Ni kweli kabisa, aliacha 400/= "abaki nazo," uko sawa.Sasa kinachowashinda kuelewa aliacha 400 ni kipi?
tumenunua karanga za shilingi mia tatu na tumemwachia shilingi mia nne abaki nazo.
Pamoja na yatakayowatokea kiserikali, Mungu huyu wa Yakobo hatawaacha bila kuwaadhibu mabaradhuli hawa wawili pamoja na huyoMsanifu wao wa mpango huu i.e. Jairo. Halafu fedha nyingi hizi zinaishia kuhonga vimada laana wakubwa hawa.Ndugu zangu, Leo nilipata tabu sana hata kunyanyuka kitini kwenda haja ndogo wakati mjadala wa ripoti ya Kamati Teule ya Nishati na Madini ukiendelea. Niliufuatilia tangu mwanzo hadi mwisho. Na mchana huu nikawachukua wanangu kwenda kupata mahitaji sokoni. Njiani nilisimama kununua karanga za kukaanga. Mwuuza karanga ni msichana asiyezidi miaka 16. Nilimwona akiwa amekaa juani anauza karanga zake. Pakiti ya karanga ni shilingi mia. Nikatoa noti ya shilingi mia tano kununua paketi tatu za karanga. Nilimwangalia msichana yule akihangaika na chenji ya shilingi mia mbili. Hapana, acha tu! Nilimwambia. Mmoja wa watoto wangu akaniambia; Baba, nina shilingi mia mbili nyingine mfukoni, ngoja nimwongezee. Msichana yule ikamchanganya. Akachukua karanga nyingine paketi nne anipe. Alidhani, kuwa nimebadili mawazo, kuwa ile mia mbili niliyomwachia na hii ya sasa tunataka karanga nyingine. Akashangaa na kushukuru alipofahamu kuwa tumenunua karanga za shilingi mia tatu na tumemwachia shilingi mia nne abaki nazo. Niliondoka mahali pale nikitafakari sana juu ya umasikini wa watu wetu huku bado kumbukumbu ya mjadala wa bungeni leo Jumamosi ungali kichwani mwangu. Nawafikria akina Ngeleja na Malima na ujasiri wao wa kifisadi wa kusaini malipo ya shilingi milioni nne kila mmoja kama Posho ya kukarimisha. Nawafikiria akina Jairo na Luhanjo na ufisadi wa Wizara kuchangisha mamilioni ya shilingi na kupeleka watumishi zaidi ya mia mbili Dodoma kufanikisha uwasilishaji wa bajeti ya Wizara. Maneno ya Mheshimiwa Lembeli yananijia; Ndugu yangu Ngeleja jiuzuru!. Na hakika, wabunge wengi niliowasikia leo wamezungumza kwa uchungu juu ya kashfa na aibu hii kwa taifa akina akina Ngeleja na wenzake wametuletea. Nawapongeza sana wabunge wetu kwa ujasiri waliouonyesha leo. Nami kama raia tu nasema; walichofanya akina Ngeleja na wenzake ni uhalifu na hakuna kingine cha wao kufanya sasa bali kuachia ngazi ili kulinda heshima zao, ya Rais na nchi yetu. Na juu ya hapo wafikishwe mahakamani. Na kwa mtani wangu Ngeleja kama ni disco leo awe amecheza Last Dance!. Kumwona Ngeleja Bunge lijalo akiwa kama Waziri si kingine bali ni matusi kwa WaTanzania. Nahitimisha.Maggid Mjengwa,Iringa,
Ubishi uko wapi jamani? Majjid kasema alitoa noti ya Tsh 500 akanunua karanga za mia 300, akamwachia chenji na mwanaye akamuongezea binti yule 200.. Sasa kinachowashinda kuelewa aliacha 400 ni kipi?
Ni kweli kabisa, aliacha 400/= "abaki nazo," uko sawa.
Akaondoka na karanga zenye thamani ya 300/=. Hivyo aliacha bakhshish ya 100/= tu. Sasa ukimpa mtu 100/= bure ukakimbia kuja kuianzishia thread nashangaa cha ajabu katika 100/= ni kipi.
Kama "jumla ya ulichokiacha kikawa mia nne" na ukaondoka na vifuko vitatu vya karanga vya 100/= kila kimoja, basi umetoa bakhshish ya shilingi 100/= tu.na kufanya jumla ya ulichokiacha kikawa mia nne!
tumenunua karanga za shilingi mia tatu na tumemwachia shilingi mia nne abaki nazo.
Kama "jumla ya ulichokiacha kikawa mia nne" na ukaondoka na vifuko vitatu vya karanga vya 100/= kila kimoja, basi umetoa bakhshish ya shilingi 100/= tu.
Umesema tena na kuzidi kusisitiza, muuzaji amebaki na jumla ya shilingi mia nne!
Maggid, unasomwa na maelfu ya Watanzania, umeanza kuwaandikia si jana, si juzi, unashindwaje kuanisha hadithi ya hesabu za karanga tatu hata kama Kiswahili si lugha ya asili au mazoea yako ya Iringa? Angekuwa mtu wa ajabu ajabu mwingine humu isingekuwa tatizo, lakini kwa wewe kuhangaika kunyoosha maelezo ya salio la manunuzi ya karanga ni fedheha na dhihirisho la ubovu wa mfumo wa elimu yetu.
Mbona ni wakristo watupu? yaani hapo Adam Malima hausika? au ndio mfumo Bakwata unasimikwa nchini? tunahitaji kauli ya maaskofu, huu ni uonevu dhidi ya wakristo.
Kikwete anasakamwa kutokana na uislamu wake by BAKWATA.Haya sasa 500-300+200=UDINI.
Ubishi uko wapi jamani? Majjid kasema alitoa noti ya Tsh 500 akanunua karanga za mia 300, akamwachia chenji na mwanaye akamuongezea binti yule 200.. Sasa kinachowashinda kuelewa aliacha 400 ni kipi?