NEC yatishia kusitisha uandikishaji wa BVR

NEC yatishia kusitisha uandikishaji wa BVR

akumbuke hela wanazotumia ni kodi za watanzani ..hatishiki mtu hapa....
 
Hawa ndio wenyeviti wa tume na wakati huohuo ni Wanasiasa..!!

Sasa ikiwa hakuna tatizo hizo mashine kumi wameongeza za nini huko Arusha ikiwa kwa mikoa mingine hizo zilizokuwapo awali huko Arusha ndizo zilizotumika? Akili za kijinga kukiri kosa kwa kulalamikia waliokuonyesha kwamba umekosea..!!! Hivi ni kwanini kiongozi aliyestaafu kwa ngazi ya utumishi Serikalini ndiye anakabidhiwa kazi nyeti kama kuongoza Tume ya Uchaguzi?

Hawa wazee walitakiwa kukaa pembeni waache watu wenye akili zinazochemka sawasawa. Suala la Uchaguzi ni nyeti na sehemu kadhaa tumeona likisabisha vita ndani ya nchi husika. Sasa huyu mzee pamoja na makosa yote ya Tume naw Serikali kwenye suala la BVR, Anadiriki kusimama hadharani kusema nitasitisha zoezi la kandikisha kwasababu wanasiasa wananiingilia.! Hivi hiki kiburi wanapata wapi hawa.!!

Kwahiyo ninyi mlitaka watu wakae kimya tu wasikemee ujinga wenu? Akili hizo zilishakufa kitambo sana.. Akili zilizopo leo zinahoji kila jambo..!! Hata ukikojoa kichakani. ilhali wewe ni mtu mzima mwenye akili tumamu tutahoji sembuse suala la Uchaguzi? Hivi mnadhani tunajisikia raha sana na uongozi wa asamu hii? Mnadhani tunajisikia raha kwa nchi yetu kuzidiwa kiuchumi na vijinchi kama Rwanda? Leo hii dola iko Tsh2200 per one dollar mnadhani tunajisikia raha eeeeeeehhh..!!

Sasa urogwe hata kidogo sitisha zoezi hilo.

BACK TANGANYIKA

Wameona watu wamestukia kutaka kujiongezea muda wa rais kukaa madarakani sasa wanaendesha zoezi kwa hila maana wanajua watu lazima wapaze sauti zao ila watafute kisingizio. Hivi ndugu yangu inakuingia akilini kweli kifaa kina miezi chini ya sita kinafanya kazi kwa kusuasua hivyo. Kila siku huku kwenye vituo vya kujiandikisha mashine za bvr zinagoma na matatizo lukuki. Na nijuavyo mimi serekali hainunui vitu chakavu, inakuwaje hivi vipya vina mizengwe hivi? Sisi wote tumeshanunua vifaa vya electronic kama laptop, computer, tv, calculator, simu nk. ni nadra sana vifaa hivi kusumbua miezi sita ya mwanzo na mara nyingi vina warranty kiasi kwamba unaweza kurudisha kwa muuzaji ili ubadilishiwe ama hata ikibidi marekebisho. Iweje hivi vya serekali hatuoni hatua stahiki.

Huyu jaji tungemuona wa maana kama mpaka sasa kwenye mikoa waliyopita angetuambia wameandikisha watu wangapi, ni changamoto gani wamekutana nazo na nini suluhisho. Yeye anasubiri mpaka watu kama akina Lema ambao hawana nidhamu za woga wanapoamua kujitoa muhanga kwa faida ya wengi. Kwa taarifa yake watu wengi wanaoadhibika na hili zoezi wamemuunga mkono Lema kuliko anavyodhani wanamuunga mkono yeye.
 
Huyo mstaafu ni bora angeikataa hiyo nafasi ya uenyekiti ili kuitunza heshima yake. Haya ya mashine ni madogo sana asubiri kimbembe siku ya uchaguzi ndo ataijua ladha ya dhuluma na kujutia u-ccm wake. Namhurumia.
 
Huyu Jaji Lubuva wa ccm amelewa madaraka kwani hizo mashine ni mali ya ccm .Anamtishia nani
 
Wameona watu wamestukia kutaka kujiongezea muda wa rais kukaa madarakani sasa wanaendesha zoezi kwa hila maana wanajua watu lazima wapaze sauti zao ila watafute kisingizio. Hivi ndugu yangu inakuingia akilini kweli kifaa kina miezi chini ya sita kinafanya kazi kwa kusuasua hivyo. Kila siku huku kwenye vituo vya kujiandikisha mashine za bvr zinagoma na matatizo lukuki. Na nijuavyo mimi serekali hainunui vitu chakavu, inakuwaje hivi vipya vina mizengwe hivi? Sisi wote tumeshanunua vifaa vya electronic kama laptop, computer, tv, calculator, simu nk. ni nadra sana vifaa hivi kusumbua miezi sita ya mwanzo na mara nyingi vina warranty kiasi kwamba unaweza kurudisha kwa muuzaji ili ubadilishiwe ama hata ikibidi marekebisho. Iweje hivi vya serekali hatuoni hatua stahiki.

Huyu jaji tungemuona wa maana kama mpaka sasa kwenye mikoa waliyopita angetuambia wameandikisha watu wangapi, ni changamoto gani wamekutana nazo na nini suluhisho. Yeye anasubiri mpaka watu kama akina Lema ambao hawana nidhamu za woga wanapoamua kujitoa muhanga kwa faida ya wengi. Kwa taarifa yake watu wengi wanaoadhibika na hili zoezi wamemuunga mkono Lema kuliko anavyodhani wanamuunga mkono yeye.

Mkuu tindo,

Hilo jambo liko wazi nao wanajua wazi kwamba Lema kawashika vilivyo, hawana pa kupumulia. Mpango wao mbaya dhidi ya Lema kwa Arusha utagonga mwamba, ole wao sajaribu kuchakachua iwe ni kura au kuandikisha wapiga kura.

BACK TANGANYIKA
 
Umejitahidi sana kuandika lakini hueleweki, Lema hana utaalam wa BVR asipotoshe watu, hajasomea popote BVR wala hakuna shahada ya BVR.

Sasa ndugu yangu Stroke nikusaidieje, ikiwa andishi la paragraph moja tu umeshindwa utaelewa nini mkuu? Wewe kuanzia leo amua kuwa msomaji, utakapokidhi viwango vya kuelewa ndipo uanze ku-argue na wanajukwaa hapa.. Huu ni ushauri wa bure..!!!

BACK TANGANYIKA
 
Akiwa anaongea na ITV kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku huu Jaji Lubuva amesema "Kama wanasiasa wataendelea kuingilia zowezi la uandikishaji wa BVR nitaondoa mashine za BVR na kusitisha zoezi la uandikishaji"
 
Huyu mzee kashiba sasa anaanza kuropoka!
Hana uwezo wa kusitisha zoezi! Ni ulevi tu wa madaraka na kuropoka!

Kama anaona wanasiasa wanavunja sheria taratibu zipo za kufanya na sio kuropoka eti atasitisha zoezi wakati anajua uwezo huo hana!!
 
Huyu mzee anazeeka vibaya... Anafikiri kuandikisha bvr ni sawa na kulipa bili ya maji?

Mwambieni aache usengerema kuandikishwa ni haki ya kikatiba yeye hana mamlaka ya kunyima watu haki ya kupiga kura na kuchagua viongozi wawatakao.

Cheo chenyewe cha kuwekwa na mtu.
 
Jamani wazee tuwaheshimu kwa kuwapa kazi zisizowaumiza. Mnamtesa sana huyu babu.
 
Sijui alikunywa soda ya wapi?

Wavivu wa kufikiri ndo wateule wa mzee wa tezi dume.

kwa nini asiwashughulikie?

Atakuwa alikula limao huyoo....
 
Wadau hivi hela na fines za parking wanazokusanya hii kampuni zinaenda wapi maana hamna maboresho yoyote ya parking lots wala barabara.

Naona wameanza uhuni mwingine wa kusema baadhi ya parking spaces zina watu.Wengine tukapaki wapi?

Pia wameanza kuvizia maeneo nje ya katikati ya mji ambayo yana offices zilizo busy kama bank branches wanasema eneo la parking ni la kulipia.

Wanakeraaaaa.
 
Mimi nilidhani atajihudhuru kumbe ni kuondoa mashine lakin aendelee kula kodi za wananchi bila kazi.Kazi kwelikweli
 
Huo ni ufisadi mwingine wa serikali ya CCM na familia ya Kingunge.
 
Huyu Mzee sijuhi alikula maharage ya wapi leo..... Hivi anafikiri kujiandikisha daftari la wapiga kura ni hisani ambayo anaweza kusitisha apendavyo...???

Nimegundua kumbe majaji wakizeeka wanageuka kumbikumbi.....!!
 
Mradi wa Kingunge huo. Anadhani EL akiwa Rais ataendelea kula bila kunawa.
 
Back
Top Bottom