NEMC na NEC wekeni sheria ya kuondoa mabango na kupiga marufuku uvaaji wa nguo za kampeni, kapelo, tshirts, vilemba na kanga baada ya Uchaguzi Mkuu

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,460
2,000
Moja kwa moja kwenye mada.

Nashauri Baraza la Taifa la usimamizi wa Mazingira NEMC na Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC kuweka muda maalumu kwa vyama kuondoa mabango na matangazo yote ya kampeni baada ya uchaguzi ili kuweka mazingira safi.

Sasa hivi uchaguzi umekwisha lakini mitaani, barabarani, kwenye vituo vya mabasi na nguzo za taa kumejaa mabango ya wagombea kana kwamba bado tupo kwenye kampeni. Baada ya uchaguzi yote hayo huwa ni uchafu hivyo ni lazima kuondolewa.

Vile vile kuwe na marufuku ya kuvaa nguo za kampeni kama kapelo, tshirts, vilemba na kanga baada ya uchaguzi kwani ni kujidhalilisha na kutojua maana na pia ni uchafuzi wa mazingira.

Yaani mpaka leo unakuta mtu kavaa kapelo au tshirt ya CHAGUA MKAPA au CHAGUA KIKWETE au CHAGUA MAGUFULI au ARI MPYA, NGUVU MPYA, KASI MPYA. Hayo yote iwe ni marufuku.

Mimi nashauri kuwe na sheria inayouazimishaviwanda vinavyo tengeza nguo za kampeni kutengeneza zile zitakazo dumu kwa muda usio zidi siku 70. Yaani ziwe zina expire ndani ya muda huo ili kuwakomoa wanaoendelea kuvaa hata baada ya uchaguzi. Yaani baada ya muda huo mtu akivaa tshirt au kanga au kapelo iwe inageuka lami na kuganda mwilini au akifua iwe inachanika na akianika iwe inageuka jivu. Kwa mtindo huu tutakuwa tunalinda mazingira kutokana na uchafu unaotokana na shughuli za uchaguzi.

Naomba kutoa hoja!
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,668
2,000
Hizo tshirts wengine ndio nguo zao za kushindia, wanavaa toka za enzi ya Kikwete sasa hiki unachokitaka wewe sijui unataka wale jamaa watembee vifua wazi.

CCM inawafanya watu wawe masikini ili waendelee kutawala kwa kuwadanganya kwa kanga na tshirts, huku wakisaidiwa na Mahera.
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
13,496
2,000
Kila baada ya hatua 10 bango la mgombea, kwamba Watanzania ni wasahaulifu kiasi cha kumsahau mgombea hatua 10 tu tangu ameona picha yake?
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,136
2,000
Haya ni matokeo ya kuishi in a shithole country,nguo za vyama ni haki ya kila mwenye nayo kuivaa au kutoivaa BUT mapango yote ya kampeni za vyama lazima yatolewe within 30days baada ya uchaguzi kufanyika na ni mamlaka ya local governments kusimamia hili na wana sheria ya fine kwa bango lolote litakalopitiliza muda uliowekwa.
 

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
5,359
2,000
Mkuu sasa itakuaje wakati nchi nzima imejaaa mabango ya Yesu(kwa sauti ya Lugola)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom