NECTA wapeni walimu stahiki zao

yoga

JF-Expert Member
Jan 6, 2013
1,820
8,498
Dhuluma ni kitu kibaya sana. Heshima mnayopewa na wanaoitwa waalimu na nyie kuipuuza na kuwafanya waonekane kama takataka si sahihi hata kidogo!

Toka mwezi wa 11 mwaka jana mpaka leo hamna hela za kuwalipa watu kwa kazi waliyowafanyia? Mumewatoa watu kwenye makazi yao na kuwasafirisha mlikowapangia kwa gharama zao, za kwenu mlipeleka wapi?

Na nyie waalimu hivi mtaendelea kuonewa mpaka lini? Kazi kupiga simu na kuulizia malipo! Hivi kiutaratibu, protokali ikishindwa hamjui mfanyeje kudai haki yenu?

Pombe Magufuli unayo kazi. Kama kuna watu wanasoma humu hizi post wakufikishie taarifa!

Una habari waalimu wako unaodai hawafanyi kazi mliwapangia majukumu ya kusimamia mitihani toka mwaka jana mpaka leo wengi wao hawajalipwa? Unadhani hawa watu watafanya kazi kama unavyodhani?

Hawawezi kugoma kwa kuwa hawana kipato cha kuwafanya wagome lakini nakuhakikishia watoto wetu ndio wanagomewa!
 
Waalimu bhana huwa wananishangaza saana. Huwa hawajiamini kama walistahili kufanya ile kazi. Hata ikifika kwenye kudai haki zao wananyamaza tu.

Yaan wako kama;
"Cha kutumaini sina"
 
Waalimu bhana huwa wananishangaza saana. Huwa hawajiamini kama walistahili kufanya ile kazi. Hata ikifika kwenye kudai haki zao wananyamaza tu.

Yaan wako kama;
"Cha kutumaini sina"


Ni shida aiseee kwa stail hii kazi ipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom