Uchaguzi 2020 NEC yataka wagombea wasiwe na matokeo mfukoni

Hii idadi ya wapiga kura ni ya kupika, na ndio maana NEC hawataki watu walinde kura, na sasa kuruhusu matumizi ya passport, driving license nk kupigia Kura. Hii ya yote ni kuhakikisha yanapatikana matokeo waliyoyapanga.
Sio kila kitu unapinga tu kisa upo Chadema. Daftali la kudumu kila chama kimekabidhiwa hiyo idadi ya kupika inatoka wapi?

Unataka wananchi walinde kura kwa sheria ipi?

Driving licence na Passport zitatumika kama mtu amaepoteza kadi ya kupigia kula. Na majina lazima yafanane.

Alafu mmefanya fitina mmechongea Pascal Mayalla amepigwa ban
Kwani ushindi upo Jf?
 
Misungwi tuuu kuna vituo 'hewa' 79, Pemba jumla ya vituo hewa 94, shinyanga mjini vituo hewa 122, tukisema hii tume ya huyo mpumbavu inataka kuleta vita vya wenyewe kwa wenyewe ma CCM yanalalama eti kuna watu wanataka kuleta vurugu…………...pambafuu zao!
 
Nec tunajua nyie ndio waharibifu wakubwa wa uchaguzi kwani tayari mna matokeo ktk mabegi yenu! Acheni uchoro!
 
Kwanini swali kuhusu hizi takwimu huwa hawaulizwi NEC na waandishi wa habari ama vyama vya siasa vishiriki ili kujua ukweli na uhalali wa takwimu hizi?

Na mwaka 2015 hivi kulikuwa na wapiga kura wangapi halali walioandikishwa?

Kati ya 2015 na 2020 wameongezeka wangapi? Projection ya ongezeko hili in relation to the county's total population ikoje agewise? Je ingezeko hili linakubalika?

Maana kwa mfano tu;

Kama ongezeko ni wapiga kura 9,000,000 toka 20,000,000 wa mwaka 2015 na kuwa 29,000,000..

Swali litakuwa ongezeko hili linawiana na population yenye sifa za kuwa wapiga kura ambao mwaka 2015 hawakuwanazo hizi sifa..?

Basically, hata mimi takwimu hizi za NEC zinanipa mashaka makubwa. Siziamini hata kidogo..!

Ni eneo lingine hatari na lililojificha na wanaotaka kushinda kwa nguvu watalitumia kuiba kura..!!
Acha uongo 2015 wapiga kura waliojiandikisha walikuwa milioni 24 sio milioni 20 .Ongezeko ni milioni 5 sasa hivi

Takwimu zako wewe ndio za uongo
 
Kwanza hata idadi ya wapiga kura wanaotangazwa na nec sio kweli, idadi imepikwa ili kuwepo na kura za kughushi kwani hii ndio kawaida ya Nec-ccm.
 
NEC ni wapumbavu sana,kwa mfano huko Tanga jimbo moja wamewaengua wagombea udiwani wa upinzani 16 kati ya 21 kwa sababu za kijinga kabisa...hapo huyo Mahera alikuwa anaongea upumbavu gani sijui
 
We punguwani kweli yani mtu unamuona barabarani anaomba kura bado unasema ana tegemea kubebwa jinga sana.
Unaelewa kuwa mtu kuwa barabarani kwa ajili ya kuomba kura siyo kigezo cha kuthibitisha kuwa hategemei kubebwa?Unaelewa kuwa mtu ambae anategemea kubebwa anapaswa kuwa barabarani ili kuzuga wananchi kuwa na yeye yumo kwenye kinyang'anyiro?
 
Sio kila kitu unapinga tu kisa upo Chadema. Daftali la kudumu kila chama kimekabidhiwa hiyo idadi ya kupika inatoka wapi?

Unataka wananchi walinde kura kwa sheria ipi?

Driving licence na Passport zitatumika kama mtu amaepoteza kadi ya kupigia kula. Na majina lazima yafanane.

Alafu mmefanya fitina mmechongea Pascal Mayalla amepigwa ban
Kwani ushindi upo Jf?

Kukabidhiwa daftari ni jambo moja, ila kuhakiki inachukua muda. Vuta subira kwenye hili. Wananchi wanalinda kura baada ya kuona uhuni wa wazi kwenye chaguzi zetu. Watunga sheria hawawezi kutunga sheria ya kulinda kura, maana wao ni wafaidika wa huo wizi wa kura.

Tume hii imekataa mambo na mapendekezo mengi ya kupiga kura, lazima tuwe na shaka na huu wema wa dakika za mwisho. Ikumbukwe watu waliboresha taarifa mpaka mwezi wa tano, hivyo waliopoteza kadi walikuwa na muda wa kupata nyingine.

Tumchongee Paskali kwa lipi, kwanza ww ndio unaniambia kapigwa ban wala mimi sijui.
 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wagombea wanaowania nafasi za kuchaguliwa kupitia Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani, utakaofanyika wiki ijayo waache kuwa na matokeo mifukoni mwao, bali watambue kuna kushinda na kushindwa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk Willson Mahera, alitoa tahadhari hiyo kwenye kongamano la amani, lililoandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Twariga jijini Arusha.

Alitahadharisha kuwa wagombea wakiamini ni lazima watashinda, itasababisha vurugu na uvunjifu wa amani matokeo yakitoka tofauti na matarajio yao.

“Tatizo ninaloliona wapo baadhi ya wagombea wanakwenda kupiga kura wakijiaminisha tayari wameshashinda na inapotokea wameshindwa kihalali wanakataa matokeo,” alisema.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na viongozi wa dini, wa vyama vya siasa na wa mila wa makabila mbalimbali mkoani humo kwa lengo la kusisitiza wananchi walinde amani wakati huu nchi ikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu.

Dk Mahera alisema NEC itahakikisha inatenda haki na kuwatangaza wagombea watakaoshinda kihalali kwenye nafasi ya urais, ubunge na udiwani.
Aliwataka wagombea watakaoshindwa, wakubali matokeo na wasiwe sehemu ya kuanzisha vurugu.

“Mgombea yeyote atakayeshinda uchaguzi atatangazwa bila kujali anatoka chama kipi cha siasa hivyo wanaotaka kujitangaza kuwa wameshinda kabla ya upigwaji kura wanajidanganya,” alisema.

Dk Mahera alisema NEC itatenda haki kwa kila mgombea kwa kuzingatia sheria za uchaguzi, katiba ya nchi, kanuni na taratibu za uchaguzi na si vinginevyo.

Kuhusu madai kuwa matokeo ya baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani hubadilishwa, Dk Mahera alisema jambo hilo haliwezi kutokea kwa kuwa sheria hairuhusu kubadili matokeo ila kumtangaza mtu aliyeshinda kwa kupata kura nyingi kuliko wagombea wengine.

“Vyama vya siasa vitaweka mawakala kwenye vituo vya kupigia kura na wakati wa kuhesabu kura na wakati wa kutangaza matokeo watashiriki kikamilifu, hivyo siyo rahisi mawakala wa vyama vyote wawepo kwenye vituo halafu matokeo ya kura kubadilishwa,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi katika kongamano hilo, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini na Kati, Naibu Katibu Mkuu wa Misioni na Uinjilisti, Jasson Kahembe, aliwataka wananchi kutambua kuna maisha baada ya uchaguzi hivyo waepuke vurugu.

“Kuna maisha baada ya uchaguzi, Tanzania kwanza watu wasifikirie leo bali waangalie na kesho itakuwaje, neno la Mungu kutoka kitabu kitakatifu cha Biblia linasema haki huinua taifa bali dhambi ni aibu kwa watu wote,” alisema.

“Mungu aliwaahidi wana wa Israel kama watamsikiliza, kumtii na kufuata maagizo yake atawabariki, lakini pia aliwaambia watalaaniwa kama watakwenda kinyume na maagizo yake, hivyo taifa lenye utii mbele za Mungu hubarikiwa.”

“Tunapoelekea katika uchaguzi tutambue tunataka mafanikio ya Watanzania na siyo ya tunaowapenda, hivyo tuchague aina ya maisha tunayohitaji kuishi na siyo watu tunaowapenda sisi, pia tusifurahishwe na maneno mazuri ya wagombea wakiwa majukwaani kwa kuwa hizo ni harakati za kutafuta mchumba na uzuri, lakini ubaya wa mchumba hujulikana baada ya harusi,” alisema.

Msemaji wa Taasisi ya Kiislamu ya Twariqa, Shehe Haruna Hussein aliwataka viongozi wa dini wasimame kwenye nafasi yao, wahubiri amani, wasiwe sehemu ya wanasiasa na wasiwachagulie wananchi mgombea, kwa kuwa wakifanya hivyo wanawagawa waumini.

“Viongozi wa dini hatupaswi kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa kusema mgombea huyu anafaa kuwa kiongozi na mgombea mwingine hafai, naomba tuache wananchi wafanye uamuzi wao wenye kwenye sanduku la kura,” alisema Shehe Haruna.

HabariLeo
Tumeccm NECCCM sasa ni makada wa CCM nao wapo kwenye kampeni za CCM, hivi hawaoni kule Same magufuli katoa Rushwa live kwa kutoa pesa kutekeleza miradi, Tumeccm NECCCM sasa si tume ya uchaguzi bali na wao wanaipigia debe CCM
 
Kukabidhiwa daftari ni jambo moja, ila kuhakiki inachukua muda. Vuta subira kwenye hili. Wananchi wanalinda kura baada ya kuona uhuni wa wazi kwenye chaguzi zetu. Watunga sheria hawawezi kutunga sheria ya kulinda kura, maana wao ni wafaidika wa huo wizi wa kura.

Tume hii imekataa mambo na mapendekezo mengi ya kupiga kura, lazima tuwe na shaka na huu wema wa dakika za mwisho. Ikumbukwe watu waliboresha taarifa mpaka mwezi wa tano, hivyo waliopoteza kadi walikuwa na muda wa kupata nyingine.

Tumchongee Paskali kwa lipi, kwanza ww ndio unaniambia kapigwa ban wala mimi sijui.
Mnafiki mkubwa weee. Unajifanya hujui kapigwa ban? Mashambulizi ya wanaCcm yamewazidia msaada mkubwa kwenu ni ban.
Kama daftali la wapiga kura mmekabidhiwa wasiwasi wa nini?

Wananchi walinde kura kinyume na sheria za nchi? Acha siasa za kihuni.
 
CCM bila Polisiccm bila Tumeccm bila mahakamaccm bila wakurugenziccm bila Msajiliccm bila uchakachuaji bila wizi wa kura ni weupe sana
 
Tumeccm NECCCM sasa ni makada wa CCM nao wapo kwenye kampeni za CCM, hivi hawaoni kule Same magufuli katoa Rushwa live kwa kutoa pesa kutekeleza miradi, Tumeccm NECCCM sasa si tume ya uchaguzi bali na wao wanaipigia debe CCM
Magufuli anatekeleza majukumu kama rais wa JMT anatoa pesa kutekeleza miradi kama mkuu wa nchi tumia akili we Minyoo.
 
Mnafiki mkubwa weee. Unajifanya hujui kapigwa ban? Mashambulizi ya wanaCcm yamewazidia msaada mkubwa kwenu ni ban.
Kama daftali la wapiga kura mmekabidhiwa wasiwasi wa nini?

Wananchi walinde kura kinyume na sheria za nchi? Acha siasa za kihuni.
Sheria inaruhusu kulinda kura ukiwa mita kadhaa , Lakini Tumeccm NECCCM kwa njia haramu za kishetani walizokariri toka CCM yao wanazua watu kulinda kura zao zisiibiwe na CCM
 
Back
Top Bottom