwasilishaji wa bajeti ya Wizara.

Maneno ya Mheshimiwa Lembeli yananijia; ” Ndugu yangu Ngeleja jiuzuru!”. Na hakika, wabunge wengi niliowasikia leo wamezungumza kwa uchungu juu ya kashfa na aibu hii kwa taifa akina akina Ngeleja na wenzake wametuletea.

Nawapongeza sana wabunge wetu kwa ujasiri waliouonyesha leo. Nami kama raia tu nasema; walichofanya akina Ngeleja na wenzake ni uhalifu na hakuna kingine cha wao kufanya sasa bali kuachia ngazi ili kulinda heshima zao, ya Rais na nchi yetu. Na juu ya hapo wafikishwe mahakamani.

Na kwa mtani wangu Ngeleja kama ni disco leo awe amecheza ’ Last Dance!’. Kumwona Ngeleja Bunge lijalo akiwa kama Waziri si kingine bali ni matusi kwa WaTanzania.

Nahitimisha.

Maggid Mjengwa,
Iringa,

Mhehe umeamdia vyema . sikio la kufa unalijua?
 
Mjengwa acha udalali wa uandishi, safari hii umetumwa na JM?
 
Huu ndio mwisho wa huyu kijana Ngeleja.Mungu hadhikiwi hata siku moja.Dhambi ya kuwanyanyasa hao yatima huko Mwanza itakugharimu.Hiyo nyumba ni mali yao hao vijana,kwa nini uwatese kwa ajili ya mali yao.wewe umejenga umewakuta hapo,kama unaona nyumba yao inastahili kuvunjwa ili upate parking ya magari yako kwa nini usingeongea nao uwalipe kuliko ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu kufanywa na mwanasheria km ww.Matokeo yake umeshindwa na kuaibika.Yaani mmemaliza rasilimali za taifa ss mnataka kuchukua kwa nguvu mali za yatima,wewe na diwani wako mnakidhalilisha chama, naomba mjengwa tuwasiliane nikupe details uandike makala juu ya ufisadi wa huyu mtu.Kitendo cha kiongozi kunyanyasa yatima kutokana na mali yao kamwe hakivumiliki hii ni laana itamwandama daima
 
Nilikuwa nafanya utafiti ni kwa nini division zero zimekuwa nyingi siku hizi, kumbe hata hapa JF wapo zero brain wengi, kwahiyo mia2 + mia2= mia1!?

Hao ni walewale ambao hawasomi between the lines!
 
Mleta maada amehusianisha na maisha ya kwake, mnaosema oooh sh. 100 si ya kuwekea uzi humu, hapa Dar mbona kuna vijana hadi wanachomana visu kwa ajili ya sh. 100, namkubali Maggid, kwakuwa ukisoma maandiko yake unatakiwa kufikiri. Kwa ujumla Ngeleja hawezi kwa kujiuzulu kuna nguvu kubwa iko nyuma yake, ikumbukwe Ngeleja alikuwa mwanasheria huko Vodacom kwenye kampuni ambayo Rostam ana hisa za kutosha na baadaye amepewa uwaziri wa Nishati na madini ambako Rostam na genge lake including Kikwete walikuwa wameweka mirija ya kunyonya jasho la Tz, je Ngeleja wakimtosa akiamua kusema itakuwaje? naamini hata Lowasa leo anajuta kwanini alijiuzulu
 
Kila jambo na wakati wake, Ngele jaa asipojiuzulu mambo yanapozidi kuendelea kuwa hovyo ndivyo tunapotengeneza njia nzuri zidi ya mabadilko ya lazima pale ambapo ya kidemokrasia na hiyari yatakaposhindikana.
 
Mbona ni wakristo watupu? yaani hapo Adam Malima hausika? au ndio mfumo Bakwata unasimikwa nchini? tunahitaji kauli ya maaskofu, huu ni uonevu dhidi ya wakristo.

Angeyasema Faiza angeambiwa mdini. mnapokosa hoja kutaka kuchakachuwa ndipo mnapokuwa kweli ma "great thinkers" keep it up.
 
Back
Top Bottom