Maggid umeanza vyema kabisa lakini umemalizia kwa ushabik na hoja imekuwa ni dhaifu x 2 (mara mbili).
Kwanza, huwa hatutowi sadaka ya shillingi 200 halafu tukatangaza, halafu umeshajiuliza? ikiwa wewe uweze kutoa mia 200 na mwanao (ambae nadhani bado ni mwanafunzi) katika vi "pocket money" vyake nae aweze kutowa 200 na uje humu kumtangazia kuwa anazo za kutumia kama zako, jee ulikuwa unatuonesha kuwa unazo za ziada au kuwa wewe na mwanao ni wakarim sana?
Pili, huyo uliyemkuta anauza karanga ni bora mara elfu kuliko wale ambao ukipita Ohio utawakuta wakijiuza, au wale wanaosimama "traffic lights" wakiomba omba na wazee wao pembeni wanawachombeza.
Kwa mimi, ningekuona wa maana sana ungeleta hoja nyingne kabisa kwa uliyoyasikia bungeni na si kwa kumbeza au kumuonea simanzi uliyemkuta anauza karanga, huyo ni mfanya biashara, vyovyote ilivyo alikuwa kazini na hapo ni pakusifia na ungekuwa na huruma nae sana ungemkirim kwa kumpeleka chuo cha ujasiriamali au kumuongeza mtaji na si kumpa viji mia mbili vyako na vya mwanao kisha uvitolee mfano humu JF, hiyo ni kutokuwa na nadharia ndefu.
"Give a man a fish and you feed him for a day. Teach a man to fish and you feed him for a lifetime." Chinese Proverb.
Wasio nacho si vyema kuwatumia kwa kuwatolea mifano wapo wengi sana na wanahitaji msaada zaidi ya 200 za "keep change".
Naomba tumia kalamu yako vizuri "Pen is mightier than the sword".
Qur'an 68:1 Nun. By the Pen and the (Record) which (men) write,-
"Noon waalqalami wama yasturoona"
Hilo neno la mwisho "yasturoona" si kuandika tu, na vipi wanastiri katika maandiko yao.
Kupokea Ngeleja (Waziri) pesa za dhifa million 4 kama zilikuwepo kwenye bajeti, ziliombwa na kupitishwa kihalali bungeni, sioni kuwa ni kosa, kinyume cha hapo (ubadhirifu) ni kosa tena kubwa sana. Millioni nne si kubwa hivyo kwa wadhifa na dhifa za Waziri. Ni kubwa sana pale tu zitakapotumika kujinufaisha binafsi au kinyume na zilivyoombwa.
Naomba nielewe vizuri, sitetei makosa nachelea ukiitumia vibaya kalamu utajikuta unafanya kosa katika kujenga hoja za kukosowa.