BUNGE: Hatuwatambui wabunge 8 wa CUF waliorudishwa na Mahakama

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
BUNGE limeweka wazi kuwa hawatambui wanachama wanane waliovuliwa uanachama na Chama cha Wananchi (CUF) na baadaye kutangazwa kuvuliwa nafasi zao za ubunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Taarifa hiyo ya Bunge, imetokana na barua ya CUF kwenda kwa Katibu wa Bunge, Stephen Kigaigai inayomtaka amjulishe Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai, kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu ya kutengua uamuzi wa awali wa chama hicho wa kuwafuta uanachama wa wabunge hao na kuomba Bunge liwatambue kama bado ni wabunge halali.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu taarifa hiyo ya Mahakama Kuu kutengua uamuzi wa awali wa CUF wa kuwafukuza uanachama wabunge hao, Kigaigai alikiri kupokea barua ya chama hicho, lakini alisisitiza kuwa bado chombo hicho hakiwatambui kama wabunge halali.

“Ndio nimeipata barua yao na naanza kuifanyia kazi, ila kifupi tu Bunge haliwatambui watu hao. Sisi tunawatambua wabunge wapya tuliopatiwa orodha na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),” alisisitiza.

Alisema kwa kawaida Bunge hupokea majina ya wabunge wote, wanaoingia ndani ya chombo hicho kutoka NEC na si kwa chama husika, hivyo mpaka sasa hawajapata barua yeyote kutoka kwa tume hiyo, inayobainisha uhalali wa watu hao kuwa wabunge.

Wanachama hao waliokuwa wabunge wa viti maalumu, baada ya kuvuliwa uanachama wao Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kutokana na ukosefu wa nidhamu, walikosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.

Wanachama hao ni Saumu Heri Sakala, Salma Mohamed Mwassa, Raisa Abdallah Mussa, Miza Bakari Haji, Khadija Salum Ally Al-Qassmy na Halima Ali Mohamed. Baada ya kuvuliwa uanachama na kuvuliwa ubunge, NEC ilitangaza majina ya wabunge wapya waliochukua nafasi za wabunge, ambao tayari waliapishwa na wanaendelea kulitumikia Bunge hilo

Chanzo: Habari Leo
 
Serikali inabomoa nyumba za watu and now..Bunge linazarau Mahakama

Tume ya uchaguzi haitahojiwa mahakamani

Wananchi wamekunyima Kura, ....halafu unawapora kura na kutangaza kuwa mnapendwa na mmeshinda, hivi huu ni uhayawani? Unamtangazia nani kuwa umeshinda au unapendwa? unayemtangazia huyo amekunyima kura..>Shameeee

UVCCM na Usalama kukata wananchi mapanga ni laana, Mungu atawaadhibu....Ndio maana uchumi unaporomoka na mumekuwa vipofu....mnasema umekuwa..Kwa sababu tu mfalme anakupa makombo....

Hao Madiwani waliopewa ushindi kwa hila, walaaniwe na wafe au waparalyse

Wananchi musiwape ushirikiano, muwazomee na kuwapa tabu mbali mbali....hata kuvamiwa na kupigwa

Hii ndio sababu ya kuzaa vikundi vya ugaidi..

Amani ni tunda la haki...

Mwisho, wasanii watunge nyimbo nyingi sana kuhusu unyama unaofanywa na kukata watu Mapanga

[HASHTAG]#romazimbabwe[/HASHTAG]
[HASHTAG]#neywamitego[/HASHTAG]
 
mimi sijui jamani hivi uamuzi wa mahakama unahitaji baraka za tume? wanasheria watusaidie.
Uamuzi huwa unalenga mtu au taasisi, siyo kila mtu au taaisi. Maamuzi yaliyopinduliwa ni yale ya Tume, ambayo iliwatambua wabunge wapya.
 
