Tume ya uchaguzi NEC imebadilisha matokeo ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Vunjo baada ya kugundua ilitangaza matokeo tofauti na yale yaliyotangazwa awali na msimamizi wa uchaguzi.
Nec imetangaza matokeo mapya ya Jimbo la Vunjo yanayoonyesha kuwa mgombea wa TLP, Augustine Mrema alipata ushindi wa asilimia 54 na si 50 kama ilivyotangazwa awali.
Mabadiliko ya matokeo ni kama ifuatavyo kura za zamani kwenye mabano
Augustine Mrema TLP 30,810 (29,047)
Chrispin Meela CCM 23,870 (17,498),
John Mrema Chadema 6,558 (6,316)
Lyimo wa NLD kura 811 (118)
Pia idadi halisi ya wapigakura imebadilika kutoka 55,013 iliyotangazwa awali hadi kufikia 55,102 ya sasa huku idadi ya kura halali sasa ikiwa ni 53,914 tofauti na kura halali 53,705 zilizotangazwa awali.
Kutokana na hali hiyo, Mrema ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mazingira ya mabadiliko hayo ya kura, akisema kuwa anahisi kulikuwepo na njama za kuchakachua matokeo ambazo ziligonga mwamba.
My take: Kwa sababu kasoro za matokeo zinazidi kuongezeka, ili kuondoa manung'uniko kwa wananchi kuna haja ya kuundwa kwa tume huru kuchunguza uhalali wa matokeo. Serikali zinazoongoza huku wananchi wake wakinung'unika mara nyingi huwa hafanikiwi na hukumbwa na mikosi mbalimbali kwenye utawala wake.
Sahihisho kidogo Meela wa CCM kura za sasa ni 17,498 badala ya 23,870 alizopewa awali ina maana ailkuwa ameongezewa kura 6,372 zaidi.Hizo kura jumla yake ni 62,049. Hivyo hata haya marekebisho hayako sahihi.
Kisheria, tume ikishatangaza matokeo inayoweza kutengua ni mahakama. Kwa hiyo sasa hivi tume kazi yake imemaliza. Waiache mahakama iendelee na kazi zake.
Swali: Je, ni nini kilikuwa chanzo cha tume kufanya marekebisha/masahihisho haya? kulikuwa na malalamiko au?
Dah kumbe ndo wanavyofanyaga ehe?..Hii imenifungua macho mazee!..This being the case all election results can not be trusted.Sahihisho kidogo Meela wa CCM kura za sasa ni 17,498 badala ya 23,870 alizopewa awali ina maana ailkuwa ameongezewa kura 6,372 zaidi.
Lakini total bado inazidi idadi ya waliopiga kura ukijumlisha unapata kura 55,677 lakini wao wanasema kura halali ni 53,914 hii imekaaje, asante ZeMarcopolo kwa kunote hilo.
2015 Watasema hata matokeo ya Urais yalikosewa
matokeo yote yakianza kupitiwa namna hii tunaweza kujikuta tunaingia matatizoni tu..
Kuna watu 6 nchini Kenya ambao mwanzoni mwa mwaka kesho watakuwa wamekwisha fikishwa mbele ya ile mahakama ya kimataifa (ICC) kutokana na vurugu zilizofuatia uvurugaji wa uchaguzi mkuu nchini humo. Nafahamu kuwa mahakama yetu haina ubavu wa kumshughulikia Makame na genge lake. Hivi ushahidi wa namna hii hautoshi kuwapeleka ICC, au mpaka watu wawe wamekufa!