Necta: Hivi ndivyo kudumisha muungano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Necta: Hivi ndivyo kudumisha muungano?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by muhogomchungu, Jan 28, 2011.

 1. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NECTA: HIVI NDIVYO KUDUMISHA MUUNGANO?

  Na: Malik Nabwa
  Katika mambo ambayo yanauma sana na kuumiza matumbo ni pale mtu au kikundi cha watu chenye kufanya mabaya, kinapojitakasa kwa kutumia lugha nzuri kuhalalisha maovu wayafanyayo. Kwa mfano, kuna watu huweza jiita mujahidina ili kutoa picha nzuri kwa jamii kubwa ya Waislamu ili pia na vitendo vyao viungwe mkono kwa kuamini wao ni wana jihadi, lakini ukivipima hivyo vitendo vyenyewe havimo katika uislamu kabisa
  Kuna watu hujiita watetezi wa haki za binaadamu lakini kiudhati wao huwa ndio wavunjaji wakubwa wa haki hizo. Na wako pia wanaojiita watetezi wa wanyonge lakini ikawa hiyo ni njia yao au kibali chao cha kupata kuwanyonyoa vizuri hao wanyonge inaojitia kuwatetea.
  Natamaka haya kwamba hapa kwetu tumepata kijisababu kiitwacho Muungano. Imekuwa jambo kunuka kiambo. Kila Mzanzibari anavyojaribu kujitetea na kudai haki zake basi hubambikizwa neno la ‘mvunja muungano’. Wakati tukijuwa wazi kuwa muungano ni mashaka na zigo la mazagazaga ya taka iliyokolea vundo kwa Mzanzibari, Viongozi wetu wa bara na Wa hapa Zanzibar wakija kwetu, hutuimbia wimbo huu wa ‘’kudumisha Muungano’’. Ninavyojua mimi muungano madhubuti hujengwa kwa misingi halali iliyosimamiwa kisheria ikiwa ni pamoja na kutendeana haki pande zote zilizoungana bila ya kuwepo hujuma au kinyume , mtima nyongo, au machapa kungu Fulani hivi.
  Nijuavyo Muungano ni kupendana kwa dhati na kutakiana mema kila uchao. Muungano ni kudumisha amani na utulivu wa kweli na sio wa katika bomba tu. Muungano ni kuunga nguvu isiyo chembe ya unafiki, wala Uazandiki ndani yake. Muungano ni kujitakasa na unafiki, na unyonyaji au Ukandamizaji wa aina zote kati ya pande zinazoshirikiana. Muungano ni kuungana nguvu, na kushikana mikono pale mmoja anapokwama akakwamuliwa. Hivi tujiulize huu muungano wetu una maana hii? Una sifa hizi?
  Mfano mdogo tuzungushie shingo Baraza la mitihani la taifa (NECTA).Tangu miaka ya 1970 na baada ya kuundwa kwa baraza la mitihani la Bara na sio la Tanzania, Wazanzibari tumekuwa wahanga wakubwa wa baraza hili hasa pale inapokuja mitihani ya masomo inayosimamiwa na wao wenyewe chini ya baraza kandamizi pendelezi liitwalo NECTA.
  Kuna wakati kabla ya Marehemu Kigoma Malima baraza hili likuwa na njama dhidi ya wanafunzi wenye asili ya kiislamu. Ikawa ukiwa na uislamu tu hupiti kwa njia yoyote ile. Unaletewa ‘C’ ya dini, na kiarabu, tena hapo uwe ni hodari wa kutafutiwa watu. Mungu akampa maarifa kabla hajahujumiwa Bwana Malima akabadilisha mfumo akaleta nambari za mitihani bila majina. Tukawa tunapata asilimia kumi kuendelea usoni. Ndio akina sisi wawili watatu.
  Lakini kila uchao, muelekeo wa sasa ni wazi kuwa Baraza la mitihani linaendesha hujuma za chini kwa chini dhidi ya Waislamu na hasa sasa wazanzibari. Mimi siwezi amini hata siku moja kama watu wote katika darasa moja huwa na ufahamu wa aiana moja au unaolingana kwa karibu mno kwa wote darasa zima.
  Hakuna utafiti uliowahi kuthibitisha hili kuwa watu 40 Darasani waliochaguliwa tu hivi (randomly) kisha wakawa na uwezo wa aina moja kwani watalamu husema Individual differences are Inevitable’’. Lakini hili bara wanalikataa kabisa kupitia NECTA. Kuna shule huko darasa zima lina Div 1, na nyengine Division 1-2, hakuna 3 Darasa zima. Kila mwaka huwa hivi. Maajabu ya nani haya, maana si ya Musa wala Firauni.
  Sasa kwa sisi ambao hatuujui ualimu hata kidogo hatuwezi fahamu kitaalamu lakini kwa akili hii ya kichwa mchungwa hili haiyumkiniki hata kidogo. Lakini kwa baraza la mitihani hii ni hali ya kawaida katika dunia yao. Ukweli ni kwamba bara kuna Skuli haizijawahipo kukosa hizo Div 1 na 2 kwa kila mwaka na kila mwanafunzi utamkuta kapata alama hizo.
  Huku Zanzibar Division One huwa lulu au kipusa (Pearl in the Crown). NECTA kwa maana yao inajaribu kutushawishi kila hali tukubali kuwa Zanzibar hawana uwezo wa kusoma na kwa maana hiyo Muungano ni msaada mkubwa kwetu kutufikisha anaglau hapao padogo tulipo. Na ndio ukaona hata Viongozi wanatuchagulia wengi huwa ni wale waliowakataa wao NECTA kwani wakiwaeka wenye maarifa makubwa watahoji kama alivyofanya Bwana Kigoma Malima.
  Ukiuliza sababu za kufeli sana huku siku hizi utatajiwa nyingi sana. Hakuna walimu wazuri, moja bara bila shaka walimu wao hutoka angani. Mbili, hakuna vifaa vya kutosha, mbili, bara hutengeneza vyao. Walimu hawalipwi vizuri, tatu, sawa lakini khaah! Hata hili?. Wazanzibari hawataki kusoma ni wanyeye (Bogus), nne, ni kiasi tuitwe hivi maana mtu kukubali changanya ng’ombe mmoja na mmasai alien a Ng’ombe milioni arubaini si ubwege mdogo huo, lakini sidhani kama unaathiri matokeo nchi nzima, pengine labda!. Na sababu nyengine mutajazia nyie wenyewe. Maneno haya ndio yanayosemwa na kufanywa kuwa hoja kuu huko NECTA na kwa wenzetu wa bara kuhusu kuanguka kwetu katika matokeo ya mitihani ya taifa..
  Lakini mimi kwa maarifa yangu kumvikumvi, na mawazo manayaufunyaufu ni kuwa haiwezekani kabisa kuwa wanafunzi 40 wote wakawa wana daraja moja ya uwezo au inayolingana kiasi ya kuwa siku zote ni Divisheni 1-2 basi tena kwa kila somo. Dhana hii potevu inapingana kabisa na tafiti kongwe za kisaikolojia ya Elimu zinazoamini kuwepo kwa ‘’ndividual differences’’ madarasani na hata ‘’exceptionality’’ humo madarasani. Sasa tukisema kuwa NECTA imegawa maeneo yake itakavyo na kuyafanya yote yawe ya kiwango sawa (Homeogeniouos) ili kuyata kafara kutimiza azma yao ya kisiasa hilo halina mushkeli, tusidanganyane.
  Kwa mafano anuai angalia matokeo, Maeneo ya pwani yote ya Tanzania na Zanzibar yake hao ni watu wa kupata C za kuchaguwa, D rundo kwa rundo na waliobaki wote F tupu hata wakiwa vipi. Wakijua wazi mgao huu uatawapitisha Wazanzibari chini ya asilimia 20% kuendelea na masomo ya juu. Huku kwao wakitoa alama za juu kwa shule zao za Seminari na nyenginezo katika malengo yao ya milenia, darasa zima hupewa alama A tupu na waliobakia B na wasio na bahati kidogo huishia C lakini kwa ufupi hafeli mtu huko si kama huku kwetu.
  Nionavyo, pamoja na sababu zote wanazozitoa kuhusu Zanzibar kuhalalisha kufanya kwetu vibaya takribani mara zote katika mitihani ya taifa, kuna hujuma na ukorofi dhidi yetu huko katika baraza la mitihani. Na ningekuwa bungeni au uwakilishini hivi sasa (Siwezi kuwa tena kwa sasa maskini) basi ningeomba iundwe tume ya kuchunguza uhalali wa matokeo baraza la mitihani la Taifa (NECTA). Kwa hili nisingekuwa na wasiwasi maana ukweli haufichiki.Tungewakamata tu maana Dr. Malima alipitia nia hii hii na hakuchukua muda aliwatia nguvuni.
  Haiwezekani hata siku moja watu wa nchi Fulani wawe ni mazuzu karibu wote na wa nchi nyengine jirani wawe mahodari wote hata kama wangeumbwa na kuzaliwa tumbo moja.Vyovyote iwavyo, nasema NECTA kuna hujuma tena ya muda mrefu na sasa kama ni jipu lishawiva tulipasuwe tulitowe moyo tuuguze kidonda siku mbili ya tatu tubakishe kovu. Bila hivyo hawa watatumaliza maana wanajua wazi kutufanyia hivyo ni kunedeleza kuudumisha huo Muungano kwani tutakuwa hatuna sauti ya kuhoji na kudai haki zetu.
  Muda si muda hivi, MATOKEO yameshatoka na Shule ya Biashara Mombasa ni ya pili kwa Zanzibar huku Lumumba ikiongoza na katika gredi ya taifa ni 93 nchi nzima. Hodari wetu hao wako katika nafasi hiyo. Hii ni taswira ya kututawla kisaikoljia na kutufanya tujione matobwe mbele yao siku zote. Hata ukiangalia vipindi vyao vya vituko basi dhihaka (Stereotypes) zao zote ni za kejeli tu dhidi yetu kutuona nyungunyungu au konokono asie gamba (Escargot). Ndio ukasikia mara ‘mdebwedo’, ‘ami’, ‘akhee’, yote hii ni dhihaka ya kutuona sisi wazulufu na wabole na sio utani kama tunavyodhani.
  Mpendwa msomaji na mzalendo, nikiwa naandika makala hii niko na jazba kidogo (emotional) kumradhi, lakini kwa yoyote anaetaka kujaribu kuchunguza uukweli huu, basi na iundwe tume huru kuichunguza NECTA kisha itupe majibu. Hilo moja. Pili, Zanzibar na ijitoe iingie katika mitihani ya Cambridge ambayo itatungwa na kusahishwa hukohuko Maksifodi na makambriji na huku bara nao wakifanya mitihani yao na hiyo ya Cambridge tuone. Naamini hawatapasi wanafunzi wote huku Zanzibar lakini haitakuwa dhulma kama hivi ilivyo sasa chini ya NECTA. Tuamke, tutanabahi, tufikiri namna ya kujivua na baraza hili. Bila hivyo tutakuwa vilaza wa Elimu wa Kimataifa muda si mrefu kwa sababu hiyo ndio taswira wanayoijenga NECTA mbele ya dunia.
  ‘Mbuyu zishakaangwa wenye meno tafuneni!’
  Wakatabahu.
  Nabwa!
   
 2. m

  mshaurimkuu Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama kweli hiki ni kichekesho kama sio uendawazimu! Inawezekana (na kwa kweli zipo) kukawa na kero za muungano lakini kilichoelezwa hapa kwangu ni "utumbo" mtupu tena ni uchochezi wa kipuuzi. Ndio yale yale ya tunaonewa, tunanyanyaswa, sijui tuna ..., ...!

  Hapa mambo kama matatu hivi yanajaribu kutumika ili kujenga hoja hii ya kipuuzi - UDINI, UTAIFA, UKANDA - sijui tuelewe lipi?

  UDINI: Eti matokeo ya mitihani katika nchi hii yanapangwa kidini! Alipokuja Mh. Prof. Kighoma Ali Malima, kidogo alirekebisha hali lakini ila kwa sasa mambo yamekuwa tena mabaya kwa wenye dini hiyo! Ndugu, ongea kwa hoja, acha kuropoka.

  UKANDA: Ameona dini haitoshi kushadidia vizuri hoja yake, anaongeza na ukanda - eti maeneo ya PWANI mambo ni mabaya zaidi.

  UTAIFA: Bado dini na ukanda havikumtosha vizuri kujenga hoja yake, ameongeza na utaifa - WAZANZIBARI!

  Hivi mwandishi anataka kutuambia vigezo alivyoeleza ndivyo hutumiwa na baraza kupanga matokeo ya mitihani? Namshauri andelee kusubiri nadhani kuanzia mwaka huu matunda yataanza kuonekana kwa kuwa kwa miaka minne iliyopita na kwa awamu hii mawaziri wa elimu ni wale wa DINI yake tena wa sasa hivi ni wa UKANDA wake ambapo si mbali za Zanzibar ni kama km. 35 tu. Hata mkuu wa nchi anatoka maeneo hayo hayo.
   
 3. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,934
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  hii habari imeandikwa na cherehani au binadamu...?
   
 4. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,738
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Duh, mada yako imejaa uchungu kama muhugo muchungu.

  Ila nakushauri utafute sababu zingine za wanafunzi wa visiwani na pwani kushindwa vibaya, of course hata wanafunzi wengine mikoa mingine wamefeli sana, hasa shule za kata. Lakini tafadhari sana, usisingizie NECTA.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,546
  Likes Received: 18,195
  Trophy Points: 280
  Malik Nabwa na Muhogo Mchungu, poleni kwa matokeo haya. Huu ndio mchungu kuhusu elimu yenu. Matokeo haya ni reflection ya social dynamic ya education background ambayo ni madrasa. Kwenye matokeo haya Nabwa ameifuatilia ya Zanzibar tuu hali ndio hivyo hivyo kwa maeneo yote ya Muslim dorminated sambamba na Islamic Seminaries.
  Poleni!
   
 6. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha udini pasco, mimi nimesoam madrasa. lkn niliwashinda mapdri darasani tulipokuwa chuo kimoja, na yeye akija na mslaab mkubwa shingoni. lkn kumbe alikuwa mbovu ktk math, yaani 0 kabisa.
   
 7. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Sasa Amijei Cambridge Ndipo Ugalatia ulipoanzia kabla ya kuja huku.Si ndio kifo kabisa.
  Na Div 1 Amijei sawa kwa Darasa zima lakini wewe angalia Point za hizo one azilingani Amijei.
  Amijei ni kweli Zanzibar amsomi ati,someni mwone
   
 8. a

  adobe JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Hayo majungu ndo yanayowasabisha jamii yenu ifeli.Badala ya kukaa madarasani na kusoma mnaishia kupiga majungu.Mtasoma saa ngapi na mtafaulu vipi? Nakushauri uende NECTA upitie mitihani ilivyosahihishwa kati ya wakristu na waislamu.Linganisha walau majibu ya waislamu 10 na wakristu 10.Hapo utajuwa aidha mnahujumiwa au la.Ubaguzi mnao ninyi.Hebu nenda vyuo vikuu vya kikristu waislamu wako kibao ila vyuo vya kiislamu hamtaki wakristu.Acheni majungu someni na mfanye kazi
   
 9. P

  Pokola JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  :clap2:Hahahaaaaa, sasa huyu jamaa anataka watungiwe mitihani yao peke yao, mirahisi? Ona kwanza mwenyewe alivyoandika hovyo, asivojua kupangilia anachoandika.

  Teh, teh!!!! Nimeishi na hawa jamaa aisee, ni wavivu kupindukia. Wacheni usultani wajomba, someni na mjitume asee!!!:clap2:
   
 10. L

  Lweye Senior Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
   
 11. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakuna hoja hapa, ni majungu makubwa yenye lengo la kuwagawa watu.NECTA haina lawama na kushindwa kwa watu mitihani. mitihani haipimi "group normality" kama ulivyojengea hoja, bali "individual candidate excelence"; hivyo kupata darasa zima Div. 1 or div. 0 ni kawaida, kwani ndo kilamtu alivyofanya.
   
 12. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,738
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Duh, mada yako imejaa uchungu kama muhugo muchungu.

  Ila nakushauri utafute sababu zingine za wanafunzi wa visiwani na pwani kushindwa vibaya, of course hata wanafunzi wengine mikoa mingine wamefeli sana, hasa shule za kata. Lakini tafadhari sana, usisingizie NECTA.
   
 13. M

  Marytina JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  well said, nadhani ni binadam mbumbumbu, JANA MWINGINE KANIAMBIA WASAHIHISHAJI wamewachezea rafu watu wa kabila lake, NIKAMUULIZA VIPI HAO UNAODAI WAMEFELISHWA TUKAWAPA VYETI LEO tena vya udaktari wakutibie?akanjibu daktari hapana wataua watu lakin kazi nyingine wapewe,nkabakia kucheka.

  imekuwaje walenge watu wa dini yako wakati namba hutumika badala ya majina? hata hapa bara wamefeli wengi acheni fikra za ajabu

   
 14. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  mwaka huu 50% wamepata div 0, waislam wangapi na wakristo wangapi?

  wakati nasoma Pugu, waislamu karibu wooooote walihamia na magodoro yao msikitini sie tuabaki tunapiga buku class, discussions za kufa mtu tena wanafunzi toka wa shule mbalimbali. kuna waislam wachache wakastuka walipoona wale wanaolala masjid wanagalagazwa vibaya kwenye Continous Assessment Tests (CATs) na 'makafiri' (maana walikuwa wanatuita waziwazi ila Headmaster aliyekuwa pia muislam akatusihi tusijibu kitu maana haitapunguza As zetu) wakaamua kujitoa masjid na kujichanganya na sisi. Mwisho wa siku..AIBU KWAO..so watu wa aina hii wanabaki kutoa visingizio wanapunjwa maksi na NECTA kwa vile Examination numbers zao ni za kiislam (maana hawasemi wanapunjwa vipi).

  Shule za seminary huwa zinachuja tangu Form I hatimaye wanabaki na cream tu so hii inajibu upuuzi wako eti kwa nini wanafunzi wote 40 wana div I.
   
 15. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kwa nini Wazanzibar wasianzishe necta yao halafu wakawapa wanafunzi wao Div one point 7 kwa form four na Div one point 3 form VI hata kama hawaendi kabisa shule? Wakitaka kuja kusoma huku tuwapige matrix test za kufa mtu ili wapeleke ujinga wao huko huko Zanzibar
   
 16. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ok, hata ud hulala msikitini na matukio yao mazuri tofauti na wakiristo .
   
 17. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Hiki sasa kituko at least nimefahamu muhogomchungu ni mzanzibari yaani amijei mdebwedo,
  Huwezi ukatumia akili na kufikiri kucheza draft ni matumizi mabaya ya akili na kufikiri
   
 18. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  waalim wa wazanzibar wawe na kamati za ushindi ingawa dini hairuhusu lakini kwenye vita haina budi mbinu kutumika!mfano division I nyingi za seminari zinatokana na masomo ya BIBLE KNOWLEDGE,COOKERY,NEEDLE WORK wanapata A.Wakati islamic knowledge mwanafunzi wa kwanza C
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,832
  Trophy Points: 280
  Niliposoma mimi hawa jamaa walikuwa na mitihani yao maalumu toka NECTA hiyohiyo.....lainilaini kabisa kuliko tuliyofanya sisi...sijui bado hali ni hiyo kwa sasa?
   
 20. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,549
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Kazi kweli kweli kubishana na watu wa mihadhara, hawa hoja zao zimejaa chuki dhidi ya ukristo.Wanashindwa kuelewa kuwa hawatapata jibu la matatizo yao kwa kuendeleza chuki kwa wakristo.Chanzo cha matatizo ya watz wote ni umaskini, na umaskini huu umesababishwa na ufisadi uliokithiri kwa viongozi wetu bila kujali dini zao, ufisadi hauna dini kwani wenyewe ufisadi ni dini. Sasa ndugu zetu hawa wamelishwa sumu ya kuona kuwa kanisa ndiyo linawaletea umasikni, nao wameinywa sumu hii, lakini ukweli utabaki kuwa udini na chuki hizi zinawanufaisha chama cha mafisadi (CCM), na miongoni mwa hawa mafisadi ni WAGALATIA( kwa mujibu wa msamiati wao).
   
Loading...