Neno La Leo: Ngeleja's Last Dance! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Ngeleja's Last Dance!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Nov 19, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]Ndugu zangu, [/FONT]

  [FONT=&amp]Leo nilipata tabu sana hata kunyanyuka kitini kwenda haja ndogo wakati mjadala wa ripoti ya Kamati Teule ya Nishati na Madini ukiendelea. Niliufuatilia tangu mwanzo hadi mwisho.[/FONT]

  [FONT=&amp]Na mchana huu nikawachukua wanangu kwenda kupata mahitaji sokoni. Njiani nilisimama kununua karanga za kukaanga. Mwuuza karanga ni msichana asiyezidi miaka 16. Nilimwona akiwa amekaa juani anauza karanga zake.[/FONT]

  [FONT=&amp]Pakiti ya karanga ni shilingi mia. Nikatoa noti ya shilingi mia tano kununua paketi tatu za karanga. Nilimwangalia msichana yule akihangaika na chenji ya shilingi mia mbili.[/FONT]

  [FONT=&amp]" Hapana, acha tu!" Nilimwambia.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mmoja wa watoto wangu akaniambia; " Baba, nina shilingi mia mbili nyingine mfukoni, ngoja nimwongezee."[/FONT]

  [FONT=&amp]Msichana yule ikamchanganya. Akachukua karanga nyingine paketi nne anipe. Alidhani, kuwa nimebadili mawazo, kuwa ile mia mbili niliyomwachia na hii ya sasa tunataka karanga nyingine.[/FONT]

  [FONT=&amp]Akashangaa na kushukuru alipofahamu kuwa tumenunua karanga za shilingi mia tatu na tumemwachia shilingi mia nne abaki nazo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Niliondoka mahali pale nikitafakari sana juu ya umasikini wa watu wetu huku bado kumbukumbu ya mjadala wa bungeni leo Jumamosi ungali kichwani mwangu.[/FONT]

  [FONT=&amp]Nawafikria akina Ngeleja na Malima na ujasiri wao wa kifisadi wa kusaini malipo ya shilingi milioni nne kila mmoja kama ' Posho ya kukarimisha'. Nawafikiria akina Jairo na Luhanjo na ufisadi wa Wizara kuchangisha mamilioni ya shilingi na kupeleka watumishi zaidi ya mia mbili Dodoma kufanikisha uwasilishaji wa bajeti ya Wizara.[/FONT]

  [FONT=&amp]Maneno ya Mheshimiwa Lembeli yananijia; " Ndugu yangu Ngeleja jiuzuru!". Na hakika, wabunge wengi niliowasikia leo wamezungumza kwa uchungu juu ya kashfa na aibu hii kwa taifa akina akina Ngeleja na wenzake wametuletea.[/FONT]

  [FONT=&amp]Nawapongeza sana wabunge wetu kwa ujasiri waliouonyesha leo. Nami kama raia tu nasema; walichofanya akina Ngeleja na wenzake ni uhalifu na hakuna kingine cha wao kufanya sasa bali kuachia ngazi ili kulinda heshima zao, ya Rais na nchi yetu.[/FONT] Na juu ya hapo wafikishwe mahakamani.

  [FONT=&amp]Na kwa mtani wangu Ngeleja kama ni disco leo awe amecheza ' Last Dance!'. Kumwona Ngeleja Bunge lijalo akiwa kama Waziri si kingine bali ni matusi kwa WaTanzania.[/FONT]

  [FONT=&amp]Nahitimisha.

  Maggid Mjengwa,
  Iringa,
  [/FONT]
   
 2. GodfreyTajiri

  GodfreyTajiri JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 846
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  naona sisi tushazoea "kutukanwa". sitashangaa huyo ngeleja
  kutocheza hiyo dansi ya mwisho na hakuna kitakachotekea
  zaidi ya kupokea "matusi" mengine. inasikitisha sana. loh!
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nchi ya kitu kidogo hii ndugu Mjengwa.

  Kushangaa mtashangaa sana lakini Ngeleja ataendelea kuwa waziri wa Nishati na madini.

  Hii wizara ilimshinda siku nyingi, hata aliyemteua anajua, lakini kwa kuwa mawaziri wanawekwa strategically, Ngeleja yuko pale kwa sababu maalum anazozijua aliyemteua, angekuwa ni wa kuwajibika leo angetangaza kujiuzulu kwa jinsi wabunge walivyomkomalia.

  Hata hivyo nani kasema Kujiuzulu na kufikishana mahakamani ni utamaduni wetu watanzania?
   
 4. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Hussein Mwinyi alisema hawezi kujiuzulu na bado hakujiuzulu,ngoja tuendelee kutukanwa Tanzania lakini..
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,597
  Trophy Points: 280
  Hata Ngeleja alishakataa kujiuzulu na kudai tatizo la umeme yeye kalikuta na ni la Serikali yote. Na kwa kuwa anafahamu kwamba fisadi Rostam kamkingia kifua na fisadi Rostam kamuweka mfukoni Kikwete basi hana wasiwasi ataendelea kuwepo pale Nishati na Madini hadi 2015 labda kama Kikwete atabwaga manyanga.
   
 6. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mjengwa ni wengi wametaka Ngeleja ajiuzulu lakini hebu ona unafiki wa Shelukindo yeye ndiye aliyewasilisha ile barua halafu leo hii anamkingia kifua asijiuzulu!!!!!
  Ni unafiki huu utakampa nguvu Ngeleja asijiuzulu. Sitegemei miujiza mpaka hapa.
   
 7. Mkasika

  Mkasika JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  No one will ever try to resign from this Government! Instead they say they are fighting from within............and the big reason is that political seat in Tanzania is so sweet it comes with goods in handy.....i.e free top range cars, drivers, bodyguards and then for the corrupt minded its an highway to their corrupt practices. So instead of choosing to use his own car, fuel, driver, wear and tear on Tanzanian roads they prefer to hang on and keep complaining through public (media), unnecessary press conferences etc. All this makes them say i better from within........anyway that is our Tanzania, shamba la bibi.
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Haah! kumbe ni Mggid Mjengwa, napita tu hapa hapanifai. ile bahasha yako waliokupa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana imekwisha ? naona unaanza kuonea gere ulaji wa wenzako.
   
 9. r

  rombo Member

  #9
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :eyebrows: mimi nimwanaCCM lakini katika hili kama ngeleja hatajiuzulu,ntaihama hiki chama rasmi na ntamtukana waziwazi.
   
 10. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu Mjengwa, Narudia tena dharau ya ccm na viongozi wake kwa watanzania ni hali ya juu kiasi kwamba hakuna wa kujiuzuru ndugu zangu hawana aibu tena wala nini wao wameamua kula nchi kuponda mali za maskini bila aibu so sitajii yeyote kujiuzuru sana sana natarajia Jairo kurejea ofisini soo.
   
 11. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 80
  Umemwachia mia nne abaki nazo, na umenunua karanga za mia tatu.

  Kwa hiyo umetoa tip ya shilingi mia. Sio mbaya, ubarikiwe. Lakini tip ya shilingi mia sio ya kuianzishia thread!
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nafanya utafiti ni kwa nini division zero zimekuwa nyingi siku hizi, kumbe hata hapa JF wapo zero brain wengi, kwahiyo mia2 + mia2= mia1!?
   
 13. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Tanzania yetu amani, hivi vingine vya kujiuzuru siyo desturi yetu.
   
 14. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #14
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Last dance ya Ngeleja inaletwa na muuza karanga?.
   
 15. mkokoteni

  mkokoteni Member

  #15
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Sasa ndo nimejua kuwa wapotoshaji wa umma wako serikalini. Katibu mkuu kiongozi ameupotosha umma.

  Control and Auditor General, amechafuka. Wabunge walitakiwa waairishe National Board of Accountants and Auditors (NBAA) Kumchunguza bwana Utoh, kwa kukiuka maadili ya NBAA. Nawakijiridhisha, ni lazima afutiwe usajili wake kwani alichofanya ni ufisadi na amedhalilisha taaluma. Shame on him
   
 16. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  embu jaribu ku-spare hata dakika moja kusoma main post kabla ya kukurupuka watu wengine bwana.
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Maggid can not stop amazing rev Fr Masa!
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Yes my man are u there? uliwaona jana wapenda ubwabwa na vipedo vyao wakati wa porojo za Mkwerre?
   
 19. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  jamani mtoa thread katoa ujumbe kwa mtiririko wa hadithi ya ukweli aliyoiona ukicompare maisha ya kimaskini ya binti muuza karanga na wa akina Jairo na Kafumu(both under Ngeleja Roof) wanaopokea posho ndefundefu kwa siku
   
 20. MBUFYA

  MBUFYA JF-Expert Member

  #20
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Karibu sana kwenye chama chetu.
   
Loading...