Elections 2010 NEC yabadili matokeo ya Vunjo yasema ilikosea

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Tume ya uchaguzi NEC imebadilisha matokeo ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Vunjo baada ya kugundua ilitangaza matokeo tofauti na yale yaliyotangazwa awali na msimamizi wa uchaguzi.

Nec imetangaza matokeo mapya ya Jimbo la Vunjo yanayoonyesha kuwa mgombea wa TLP, Augustine Mrema alipata ushindi wa asilimia 54 na si 50 kama ilivyotangazwa awali.

Mabadiliko ya matokeo ni kama ifuatavyo kura za zamani kwenye mabano

Augustine Mrema TLP 30,810 (29,047)

Chrispin Meela CCM 17,498 (23,870),
John Mrema Chadema 6,558 (6,316)
Lyimo wa NLD kura 811 (118)

Pia idadi halisi ya wapigakura imebadilika kutoka 55,013 iliyotangazwa awali hadi kufikia 55,102 ya sasa huku idadi ya kura halali sasa ikiwa ni 53,914 tofauti na kura halali 53,705 zilizotangazwa awali.

Kutokana na hali hiyo, Mrema ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mazingira ya mabadiliko hayo ya kura, akisema kuwa anahisi kulikuwepo na njama za kuchakachua matokeo ambazo ziligonga mwamba.

My take: Kwa sababu kasoro za matokeo zinazidi kuongezeka, ili kuondoa manung'uniko kwa wananchi kuna haja ya kuundwa kwa tume huru kuchunguza uhalali wa matokeo. Serikali zinazoongoza huku wananchi wake wakinung'unika huwa hazifanikiwi na mara nyingi hukumbwa na mikosi mbalimbali kwenye utawala wake.
 
Tume ya uchaguzi NEC imebadilisha matokeo ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Vunjo baada ya kugundua ilitangaza matokeo tofauti na yale yaliyotangazwa awali na msimamizi wa uchaguzi.

Nec imetangaza matokeo mapya ya Jimbo la Vunjo yanayoonyesha kuwa mgombea wa TLP, Augustine Mrema alipata ushindi wa asilimia 54 na si 50 kama ilivyotangazwa awali.

Mabadiliko ya matokeo ni kama ifuatavyo kura za zamani kwenye mabano

Augustine Mrema TLP 30,810 (29,047)
Chrispin Meela CCM 23,870 (17,498),
John Mrema Chadema 6,558 (6,316)
Lyimo wa NLD kura 811 (118)

Pia idadi halisi ya wapigakura imebadilika kutoka 55,013 iliyotangazwa awali hadi kufikia 55,102 ya sasa huku idadi ya kura halali sasa ikiwa ni 53,914 tofauti na kura halali 53,705 zilizotangazwa awali.

Kutokana na hali hiyo, Mrema ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mazingira ya mabadiliko hayo ya kura, akisema kuwa anahisi kulikuwepo na njama za kuchakachua matokeo ambazo ziligonga mwamba.

My take: Kwa sababu kasoro za matokeo zinazidi kuongezeka, ili kuondoa manung'uniko kwa wananchi kuna haja ya kuundwa kwa tume huru kuchunguza uhalali wa matokeo. Serikali zinazoongoza huku wananchi wake wakinung'unika mara nyingi huwa hafanikiwi na hukumbwa na mikosi mbalimbali kwenye utawala wake.

Hizo kura jumla yake ni 62,049. Hivyo hata haya marekebisho hayako sahihi.
Kisheria, tume ikishatangaza matokeo inayoweza kutengua ni mahakama. Kwa hiyo sasa hivi tume kazi yake imemaliza. Waiache mahakama iendelee na kazi zake.

Swali: Je, ni nini kilikuwa chanzo cha tume kufanya marekebisha/masahihisho haya? kulikuwa na malalamiko au?
 
Nina imani kuwa kama Tume ya Uchaguzi ingekuwa inatumia moja kwa moja taarifa zilizotayarishwa na wasimamizi wa vituo vya kupigia kura na nakala yake kugawiwa mawakala, matatizo kama haya yasingeweza kutokea. Na hii ingepunguza sana hisia za uchakachuaji, kwani matokeo yaliyotolewa yangelingana na jumla ya matokeo kwa kurejea nakala za mawakala zinazowasilishwa kwenye vyama.Tatizo linaanza Tume ya Uchaguzi inapoanza kupitia taarifa za vituoni na kufanya kile inachoita marekebisho!!!

Hata hivyo kwa hiyo minimal gain aliyopata Mrema baada ya marekebisho, nampa hongera, na namuunga mkono maoni yake ya uchunguzi ni nini kilitokea. Ila nashauri badala ya kuitegemea TAKUKURU afungue kesi mahakamani, huko mambo yataeleweka!!!
 
Hizo kura jumla yake ni 62,049. Hivyo hata haya marekebisho hayako sahihi.
Kisheria, tume ikishatangaza matokeo inayoweza kutengua ni mahakama. Kwa hiyo sasa hivi tume kazi yake imemaliza. Waiache mahakama iendelee na kazi zake.

Swali: Je, ni nini kilikuwa chanzo cha tume kufanya marekebisha/masahihisho haya? kulikuwa na malalamiko au?
Sahihisho kidogo Meela wa CCM kura za sasa ni 17,498 badala ya 23,870 alizopewa awali ina maana ailkuwa ameongezewa kura 6,372 zaidi.

Lakini total bado inazidi idadi ya waliopiga kura ukijumlisha unapata kura 55,677 lakini wao wanasema kura halali ni 53,914 hii imekaaje, asante ZeMarcopolo kwa kunote hilo.
 
Dah kumbe ndo wanavyofanyaga ehe?..Hii imenifungua macho mazee!..This being the case all election results can not be trusted.
Kama wamechakachua sehemu ambazo kulikuwepo na gape kubwa kiasi what about those ares with smaller margins,uchakachuaji could be very simple to implement i suppose?
 
Inaonekana kuwa mbunge wa CCM ndugu Meela alikuwa ameongezewa kura zaidi ya elfu sita(6000) na msimamizi wa uchaguzi. hebu fikiria maeneo kama shinyanga mjini ambapo mgombea wa ccm ndg. masele ameshinda kwa kura moja ebu niambieni kwa hali hii ni wazi kuwa chadema ilishinda. Hakuna makosa kama NEC inavyotaka tuamini, huu ndio uchakachuaji. Nec has finally proven that, DR.Slaa has been telling the truth all along. Na bado hali hii itaendelea kila mahala na ukweli utajulikana kwani haki ya mtu aidhulumiwi.
 
Ngoja tumsubiri Slaa aanze kuchemsha watu.

Nina hamu sana kumuona Jaji Makame akipanda kizimbani kwa kudanganya kura.

Hata kama haiwezekani kutengua matokeo ya Urais, huyu jamaa hawezi kushitakiwa?

Watu wakishitakiwa na kuanza kula moto, wataanza kutengana.

Hakuna kitu poa kama DEVIDE and RULE. Kumtenga Makame na Kikwete ni muhimu sana.
 
2015 Watasema hata matokeo ya Urais yalikosewa

Moyo wangu wanitetemeka kwa hasira, na roho yangu yataka kupasuka! Aibu! Juzijuzi NEC imesema haiwezi kutengua matokeo ya Segerea hadi Mahakama. Je, NEC ndo mahakama, au inamahakama ndani ka ndani? NEC isivunjwe bali ipondweponde na kufanyiwa LANDSCAPING...aibu kwa Tanzania. NEC imejaa madudu mpaka haioni aibu!

Watoto wa chekechea (vidudu) wanaweza kujumlisha matokeo ya nchi nzima, NEC haiwezi, what a deadily shame?
 
And yet kuna watu humu huwa wanasema eti yaliyofanywa na NEC ni matatizo ya kawaida na yapo dunia nzima!!!!!!!!!! Huko Vunjo vp kura za uraisi???

But I said it earlier hata kabla ya uchaguzi, CCM na serikali yake they are not smart kwenye numbers when it comes to forgery! They will alwayz do their way/ ways na mwisho numbers don't sum up.
 
Bangi ni nzuri ikitumiwa kama dawa lakini ni mbaya ikitumiwa kama kiburudisho hasa kwa kuwagandamiza wenginee, nadhani NEC walipata kajimoshi kidogo
 
Kuna watu 6 nchini Kenya ambao mwanzoni mwa mwaka kesho watakuwa wamekwisha fikishwa mbele ya ile mahakama ya kimataifa (ICC) kutokana na vurugu zilizofuatia uvurugaji wa uchaguzi mkuu nchini humo. Nafahamu kuwa mahakama yetu haina ubavu wa kumshughulikia Makame na genge lake. Hivi ushahidi wa namna hii hautoshi kuwapeleka ICC, au mpaka watu wawe wamekufa!
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa ukidhamiria kuua, ni sawa na kuua. Ukidhamiria kuiba, ni sawa na kuiba. Mahakama inatakiwa kuprove beyond reasonable doubt kuwa ulitenda kosa. Hivyo,basi NEC watahesabikwa ni WAUAJI tu; hata kama wanajidai hawezi kupingwa eti katiba hairuhusu. Makosa ya aibu hayo, ICC inawasubiri hata wakifa, mifupa yao itapelekwa TheHeigh, .......

Wanajua wanachokifanya.....hatuhitaji kuwakumbusha kila wakati.....Huwezi kukaa unawaambia watu, MAKOSA YA KIBINADAMU wakati unajua hata jambazi ni binadamu, so what?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom