Kadoda nguku
JF-Expert Member
- Apr 22, 2019
- 332
- 475
Uchaguzi umekwisha , na wajumbe wa NEC wamechaguliwa.
Itoshe kusema kanda ya ziwa ndio walio shinda kwa kurudi na wagombea wao wote.
Matokeo Uchaguzi wa Wajumbe wa NEC-CCM Kwa Upande wa Tanzania Bara
👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼
Mkutano wa kumi wa CCM umefanyika na haya ndio majina ya wajumbe waliochaguliwa kuwa wajumbe wa NEC-CCM kwa Tanzania bara.
Wanawake
1. Dkt Angelina S Mabula Kura 770
2. Dkt Ashatu Kijaji Kura 764
3. Christina Solomon Mndeme Kura 761
4. Hellen Makungu Kura 755
5. Fenela A. Mukangara Kura 747
6. Angellah J. Kairuki Kura 730
Wanaume
1. Mahenda Leonard 845
2. Bashungwa Innocent 720
3. Wasira Steven 680
4. Msome Jackson William 591
5. Kasheku Msukuma 587
6. Kasesela Richard 574
7. Wambura Chacha Mwita 545
8. Bashe Hussein 510
9. Nnauye Nape Mosses 508
10. Gwajima Josephat 497
11. January Makamba 452
12. Mwigulu Nchemba 450
13. Macha 435
14. Msengi Ibrahimu 428
Kimsingi washindi karibu wote wametoka kanda moja huku maeneo mengine wakirudi mikono mitupu na wagombea wao, wakiendelea kulaumiana kwamba wapiga kura wao wamekosa umoja lakini kikubwa nilichokiona ni mshikamano wa wajumbe toka kanda ya ziwa kuamua kuwabeba watu wao, lakini pia kikubwa wasukuma wameamua kushikamana na kuonyesha kwamba wao ni wengi nchi hii na kuamua watu wao waingie katika chombo cha maamuzi. Pamoja na kutumia nguvu ya pesa. Lakini umoja na mshikamano wao umeonyesha dhahiri wakidhamiria kitu wanaweza, Hivi sasa wanapongezana kwamba wamefanikiwa mission yao kwa 100%
Swali la kujiuliza ni nani aliye nyuma ya hii kadhia, Mimi na wewe hakuna anayejua, lakini kuanzia sasa hadi 2025 tutaona kila aina ya rangi.
Mikoa ya kanda ya kusini kwa maana ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe aliyepita ni Nape pekee. Tafsiri yake mikoa hiyo inabaki na wawakilishi wachache mno kwenye chombo hicho chenye mamlaka ya kupiga kura ya kumchagua Rais.
Mikoa ya Mbeya, Katavi, Rukwa, Iringa na Morogoro nadhani wameambulia patupu, wameondoka wakilaumiana.
Matokeo haya yanaashiria nini, mikoa ya kusini ndio ambayo imekuwa ngome kuu ya CCM, wamenyang"anywa rasmi ukuu huo, kwa kuwa hawana wawakilishi wengi. Kanda hiyo iliyoongoza kwa kutoa makada wakuu kama akina Nchimbi na wengineo sasa sio kitu tena.
Tutegemee nini?
Hawa wajumbe wa mkutano mkuu kwa matokeo haya tutegemee kwamba lolote linaweza kutokea 2025, kwa sababu wajumbe walio wengi ni ukanda ambao wamebezwa mno baada ya kifo cha mpendwa wao. Mikoa mingine kura walizonazo ni chache mno,hazitaweza kupingana na walio wengi kama tulivyoona.
Nini kifanyike
Kwa sasa anachoweza kufanya mwenyekiti ni kuhakikisha analichota kundi kubwa toka ukanda wenye wajumbe wengi ili kuvunja makundi, na kuhakikisha anapata uungwaji mkono mkubwa ili kujiweka katika mahali salama.
Hivi sasa maamuzi ya nani awe Rais yanategemea maamuzi ya kanda moja tu, kanda nyingine ni wasindikizaji tu. Maamuzi yanategemea mikoa michache yenye uwingi wa wajumbe.
Hii ni tafakuri fupi, itakayokusaidia kukuonyesha nguvu ya akina msukuma, Gwajima, Mabula, Bashiru ndani ya CCM.
Itoshe tu kusema kanda ya ziwa mmeupiga mwingi