President of China
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 31,548
- 89,516
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki Mkutano wa thelathini wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC COP-30), unaoendelea jijini Bélem, nchini Brazil kuanzia tarehe 03/11/2025 na unatarajiwa kukamilika tarehe 21/11/2025.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi, ameongoza ujumbe wa NEMC kuwasilisha Mradi Kwa Benki ya Maendeleo ya Africa (African Development Bank) Mradi ambao imepitishwa na benki hiyo.
Mradi huo wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 15 unatarajiwa kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo ya pwani yaani Dar es Salaam, Pwani na Pemba.
Aidha, Dkt. Semesi alikutana pia na Sekretarieti ya Mfuko wa Kimataifa wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (Adaptation Fund-AF) ambapo aliweza kuwahimiza Adaptation Fund kukamilisha taratibu za kulipatia Baraza ithibati ya pili (reaccreditation) sambamba na kukamilisha mapitio ya miradi iliyowasilishwa yenye jumla ya thamani ya Dola za Marekani milioni 35.
View: https://www.instagram.com/p/DRRuP9bDBfn/