NAKUMBUKA.
1. Tarehe 24/7/2017: Baraza kuu (Feki) la uongozi CUF liliwafukuza uanachama wabunge 8 na madiwani 2.
2. Tarehe 25/7/2017: Ofisi ya bunge ilipokea barua ya kufukuzwa kwa wabunge hao, wakati huo Mh. Ndugai akiwa nje ya nchi.
3. Kesho yake tarehe 26/7/2017 ofisi ya bunge ilitoa taarifa kwa maandishi kuwa Spika wa bunge ameridhia barua ya kufukuzwa kwao na kwa sababu hiyo wabunge hao wamekosa sifa za kuwa wabunge na tayari ameitaarifu tume ya uchaguzi ya taifa NEC.
4. Kesho yake yaani tarehe 27/7/2017 NEC ikasema imepokea taarifa kutoka ofisi ya bunge na tayari imeshateua majina 8 ya kujaza nafasi za wabunge wa viti maalumu.
Sitaki kujua hayo majina yalifika lini NEC na yaliteuliwa na chombo gani, lakini lengo langu ni kutaka kujua ni sababu zipi zimemfanya Spika kuwa mzito kutoa maamuzi ya ofisi yake kuhusiana na hukumu iliyotolewa tangu juzi trh 10/11/2017 iliyotengua kuvuliwa uanachama kwa wabunge 8 wa CUF.
Ile spidi aliyotumia wakati ule kuridhia barua ya Lipumba ya kutenguliwa kwao akiwa ughaibuni mbona haionekani wakati huu ambapo yupo nchini, hata tamko tu kutoka ofisi ya bunge kuwa tumesikia lakini hatujapokea hukumu rasmi hakuna?
Ni kitu gani kimeisibu ofisi yetu ya bunge au anasubiri maelekezo toka juu.
====================================
Hawa ndio wabunge 8 halali wa CUF waliofukuzwa kwa hila na Lipumba.