Sumve 2015
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 4,420
- 4,062
Mkurugenzi ndiye huteua miungoni mwa majina alopelekewa mwaka ule na tiari keshatangaza wabunge wateule kwenye taarifa ya TBC mchana.Mkuu siyo kazi ya NEC kubariki kufukuzwa kwa mwanachama yeyote ktk chama chochote. Wala hakuna chama kinachohitaji baraka za mtu yeyote kinapomfukuza mwanachama wake kwa kikao halali kinachotambulika na katiba ya chama husika.
Mwanachama ambaye ni mbunge akifukuzwa spika wa bunge anaandikiwa na chama husika barua ya kumjulisha kufukuzwa kwa mwanachama huyo. Naye spika akishapitia barua hiyo na kujiridhisha kwamba ni kweli mwanachama huyo amefukuzwa, naye anachukua jukumu la kuitaarifu Tume ya Uchaguzi(NEC).
NEC ikishapokea taarifa ya spika nayo inatangaza nafasi zile za hao wabunge kuwa ziko wazi. Kama ni wa kuteuliwa kuna huo utaratibu ambao umeuelezea hapo juu, sina haja ya kurudia. Kama ni wa kuchaguliwa NEC watatangaza tarehe siku na muda wa kufanya uchaguzi kwa ajili ya kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi.