Neema kwa wafugaji, Rais Samia kuifufua NARCO

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Mwenyekiti wa kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO), Mhandisi Luhemeja ameeleza kuwa Serikali inakwenda kufumua muundo wa NARCO ili kila mkoa uwe na Ranchi yake pamoja na Meneja wa NARCO wa Mkoa na hivyo ameitaka menejimenti ya NARCO ikae hataka kufumua mfumo uliopo sasa

Luhemeja ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kugusa kila sekta kwa namna yake ya kipekee tangu aingie madarakani ambapo ameonesha mwanga katika sekta za usafirishaji, utalii, na zingine nyingi lakini sasa ameamua kugeukia katika sekta ya Mifugo sekta ambayo ni mtambuka na yenye kuweza kuingizia taifa letu fedha nyingi sana endapo tu jamii itaanza kuzingatia utaalamu katika ufugaji na hivyo kujipatia mazao mengi na yanayokidhi soko la kitaifa na kimataifa.

Licha ya Tanzania kuwa ni ya pili kuwa na idadi kubwa ya mifugo barani Afrika ikitanguliwa na Ethiopia lakini imeendelea kuburuza mkia katika mapato yatokanayo na sekta hii ya mifugo hivyo Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliona hili ameelekeza kujikita katika utaalamu na kuzingatia usasa katika ufugaji kwa uthubutu wake katika kuifufua tena kampuni ya ranchi ya taifa NARCO. Ambayo ilianzishwa kwa lengo mahususi katika kuendeleza na kueneza ufugaji bora, ususani ufugaji bora wa ng'ombe wa nyama bora ambayo itakidhi vigezo vya soko la ndani na nje.

Kufikia sasa katika mwaka huu wa fedha tayari NARCO imepatiwa bilioni tano ikiwa ni mtaji wa kuanzia kazi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom