NEC yabariki kufukuzwa wabunge 8 wa CUF na kutaka majina mapya kwa ajili ya uteuzi

Nikiona mtu anashangilia na kufurahia kwa kinachotokea CUF napata shida sana kumwelewa kama kweli anatumia akili au amezikalia, ila wahenga walishawahi kusema kwa kigogo "What goes around comes around"
 
Ni dhambi kubwa sana kuliko zote hapa duniani kumnyima mtu haki yake anayostahili. Sidhani kuomba kuombewa ombewa kunaweza kumwondolea mtu dhambi hii.

Fanya zambi zote duniani lakini kwepa mno kupoka haki ya mtu anayostahili.
Alikuwa Rwanda akila bata wenzake wakihangaika..yote yana mwisho aendae India bahati kurudi akiwa na jina lile lile..
 
ubunge nao ni ajira?
maalimu kawa magufuli na genge lake la msajili wa vyama + bunge na lita.
 
Option ya kwenda Mahakamani ingepata nguvu lakini tuna kaimu jaji mkuu! Hili suala liko wazi na kuna kitu kitatokea kuwafumbua macho hata walio usingizini, hapo ndipo waliotoa haya maamuzi ya 'supersonic' watatamani kuyakana!
 
Sasa wewe kada badala ya kumlaumu huyo pandikizi lenu Profesa, wewe unamlaumu Maalim Self?

Lakini hii dhambi inayofanywa na CCM wakishirikuana na mshirika wao Lipumba, haitawaacha salama....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ha ha ha kina Maalim walifanya uzembe.
Kwa kufuatana na katiba ya Cuf walitakiwa kukaa kikao na kukubali Prof kujiuzuru ndani ya miezi 6.
Ikipita miezi sit bila kuthibitisha unarudi kwenye nafasi yako.
Sasa Lipumba alivorudi wakaanza kung'aka we msaliti ulikimbia mwenyewe...
Ukiuliza swali katiba inasemaje hakuna atakayekujibu.....je mlichagua mwenyekiti mpya....hakuna jibu..
Lipumba kawapiga technical knock out ya hatari.

Huyu profesa kweli hayuko wrong haki iko upande wake.,kwa makosa ya kimangimeza ya maalim.
Ila karma itafanya kazi yake.,
 
Ha ha ha kina Maalim walifanya uzembe.
Kwa kufuatana na katiba ya Cuf walitakiwa kukaa kikao na kukubali Prof kujiuzuru ndani ya miezi 6.
Ikipita miezi sit bila kuthibitisha unarudi kwenye nafasi yako.
Sasa Lipumba alivorudi wakaanza kung'aka we msaliti ulikimbia mwenyewe...
Ukiuliza swali katiba inasemaje hakuna atakayekujibu.....je mlichagua mwenyekiti mpya....hakuna jibu..
Lipumba kawapiga technical knock out ya hatari.
Kwa anayewaza ruzuku na ujinga mwingine anaona akina Maalim walifanya uzembe lakini kwa anayewaza chama na demokrasia ndio anaona walivyotumia busara ya hali ya juu mpaka kuiongeza hata hiyo ruzuku yenyewe. Naweza kukuhakikishia pasi shaka kuwa Lipumba alifanya utafiti mpaka kupata PhD hadi uprofesa lakini miaka michache ijayo wanazuoni wengine watakuwa wanafanya utafiti kujua huyu profesa ni nani hasa na ni nani wanaweza kushirikiana naye kufanya wanayoyafanya. Hapo wazungu ndipo wanasema 'time will tell'!
 
Mkuu jana kuna post ilitumwa humu kwamba Seif atafute njia mbadala ya kumuondoa msaliti Pumba kwa sababu wale watu anaotegemea kumsaidia kutetea haki ni wateule wa mwenyekiti was ccm; "Majagi", Mwenyekiti was NEC, Polisi, Mlezi wa vyama, na wengineo. Ndiyo haya tunayaona.
Utaona hata Spika ni mfuasi wa mkuu. Njia mbadala itafutwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo maana tunasema CUF Maalim wawe na plan B. Na hii isivuke 2018 ili wajipange kwa uchaguzi wa 2020.
 
Ni nani atakayebeba dhambi kati ya profesa na Maalim?

Huyu pr asiyejielewa alikimbilia Rwanda baada ya kubeba hela za ccm wakabaki wakina maalimu wanapambana,wakawachagua wabunge wa viti et this time liprofesa linatengua uteuzi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
NEC nayo yakubari kufutwa kwa Ubunge wa Wabunge nane wa Cuf !! yaitaka Cuf kuteua Majina nane (8) kutoka ktk orodha iliyo wasilishwa Ktk Ofisi ya Tume siku kumi na tano(15) kabla ya Uchaguzi wa 2015.

Ni wazi suala la Ubunge wa waliokua Wabunge hao nane (8) umekoma rasmi
Punde Cuf kutangaza majina nane (8) yanayo ziba nafasi zao.

Ramadhan Kailima, Mkurugenzi wa NEC amethibisha.

Ndani ya siku tatu kazi aliyotumwa imetimia wakati kesi yake inaenda mwaka kwa maagizo toka juu imekaliwa
Mbona Lissu amepata dhamana
 
Si waitishe uchaguzi wao mkuu tu kuchagua wenyeviti na makatibu fitna iishe?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tayari wako kambi mbili tofauti-nani ataitisha uchaguzi wakati anajua atapoteza. Ndo maana prof. alikwenda kuvunja mkutano wa wenzake na toka hapo wakaanzisha CUF mbili. Kwa kura za halali sidhani kama prof.ana pakutokea kwa hivyo nia yake awe na mkutano mkuu utakao muunga yeye mkono ili uchaguzi kama ungefanyika awafurushe hawa wengine. Lakini anajua hakuna kukaa pamoja sasa anawalia timing ya kisheria wafukuzwe chamani.
 
mbaya zaidi wanafanya waziwazi kiasi kila mtanzania anajua mchezo huu unavyochezwa. dhambi kama hizi huwa hazisameheki hata uombewe kiasi gani.
Sio kila Mtanzania. Ni sehemu ndogo sana ya Watanzania wanayaona na kuyang'amua mambo haya. Sehemu kubwa ya Watanzania (zaidi ya 95%) hawafikirii kwa makini
 
Back
Top Bottom