NEC yatishia kusitisha uandikishaji wa BVR

NEC yatishia kusitisha uandikishaji wa BVR

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetishia kuwa ikiwa viongozi wa kisiasa wataendelea kuingilia uandikishaji wa wapigakura kwa mfumo wa kielektroniki wa Biometric Voters Registration (BVR) haitasita kusitisha uandikishaji huo.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, alitoa tishio hilo wakati akizungumza na wadau mbalimbali wilayami Kilombero, Morogoro baada ya kuhakiki mipaka ya jimbo jipya la Ifakara litakalomegwa kutoka Kilombero.

Alisema hivi karibuni imezuka tabia za viongozi wa kisiasa kuingilia kazi ya tume hiyo katika uandikishaji wa BVR na kusababisha fujo katika vituo vya uandikishaji na kwamba hawatavumilia tena kuona mambo hayo yakiendelea.

Alitolea mfano mkoani Arusha akisema wapo baadhi ya viongozi wa kisiasa wanajifanya wana haki ya kuingilia kazi hiyo na kusababisha fujo na kusema kuwa vifaa vinavyotumia mkoani humo ndivyo vilivyotumika katika mikoa mingine na hakuna malalamiko kama hayo na kuhoji kwa nini mkoa huo unakuwa tatizo.

Hata hivyo, alisema tayari wamepekeka mashine nyingine 10, lakini bado anashangaa viongozi hao wanalalamika na kuahidi kuwa wale wote wanaopaswa kuandikishwa lazima NEC itahakikisha wanaandikishwa hata kwa kuongeza siku na sio kuingiliwa kazi na wanasiasa.

CHANZO: NIPASHE

 
Fateni utaratibu,acheni longolongo.tuambieni watu ambao hawakuandikishwa na zoezi limepita kwenye maeneo yao itakuweje
 
Aache utoto...mbona huwa hamzilii mke wake usiku? sasa anamzilia nani? au anazilia haki na demokrasia?
 
Watu huwa wanampuuza Lema hasa wa ccm tena kipropaganda zaidi, lakini ni ukweli ulio dhahiri serekali hii ilipofikia bila kuwa na watu kama kina Lema mambo mengi ya kizembe, hila nk yatafanyika sana. Hivi leo huyo jaji anadhani watz ni wajinga kwa kutumia kifaa ambacho hakina hata miezi 6 tena kipya kishindwe kufanya kazi kwa usahihi, achia mbali upungufu wa hizo mashine eneo husika. Halafu katika mazingira haya utegemee watu wakae kimya wakati wamapoteza haki yao ya msingi. Jaji afahamu kwenye kujiandikisha kupiga kura wanasiasa ndio vinara kwa hiyo wasipokuwa makini na hizi hila itakula kwao.
 
Mzee wangu huyu angelipumuzika, maana utumishi wake uliotukuka ipo siku utaishia kama wa Ndugu. Kivuitu Kenya 2007.

Nyunyu you have reminded me of one dark page in the history of Kenya Democracy, this was caused by no one but this Samuel Kivuitu.

Samuel Kivuitu (1939-25 February 2013) was head of the now defunct Electoral Commission of Kenya.[1] He was reappointed to his post by the Kenyan President Mwai Kibaki ahead of the 2007 general election, having already been in charge during Kenya's general elections in 1997, 2002 as well as a constitutional referendum in 2005. Samuel Kivuitu was appointed to the post By Daniel Arap Moi replacing Zacchaeus Chesoni, who was the head of the Electoral commission during Kenya's 1992 general election. He was among the people blamed for the elections that lacked transparency in Kenya in the year 2007 which eventually led to post-election violence. He later tried to exonerate himself, arguing that he was, more or less, a puppet of some other forces but those on the losing side could not hear any of it. Some people argue that if that was the case, Kivuitu should have stood up, principled, and resigned instead of presiding over what he knew was a sham election; that if people like him could not stand up firm at a moment of historical significance, then who would protect the common man, and tell him/her what really happened.

Kivuitu was educated in Uganda (1959-61) and Tanzania (1961-65). He was elected MP for Parklands in 1969-74 and 1983-88. He died on 25 February 2013 at the MP Shah hospital after suffering from throat cancer for years, though his death did not receive media attention as promptly as it would have been expected of a person of his status in the history of the country. Kivaitu.jpg
Samuel Kivaitu wakati akiwa afya yake imedhoofu na anajutuia kusasababisha mauaji ya watu 1700 kutokana na kukosa kwake uwajibikaji wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi​
 
Asante mpwa Mama Mdogo, huyuy mzee alitawala media 2007!

Alipomuapisha Pres. Kibaki kana anakimbiziwa Ikulu ya Kenya kuwa Mungu.

R.I.P Kivuitu.
 
Last edited by a moderator:
Hawa ndio wenyeviti wa tume na wakati huohuo ni Wanasiasa..!!

Sasa ikiwa hakuna tatizo hizo mashine kumi wameongeza za nini huko Arusha ikiwa kwa mikoa mingine hizo zilizokuwapo awali huko Arusha ndizo zilizotumika? Akili za kijinga kukiri kosa kwa kulalamikia waliokuonyesha kwamba umekosea..!!! Hivi ni kwanini kiongozi aliyestaafu kwa ngazi ya utumishi Serikalini ndiye anakabidhiwa kazi nyeti kama kuongoza Tume ya Uchaguzi?

Hawa wazee walitakiwa kukaa pembeni waache watu wenye akili zinazochemka sawasawa. Suala la Uchaguzi ni nyeti na sehemu kadhaa tumeona likisabisha vita ndani ya nchi husika. Sasa huyu mzee pamoja na makosa yote ya Tume naw Serikali kwenye suala la BVR, Anadiriki kusimama hadharani kusema nitasitisha zoezi la kandikisha kwasababu wanasiasa wananiingilia.! Hivi hiki kiburi wanapata wapi hawa.!!

Kwahiyo ninyi mlitaka watu wakae kimya tu wasikemee ujinga wenu? Akili hizo zilishakufa kitambo sana.. Akili zilizopo leo zinahoji kila jambo..!! Hata ukikojoa kichakani. ilhali wewe ni mtu mzima mwenye akili tumamu tutahoji sembuse suala la Uchaguzi? Hivi mnadhani tunajisikia raha sana na uongozi wa asamu hii? Mnadhani tunajisikia raha kwa nchi yetu kuzidiwa kiuchumi na vijinchi kama Rwanda? Leo hii dola iko Tsh2200 per one dollar mnadhani tunajisikia raha eeeeeeehhh..!!

Sasa urogwe hata kidogo sitisha zoezi hilo.

BACK TANGANYIKA
 
Aache utoto...mbona huwa hamzilii mke wake usiku? sasa anamzilia nani? au anazilia haki na demokrasia?
Inashangaza mtu kama Lubuva anachachamaa kutokana na wanasiasa wa vyama vya upinzani kusisitiza kuwa kila mwenye haki ya kuandikishwa kuwa mpiga kura ni lazima aandikishwe.

Kwa mazingira ya Tume hiyo inavyofanya kazi, kuna dalili kama vile inaendeshwa na 'remote control' toka mtaa wa Lumumba.

Yapo mambo mengi yanayohusu uandikishwaji huo ambayo walipaswa kuwahusisha wadau wakubwa ambao ni vyama vya siasa, lakini badala yake mambo yao wanayaendesha katika mazingira ya SIRI KUBWA.

Ushahidi wa mazingira unaonyesha kuwa Tume hiyo itakuwa inafanya shughuli zake 'sambamba' na chama cha Sisiem na ndiyo sababu inayofanya chama hicho tawala wawe 'mabubu' pamoja na madudu yote yanayofanywa na Tume hiyo.
 
Lubuva amechoka jamani, sisi tuko Arusha tunaona vifaa vyake feki vinavyo fanya kazi, pia Arusha watu wameamka wanajua umuhimu wa kupiga kura kuchagua wawakilishi wao, tofauti na mikoa ambayo wanabembelezwa kujiandikisha. Hivyo Watu wamejitokeza ili kuichinjia Ccm baharini. Lubuva njoo Arusha acha kuongelea mbali kama mwoga.
Pia Lubuva anatakiwa ajue hutujiandikishi kwenda kumchague yeye na tume yake. Tunakwenda kuchagua wanasiasa, hivyo ni lazima akubali kwamba wanasiasa ni wadau wakuu kwenye hili zoezi. Naahindwa kumuelewa alipokuwa Jaji alikuwa anatoa maamuzi ya aina gani kama hivi sasa hana uwezo wa kupambanua vitu vidogo.
 
Kwa hiyo huyu Babu anataka Watanzania chungu nzima ambao kuna kila dalili ya kudhulumiwa haki yao ya kikatiba ya kujiandikisha na hivyo kuwawezesha kuchagua wawakilishi na Rais wawatakao/wamtakaye wakae kimya na kuruhusu uhuni huu wa MACCM wakishirikiana na NEC.
 
Inashangaza mtu kama Lubuva anachachamaa kutokana na wanasiasa wa vyama vya upinzani kusisitiza kuwa kila mwenye haki ya kuandikishwa kuwa mpiga kura ni lazima aandikishwe.

Kwa mazingira ya Tume hiyo inavyofanya kazi, kuna dalili kama vile inaendeshwa na 'remote control' toka mtaa wa Lumumba.

Yapo mambo mengi yanayohusu uandikishwaji huo ambayo walipaswa kuwahusisha wadau wakubwa ambao ni vyama vya siasa, lakini badala yake mambo yao wanayaendesha katika mazingira ya SIRI KUBWA.

Ushahidi wa mazingira unaonyesha kuwa Tume hiyo itakuwa inafanya shughuli zake 'sambamba' na chama cha Sisiem na ndiyo sababu inayofanya chama hicho tawala wawe 'mabubu' pamoja na madudu yote yanayofanywa na Tume hiyo.

Well said,
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetishia kuwa ikiwa viongozi wa kisiasa wataendelea kuingilia uandikishaji wa wapigakura kwa mfumo wa kielektroniki wa Biometric Voters Registration (BVR) haitasita kusitisha uandikishaji huo.



Kama jaji mzoefu alitakiwa kutambua hilo kuwa haki hudawai na muda mwingine wa watu wengine hupoteza maisha kwa kudai haki ya wengine.



Hata hivyo, alisema tayari wamepekeka mashine nyingine 10, lakini bado anashangaa viongozi hao wanalalamika na kuahidi kuwa wale wote wanaopaswa kuandikishwa lazima NEC itahakikisha wanaandikishwa hata kwa kuongeza siku na sio kuingiliwa kazi na wanasiasa.

CHANZO: NIPASHE

Hili la Muda ndiyo tunalolitaka kusikia na siporojo za kilumumba. Jaji anafahamu fika hesabu za mashine zilizopo na uwezo wa wake na mahitaji yaliyopo ya watu wakuandikishwa na muda ambao Tume yake imeutoa.
 
Aisee Lema ni Mtaalam kila kitu anajua yeye, hata maswala ya BVR alijifunza cuba kabla BVR haijaja hapa.
 
Sasa anamtishia nani?

Huyu kweli hamnazo!! wameshaona ngoma nzito sasa wanaanza kutafuta sababu za kujitoa katika lawama, kwani hili zoezi wangelianza miaka 2,iliyopita kungekuwa na pressure?? kila kitu maandalizi ya kizima moto tu, wao mchakato ule wa vitambulisho vya uraia wangekuwa wameachana nao, kwani hata haukuwa na umuhimu kuliko hili la bvr, hela zenyewe za kuomba unakuwa huna kipaumbele???!! lakini tatizo kila mtu ana kuwa ameshatengeneza mradi wa kulia pesa, likibuma huko mi simo. TZ bwana kuna complications nyingi kuliko hata USA!!!? na zote hata hazieleweki!!!
 
Back
Top Bottom