udaku ni udaku... na kama kawaida ya hii forum, udaku huwa unapewa hadhi inayostahili - jina la udaku.
Angalao Kikwete ana guts za kuuacha Lowassa ajiingize kitanzini...vipi Dr Slaa ni lini ameweza kusimama mbele ya maslahi binafsi ya Mbowe????
Second, Kuhusu ujuvi ama uledi wa masuala ya Utawala nina uhakika asilimia 100 kuwa Kikwete anamzidi Dr Slaa.
Ofcourse Kikwete ana advantage ya kupewa nafasi ndani ya mfumo kujifunza kwa muda mrefu
lakini ukiangalia mapambano na sasa majigambo, vikwerombwezo na mikwara ya Dr Slaa, kimoja kiancho onekana ni kuwa hajatumia muda wake kujifunza vya kutosha namna serikali ama utawala unavyofanya kazi......
ejea suala la NUSU YA MAAFISA WA USALAMA WA TAIFA KU-REPORT KWAKE.....Ama lile la kuhusisha dili la matrekta kutoka India na kumhusisha Shimbo kama binafsi wakati ukweli ni kuwa ni shughuli waliyopewa jeshi ambalo miaka yote mnasema litumike katika maswala ya maandeleo haswa sasa wakati hakuna vita....
Bado lile suala la mfumo wa kibenki wa TISS ambalo mlidai kuwa ni fedha zilizokuwa zikpelekwa Idara ya Usalama...na mengine mengi ambayo sitayataja hapa kwa maslahi ya maendeleo ya demokrasia nchi...
Sawa kama udaku we kaa kimya lakini wahusika wanajua ukweli wake.....na wewe kama hujui hali ilivyo nyumbani kwako basi fungua akili ujifunze zaidi...
Imekugusa enhh....well ndio JF hiyo, we all dare to talk...
Usiku mwema....huku kwetu ni wakati kulala sasa..
Nilidhani utanibishia kuwa Ansbert Ngurumo, mshauri wa Dr Slaa masuala ya habari hahusiki na kampuni iliyotaka kuratibu mdahalo huo unaleta kusema watu vilaza kama vile wewe umetuanyesha credentials za u-kipanga wako tayari...
By the way, haya ya Ansbert mbona nilishayaongelea kabla hata CCM hawajaanza kuyaongelea....please I have my independent mind and dont need anybody's talking points to use my mind...
While Jenerali anaweza kuwa sio mshabiki wa Slaa lakini kamwe hawezi kuwa neutral when it comes to CCM...
Yaani, Kikwete ana guts za Lowassa ajiingize kitanzani? alikuwa na uchaguzi gani mwingine? Hakuwa tayari kumwajibisha yeye mwenyewe na hakuwa na ujasiri wa kumtetea. Kutokufanya jambo linalokupa siyo ujasiri ni woga.
Aah wapi! Yaani kweli Kikwete ana ujuzi na uledi wa masuala ya utawala? Really? kaonesha vipi na wapi? Kiongozi aliyeshindwa kusafisha Benki Kuu na badala yake kumung'unya maneno? aliyeshindwa kushughulikia suala la Meremeta, aliyeshindwa kurenegotiate mikataba ya nishati na madini na ambaye chini yake mfumo wa kulipia elimu ya juu umezidi kutumiwa na viongozi wabovu ambao wanaendelea hadi sasa? Uledi upi kwa kuruhusu watu waiingize ATCL katika madini ya kutupwa na badala yake kuwazawadia ofisi nyingine za juu? ur not serious ndugu yangu.
I mean tunaweza kwenda mbele zaidi.
Kama ni kweli kwa muda huu mrefu ndio kajifunza tunayoyaona leo hii basi kujifunza kumepoteza maana.
Sidhani kama kuna Mtanzania anayetaka kujifunza serikali inavyofanya kazi jinsi inavyofanya sasa na akataka kurudia jinsi ile ile! Of course, wapo wana CCM na baadhi ya mashabiki wao ambao wameridhika na ufanyaji kazi wa sasa ambao hawako tayari kuona mabadiliko. Tanzania haiitaji ufanyaji kazi ule ule wa namna ile ile wa watu wale wale waliojionesha kutoa matokeo yale yale. Tanzania inahitaji ufanyaji kazi na maono ya tofauti kabisa na ya sasa. Na hili ukiangalia ndio kiini cha tishio la Dr. Slaa kwa watawala wetu walioshindwa.
Tukirudi na kulinganisha na "misemo" ya watala wetu kweli Kikwete ana mshindani?
a. Aliyesema wanafunzi wanaopata mimba ni sababu ya kiherehere chao ni nani?
b. Aliyesema kuwa hatuwezi kuendelea bila wawekezaji ni nani?
c. Aliyesema kuwa kilichofanyika Benki kuu ni uhalifu na baadaye kuback down ni nani?
tunaweza tukarudi na kuangalia rekodi zao za kiongozi mwenye uzoefu na weledi na kupima kauli zake na ukweli utatuumiza macho kwa mwanga wake.
Ukweli unabakia ukweli.. yaliyofanyika na yanayofanywa kwa siri leo yako hadharani. Lakini of course hutatukumbusha kuwa ni Dr. Slaa aliyemnyoshea Ballali kidole kwenye ukumbi wa Bunge na kusimama Mwembe Yanga kuwaeleza Watanzania jinsi utawala wa CCM ulivyoitafuna nchi yetu. Haya mengine yote unayoyasema Watanzania wanaweza kuyapuuzia na kuyasamehe lakini kwa alichokisimamia Dr. Slaa ni jasiri mara 1000000 kuliko Kikwete. Hawafanani wala hawakaribiani.
We still have time and chance to make the better alternative we want to see mpambanaji...believe me, package ya UKOMBOZi huu ni haijatulia kuliko miaka mitano mingine ya hawa jamaa zetu...hakikisha tu unarudi nyumbani soon...
Hujamgusa yeyote Omar, mimi hapa nacheka tu kuwa umejidegrade yourself to this level. Haya mambo ya pumba na udaku huwa nayafanya mimi (kwa vile ambavyo wengi wenu huko ccm mnaniita). Wewe huwa unajiita mzee wa hoja na issues ... so nimecheka sana kuona ukifanya hivi.Ulianza jana na issue ya wamachame, na leo umekuja na hii..... hongera sana mkuu, very soon utakuwa kama malaria sugu.
Kwa hiyo kwa miaka mitano ijayo, serikali ya kifisadi ya ccm iendelee kuwepo madarakani?
you can't be neutral in the presence of evil for neutrality is the position of the weak!
Najua nikianza kubishana na wewe neno moja hadi jingine sitaweza maana mwenzangu hii ni fani yako.....
Lakini swali langu ni moja tu, Kwanini huo ujasiri wa Dr Slaa tuna uona katika kunyoshea watu vidole tu lakini hatujawahi kuuona katika kusafisha CHADEMA isipokuwa pale tu ambapo maslahi ya Mwenyekiti wake (establishment) yanatishiwa....
Lakini pia hivi kweli unaamini ujasiri wa kikampeni ndio ujasiri wa Urais wa ujasiri wa Upinzani ndio ujasiri wa kuongoza nchi yenye vichwa vibovu kama kina Mtikila na Mbowe who are ready to do anything hata kuhamasisha ubaguzi na umwagaji damu mradi tu mradi wao ufanikiwe?
Kama kweli mwanakijiji una imani na UKOMBOZi wa Dr Slaa na CHADEMA ilikuwaje ukakimbilia CCJ na sio CHADEMA uliyokuwa ukiisadia miaka yote hii???
We still have time and chance to make the better alternative we want to see mpambanaji...believe me, package ya UKOMBOZi huu ni haijatulia kuliko miaka mitano mingine ya hawa jamaa zetu...hakikisha tu unarudi nyumbani soon...
