SoC01 Nenda Sia, kila nikikumbuka nasimulia na wengine nawasaidia (Stori ya kweli)

Stories of Change - 2021 Competition
Nov 2, 2020
68
90
Sia ni binti ambaye wakati Fulani tuliwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi,Japokuwa ndio kwanza tulikuwa tumetoka masomoni kwa kuhitimu kidato cha sita.Si jina lake halisi ,Lakini naamini litafanikisha kufikisha ujumbe niliokusudia.

Hatukudumu sana hasa baada ya matokeo kutoka na kila mmoja kwenda kujiendeleza kitaaluma alipojua na pia kiwango cha ufaulu wake ulivyokuwa.

Japokuwa amelala usingizi wa milele na kamwe sitomuona,Lakini historia yake sitoisahau ,Kwani imekuwa sababu ya kwa nini nimefika hapa kusimulia.

Miaka kama mitatu baada ya kutengana,Kupitia rafiki yangu ambaye walisoma wote shule moja O level,Nilipata taarifa amelezwa hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Sikupoteza muda,Nilifika na kumwona wodi alipokuwa kalazwa,Siku hiyo hata mama yake alifurahi sana ,kwani mgonjwa alikula vizuri na chakula kingi kuliko ilivyokuwa kawaida.

Mama alisema kwa kuwa nilikuwa nimemtembelea,Lakini zaidi ni njia niliyotumia ya kukaa karibu yake na kumlisha.

Sia alikuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo,Tatizo ambalo muda mrefu limekuwa likimsumbua kiasi cha kufikia kulazwa.

Nilijitahidi kadiri ya uwezo kuwa nakwenda hospitali,Kwani kibarua changu wakati huo kilikuwa kinanilazimu kuingia saa 12 jioni na kutoka sa 12 asubuhi.

Hivyo nilikuwa kama siendi asubuhi kumuona,Basi jioni lazima niende,Wakati mwingine hata kwa kudanganya au kutoa hela kwa walinzi ili tu niruhusiwe kuingia.

Ilikuwa haipiti siku bila kuongea nae,kumtumia sms au kwenda kumuona na kupiga nae stori hospitali.

Hatimae baada ya mwezi mmoja,Aliruhusiwa kutoka na hapo ndio khasa tulipata muda wa kuzungumza nae kujua nini kinamfanya kuwa katika hali ile,Maana moja ya ushauri madaktari walisisitiza kucontrol mawazo na yale yanayomsumbua kichwani.

Nilipozungumza nae,Alianza kwa kunambia historia ya maisha yake baada ya miaka kadhaa ya kutnegana kwetu.

Ilitokea alibeba ujauzito,Ambao wazazi walipogundua,Walimlazimisha moja kwa moja aolewe na aliyempa .Mipango ya harusi ilifanyika haraka ili kuficha aibu kwa wazazi na hatimae akaolewa.

Kitaaluma alikuwa ni daktari wa mifugo,Hivyo baada ya kuhitimu alipangiwa moja ya kata katika wilaya za mkoa mmoja nchini.

Basi baada ya ndoa yao aliendelea kulea ujauzito,Ijapokuwa anasema haikuwa rahisi kwenye maisha ya ndoa kama ambavyo iko kwa watu wengine.Badala yake mumewe aligeuka wa kumlaumu,Kwamba kwa nini kakubali waoane ilihali yeye bado anaendelea kujipanga kimaisha,Na yeye binti ndio kaja kumuharibia maisha .

Sia ananambia alivumilia maneno hayo,Ilihali analea ujauzito wake,Tofauti na yeye,Mumewe alikuwa mwalimu,Na alikuwa nje ya eneo na mkoa aliokuwa anafanyia kazi mkewe ambae ndie Sia.

Hivyo alikuwa akienda kwa mkewe pindi anapopata nafasi.

Ilifika hatua akajifungua ,Na bahati mbaya mtoto alifariki.Kuanzia hapo maneno yakawa mengi toka kwa mumewe ambae hakuwa na msaada mkubwa kipindi cha ujauzito.

Binti alizidi kutunza vitu moyoni,Na kwa tabia yake ya upole na kutozungumza sana,Hakuwa mwepesi wa kumshirikikisha yeyote hata kwa ndugu zake sikwambii wazazi.

Sikuwahi kumuona mumewe hospitali hadi leo naandika.Nilimuuliza na hakutaka tuyajadili sana ,Japo nilijitahidi kumueleza ajifanye kumsahau kwanza hadi hapo afya yake itakapoimarika.

Alinieleza anatamani amsahau mumewe,Lakini bado mume ana deni la pesa yake,Alimkopesha kiasi cha shilingi laki tisa,Lakini mume amekuwa akimzungusha kumlipa deni lake.

Kipindi hicho binti alikuwa ameanzisha ujenzi wa vyumba viwili na sebule nyumbani kwao,Ujenzi uliofika hatua ya kupaua.Hivyo alitamani apate hela zake ambazo zingemsaidia kukamilisha ujenzi wa nyumbani.

Nilishauri kadiri ya uwezo na maisha yakaendelea.

Nikiri nilikuwa karibu sana na Sia kipindi cha maradhi yake,nae hili analijua.

Haikupita siku sijasikia sauti yake,au kujua hali yake kwa njia yeyote kadiri nilivyoweza.

Leo ni miaka sita tangu Sia ameaga dunia,Sitaki kumlaumu mumewe ambae hakuwahi kuhudhuria hospitali wala mazishini.Sitaki kuwalaumu wazazi kwa uamuzi wa kumuozesha binti ,Wala simlaumu Sia kwa ukimya aliokuwa nao.

Najiuliza wangapi katika mabinti hawana wa kuwaambia juu ya yale wanayopitia kwenye ndoa zao?

Najiuliza,wangapi hawana wa kuwaamini kuwashirikisha,na bado wako ndoani kwa kigezo cha uvumilivu na kulinda heshima ya ndoa?

Najiuliza wangapi wanateseka ndoani,kwa kigezo cha kuvumilia ili tu wawasaidie ndugu zao na familia zao?

Najiuliza wangapi wako tayari kumuozesha binti kwa asiyempenda,Na bado wakamlazimisha kwa kuficha tu aibu kwa familia au kulinda heshima ya familia Fulani?

Najiuliza wangapi wanateseka kwa kutokujua maana ya msongo wa mawazo na matatizo mbalimbali ya Afya ya akili,Na bado hawajui kuwa yanayowatesa moyoni ,yanahitaji kupata msaada kama ilivyo kwenye malaria,Tb,UTI na mfano wake?

Najiuliza wangapi wamekatisha maisha kwa kujiua ,au kujidhuru au kuwadhuru wengine kwa kutopata watu wa kuwashauri,kuwajali,kuwapongeza au kuwakosoa kwa namna ya kuwasaidia kuliko kuwaponda pasi na kuwapa au kuwashauri kupata mbadala wa kimatibabu?

Ndio hapa nasema japo Sia ameondoka na kamwe sitomuona,Maisha yake yamenifundisha kujali hisia za wengine,kuwaheshimu,Kuwasikiliza na kamwe kutochukulia poa kile ambacho mtu ananiambia katika maisha yake,Japokuwa kwangu naweza kiona cha kawaida,Lakini sijui ni kiasi gani kinamsumbua na nini kimesibu hata akanitafuta.

Pumzika salama,kamwe sitochoka kukuombea,Nimejitoa kuwasaidia wengine wenye shida kama yako,Nimejitoa kufundisha kupitia historia yako,Nimejitoa kuwa balozi wa kuelimisha juu ya msongo wa mawazo na kuwashauri watu kuwashirikisha wanaowaamini yale yanayowasumbua kwenye fikra na akili zao.

Nenda Sia!!!!!!!!!!
 
Duuuuuuuh pole sana !
 
Back
Top Bottom