mimi sijui jamani hivi uamuzi wa mahakama unahitaji baraka za tume? wanasheria watusaidie.
Kama hoja ni kutambuliwa Mahakama Basi mahakama ndiyo ingeiandikia Barua Bunge NA SIYO WABUNGE WENYEWE

Hakuna Mbunge anayetoa taarifa Bungeni kuhusu Uhalali wake Wa kuwa Mbunge ..Ni Tume tu na SIYO Vinginevyo

Hata hao waliochukua nafasi badala yao Hawakuandika Barua wao wala Lipumba hakuandika Barua kwenda kwa Bunge Bali alipeleka Barua yake Tume ya Uchaguzi...wale ndio hupeleka taarifa Bungeni

My take:- Hebu mahaba tuwekage pembeni wakati mwingine ili tuwashauri wahusika vizuri lengo ni kufanikisha

Sorry kama nimekukwaza mkuu
 
BUNGE limeweka wazi kuwa hawatambui wanachama wanane waliovuliwa uanachama na Chama cha Wananchi (CUF) na baadaye kutangazwa kuvuliwa nafasi zao za ubunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Taarifa hiyo ya Bunge, imetokana na barua ya CUF kwenda kwa Katibu wa Bunge, Stephen Kigaigai inayomtaka amjulishe Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai, kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu ya kutengua uamuzi wa awali wa chama hicho wa kuwafuta uanachama wa wabunge hao na kuomba Bunge liwatambue kama bado ni wabunge halali.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu taarifa hiyo ya Mahakama Kuu kutengua uamuzi wa awali wa CUF wa kuwafukuza uanachama wabunge hao, Kigaigai alikiri kupokea barua ya chama hicho, lakini alisisitiza kuwa bado chombo hicho hakiwatambui kama wabunge halali.

“Ndio nimeipata barua yao na naanza kuifanyia kazi, ila kifupi tu Bunge haliwatambui watu hao. Sisi tunawatambua wabunge wapya tuliopatiwa orodha na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),” alisisitiza.

Alisema kwa kawaida Bunge hupokea majina ya wabunge wote, wanaoingia ndani ya chombo hicho kutoka NEC na si kwa chama husika, hivyo mpaka sasa hawajapata barua yeyote kutoka kwa tume hiyo, inayobainisha uhalali wa watu hao kuwa wabunge.

Wanachama hao waliokuwa wabunge wa viti maalumu, baada ya kuvuliwa uanachama wao Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kutokana na ukosefu wa nidhamu, walikosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.

Wanachama hao ni Saumu Heri Sakala, Salma Mohamed Mwassa, Raisa Abdallah Mussa, Miza Bakari Haji, Khadija Salum Ally Al-Qassmy na Halima Ali Mohamed. Baada ya kuvuliwa uanachama na kuvuliwa ubunge, NEC ilitangaza majina ya wabunge wapya waliochukua nafasi za wabunge, ambao tayari waliapishwa na wanaendelea kulitumikia Bunge hilo

Chanzo: Habari Leo
unaomba hukumu ya mahakama
 
Kama hoja ni kutambuliwa Mahakama Basi mahakama ndiyo ingeiandikia Barua Bunge NA SIYO WABUNGE WENYEWE

Hakuna Mbunge anayetoa taarifa Bungeni kuhusu Uhalali wake Wa kuwa Mbunge ..Ni Tume tu na SIYO Vinginevyo

Hata hao waliochukua nafasi badala yao Hawakuandika Barua wao wala Lipumba hakuandika Barua kwenda kwa Bunge Bali alipeleka Barua yake Tume ya Uchaguzi...wale ndio hupeleka taarifa Bungeni

My take:- Hebu mahaba tuwekage pembeni wakati mwingine ili tuwashauri wahusika vizuri lengo ni kufanikisha

Sorry kama nimekukwaza mkuu

Basi cuf waindakie tume na tume iitaarifu bunge tuone itakuaje
 
Back
Top Bottom