Labda mwenzetu hujawahi kuona, lakini maslahi ya "mwenyekiti wake" ni yapi hasa? Yawezekana maslahi hayo wakati mwingine yamefungamana na maslahi ya chama vile vile na hivyo kutetea chama ni kutetea na maslahi ya mwenyekiti na wanachama wengine ndani ya chama hicho? Dr. Slaa mbona ameshafanya safisha safisha ndani ya chama kwa kuavua baadhi ya watu madaraka kitu ambacho kimemchukua umilele shujaa wako Kikwete?
Hadi hivi sasa hakuna mahali popote ambapo Mbowe au Mtikila amehamasisha umwagikaji wa damu; ila hadi hivi sasa tunajua kuwa kikwete na kundi lake wako tayari kumwaga damu ili wabakie Ikulu. Hii ni kutokana na kulazimisha kuliingiza jeshi katika mchakato wa uchaguzi huku wakihubiri katika majukwaa yao ya siasa juu ya uwepo wa umwagikaji damu wakati wao ndio wenye dhamana yakulinda amani na hadi hivi wameshindwa kumkatama hata mtoto mdogo aliyeshika kisu kutishia amani!
Unajua je kuwa kwa kukimbilia CCJ nilikuwa siisaidii ChADEMA?
nirudi nyumbani ili kiwe nini wakati wewe tayari upo? Miye nitafanya nini ambacho wewe kimekushinda au Zitto, au Mbbowe, au Kikwete, Salim na kina Lissu? Kama nyie wote mmeshindwa miye ntawezaje wakati mawazo ya watu wanaotarajiwa kuchampion change ndio kama haya?
Maana ya hoja zangu ni kuweka mstari baina ya watu hawa wawili kwani JK ni rais na Lowassa alikuwa waziri mkuu aloteuliwa na JK tofauti na Dr.Slaa ambaye ni katibu wa chama na Mbowe ni Mwenyekiti wake hivyo wadhifa wa Dr.Slaa haulingani na ule wa JK ktk dhamana na majukumu walokuwa nayo..Angalao Kikwete ana guts za kuuacha Lowassa ajiingize kitanzini...vipi Dr Slaa ni lini ameweza kusimama mbele ya maslahi binafsi ya Mbowe????
Second, Kuhusu ujuvi ama uledi wa masuala ya Utawala nina uhakika asilimia 100 kuwa Kikwete anamzidi Dr Slaa. Ofcourse Kikwete ana advantage ya kupewa nafasi ndani ya mfumo kujifunza kwa muda mrefu lakini ukiangalia mapambano na sasa majigambo, vikwerombwezo na mikwara ya Dr Slaa, kimoja kiancho onekana ni kuwa hajatumia muda wake kujifunza vya kutosha namna serikali ama utawala unavyofanya kazi...]
....
We still have time and chance to make the better alternative we want to see mpambanaji...believe me, package ya UKOMBOZi huu ni haijatulia kuliko miaka mitano mingine ya hawa jamaa zetu...hakikisha tu unarudi nyumbani soon...
and hypocrites too!you can't be neutral in the presence of evil for neutrality is the position of the weak!
First nionyeshe wapi nimewahi kujiita ama hata kuitwa mzee wa hoja...
Pili, if you need me kusubstantiate kuhusu hiki unachokiita udaku nipo tayari...je na wewe upo tayari?
Na ile ya umachame ni mimi ama mwenzako Mwafrika ndio aliileta hapa...ulitaka nisemaje...kuwa jungu lake ndilo sawa??? Nyie leteni mie nimalize...
Acid ndugu yangu,
Kama huna hoja tumalize malumbano haya. Nisingependa kutumia jukwaa hili kuzungumzia masuala ya ujira wangu, hayo ni ya binafsi. Nitafute tupate kikombe cha chai tuongee hayo. Mimi niko Iringa. Karibu sana ndugu yangu.
Then hakuna haja ya kupigia kelele MDAHALO ambao ki kawaida unahitaji neutrality...