Wasichokijua walimu kuhusu t-shirt zao za CWT

Oct 13, 2018
35
259
Na Thadei Ole Mushi.

Ununuzi wa T-shirt.
___________________
Tarehe 13/10/2020 kwenye makao makuu ya Chama kilifanyika kikao kwa ajili ya kuingia Mkataba wa kununua T-shirt za walimu kwa ajili ya Mei Mosi.

Kikao Hicho kilihudhuriwa na wajumbe watano ambao ni Mwl Leah Ulaya (Mwenyekiti) Mwl Deus Seif (Katibu) Mwl Alawi (Mjumbe) Mwl Maganda Japhet (Mjumbe) na Mwl Dina Mathan (Mjumbe)

Kwenye Kikao Hicho walikubaliana kuwa Kampuni ya L.N Shah na Gogo wachukue Tenda ya kutengeneza T-shirt hizo.

Gharama za T-shirt ilikuwa ni bilioni 3. 52 bila Kodi ukijumlisha na Kodi Mkataba ulisomeka kuwa ni Bilioni 4.1.

Gharama hii ilikuwa itengeneze T-shirt za walimu 245,000 ambazo zingetumika siku ya Mei Mosi.

Ili mzabuni akubali kuifanya Kazi hii Mkataba ulitaka Chama kilipe gharama za uchapaji kabla miezi nane.

Kilichotokea ni kwamba kutokana na Mgongano wa maslahi wa watu kutaka 10% hivyo kuchelewesha utiaji Saini malipo huku Mzabuni akiwakazia kutokutoa 10% na hatimaye walimu walikosa t-shirt zao siku ya Mei Mosi.

Kinachonishangaza ni tuhuma za dili Hili la 10% Kurushiwa Mtu mmoja. Nadhani watu hawa watano wote waliosaini katika kiambatanisho hiki wanapaswa kuwajibika kuwaambia walimu ni nini kinaendelea kwenye Chama chao.

Mchezo wa 10% ndani ya CWT haujaanza Jana Wala Juzi. Wakati KM huyu akiingia madarakani uongozi ulikuwa ukimlazimisha anunuliwe V8 (VXR) Kidogo angeingia mtegoni kumbe 10% ilikuwa imeshawekwa kwenye Mpango huo Ila kwa bahati KM alisema atakarabati gari liliokuwepo na yupo comfortable kulitumia Hilo hilo.

Ubadhirifu ndani ya CWT
__________________________
Tarehe 27/3/2017 Katibu mkuu kiongozi alimuomba CAG afanye ukaguzi kwenye chama cha Waalimu CWT.

Ukaguzi ulijikita katika tuhuma dhidi ya Uongozi wa chama cha waalimu zinazohisu ubadhirifu wa fedha na mali za chama.

Ukaguzi maalumu ulikagua taarifa za mapato na matumizi ya Chama, Uliangalia uhusiano uliopo kati ya Benki ya waalimu na waalimu wenyewe, uhusiano uliopo kati ya Mwalimu haouse na mwalimu mwenyewe.

YALIYOBAINIKA.
__________________
1.Hakuna mfumo mzuri wa wanachama unaoonyesha kumbukumbu za wanachama. Katiba ya CWT inaeleza kuwa kunatakiwa kuwe na aina nne za wanachama lakini CWT hawaonyeshi aina hizo za wanachama hivyo haijulikani CWT ina wanachama wangapi.

Pia katika swala la wanachama hakuna taarifa zinazoonyesha wanachama walijiunga lini, mishahara yao kwa mwezi, namba ya uanachama, kiwango anachochangia kwa mwezi nk. Jambo hili CAG anasema kuna uwezekano kuna fedha nyingi zinaliwa kutokana na kutokuwepo kwa taarifa hizo.

2.Malipo ya shilingi 11,924,250,620.13 yalifanyika bila viambatanisho vyovyote. Hii ina maana hakuna nyaraka zinazoonyesha matumizi sahihi ya fedha hizo.

3. Shilingi 3,287,708,358 zilipwa bila kuidhinishwa na katibu mkuu au mweka hazina wa Chama na pia hakuna viambatanisho.

4. Shilingi 11,924,250,620.13 zililipwa bila kuzingatia makisio. Hii ina maana fedha hizi zilitumika bila kuzingatia bajeti ya CWT.CAG anasema viongozi wanakosa nidhamu ya matumizi ya fedha hivyo kuna fedha hapa zilitumika bila wanachama kujua zimekwenda wapi.

5. Hakuna nyaraka zinazoonyesha umiliki wa moja kwa moja wa CWT na miradi yake.

6. Hakuna nyaraka zinazoonyesha mtiririko wa mapato wa vitega uchumi vya chama toka CWT kianzishwe.

7.Mwalimu House imesajiliwa Brela kwa jina lingine la Teachers Development kupitia usajili wa Brea 45719 Badala ya TDCL. Na CAG amebaini kuwa kampuni hilo la Teachers Development halijawahi kufanya kazi toka kuanzishwa kwake. Kwa hiyo mapato yake hayaonekani.

Rais wa CWT Bi Leah Ulaya anatakiwa awajibu walimu kuhusu upotevu wa Mabilioni haya kwa kuwa kwenye Ripoti ile anatajwa Moja kwa Moja Ukurasa wa 51.

Leah Ulaya ana maswali mengi ya kujibu walimu kuliko Mtu mwingine
________________________________
Wakati ubadhirifu huu wa Mabilioni ya Shilingi yakitokea Katibu Mkuu wa sasa hakuwa ameajiriwa bado Hili lazima walimu walifahamu ili kila mtu abebe msalaba wake kuelekea Mahakamani siku mfumo utakapoamua kumsaidia mwalimu.

Leah Ulaya atuambie ni nani aliingia Mkataba wa ujenzi ambapo Mjenzi SUMA JKT na Mshauri wa Ujenzi De Popolo walikuwa wakilipwa Fedha sawa kwenye ujenzi wa Ofisi za Chama kote nchini. Uliona wapi Mjenzi na Mshauri wakalipwa (Contractor na Consultant) wakilipwa Fedha zinazolingana? Walimu tuna tatizo la kutokufuatilia mambo na kuhoji.

Tumuulize Rais Leah ni kwa ni nani alibadilisha Report ya CAG? Yaani report ya CAG Original hakuthubutu kuisoma kwenye Kamati Tendaji ya Chama. Ripoti ya CAG ilikuwa na page 56 yeye lakini iliyosomwa kwa Kamati Tendaji ni page 18. Tatizo la walimu hatufuatilii mambo....

Tumuulize Rais Leah ni nani alikula Milioni 300 za mabati ya walimu ya kiinua Mgongo Cha kustaafu? Kule Wilayani Sumbawanga na kwingineko haya yametokea....Fedha za wastaafu za mabati zimeliwa mchana kweupe au mbafikiri hatujui?

Makundi
__________
Kwa sasa CWT imepasuka vipande vipande. Badala ya ku deal na issue za kumtetea mwalimu wanapambana kuondoana madarakani.

Kuna tetesi katibu wa Wilaya mojawapo Mkoani Morogoro anachangisha Fedha za kampeni za kumuondoa Kiongozi mmoja wapo kwenye viongozi wakuu wa Chama. Haijajulikana ana interest Gani lakini Muda si mrefu watatajana kwa majina.

Vielelezo nimeambatanisha

Ole Mushi
0712702602.

Screenshot_20210605-212559.png


Screenshot_20210605-211601.png
 
Kama hiyo report ya CAG ya mwaka 2017 haikuwahi kufanyiwa kazi hayo ndio madhara yake, walimu pamoja na mishahara yao kidogo bado wananyonywa na viongozi waliotakiwa kuwatetea, 10% is everywhere.
 
Walimu hawajawahi kujielewa. Walimu wajanja wanakula fedha za wenzao waliolala.

NB; Mtoa mada aliyeagiza uchunguzi maalumu alichukua hatua gani dhidi ya wabadhirifu?
 
Walimu hawajawahi kujielewa. Walimu wajanja wanakula fedha za wenzao waliolala.

NB; Mtoa mada aliyeagiza uchunguzi maalumu alichukua hatua gani dhidi ya wabadhirifu?
Nasikia CWT ndio hudhamini show nzima ya mei mosi Sasa nani atawagusa. Ila sishangai tabia ya kujipendekeza na unafiki ni tabia ya walimu wengi
 
Walimu nichagueni ni watetee.
Walimu munashida kibao..
Walimu ni madaraja kwa wanasiasa.
..alisikika kichaaa akiyasema hayo..
 
KILA SIKU VILIO NI CWT MBONA VYAMA VINGINE HATUSIKII? WALIMU MNA SHIDA GANI?
Mfumo wa nchi hii ni mbovu katika mambo mengi. CWT haina tofauti yoyote ile na ilivyo kwa LENGAI OLE SABAYA. Siku mamlaka zikiamua kuifuatilia kwa undani, madudu mengi yatajulikana.

Walimu waendelee tu kulalamika mpaka siku Serikali itakapo amka na kuingilia kati. Ila kiufupi hiki chama kina msaada na tija ndogo sana kwa walimu. Huu ni ukweli mchungu.
 
Back
Top Bottom