Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 297
Tume ya uchaguzi NEC imebadilisha matokeo ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Vunjo baada ya kugundua ilitangaza matokeo tofauti na yale yaliyotangazwa awali na msimamizi wa uchaguzi.
Nec imetangaza matokeo mapya ya Jimbo la Vunjo yanayoonyesha kuwa mgombea wa TLP, Augustine Mrema alipata ushindi wa asilimia 54 na si 50 kama ilivyotangazwa awali.
Mabadiliko ya matokeo ni kama ifuatavyo kura za zamani kwenye mabano
Augustine Mrema TLP 30,810 (29,047)
Chrispin Meela CCM 17,498 (23,870),
John Mrema Chadema 6,558 (6,316)
Lyimo wa NLD kura 811 (118)
Pia idadi halisi ya wapigakura imebadilika kutoka 55,013 iliyotangazwa awali hadi kufikia 55,102 ya sasa huku idadi ya kura halali sasa ikiwa ni 53,914 tofauti na kura halali 53,705 zilizotangazwa awali.
Kutokana na hali hiyo, Mrema ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mazingira ya mabadiliko hayo ya kura, akisema kuwa anahisi kulikuwepo na njama za kuchakachua matokeo ambazo ziligonga mwamba.
My take: Kwa sababu kasoro za matokeo zinazidi kuongezeka, ili kuondoa manung'uniko kwa wananchi kuna haja ya kuundwa kwa tume huru kuchunguza uhalali wa matokeo. Serikali zinazoongoza huku wananchi wake wakinung'unika huwa hazifanikiwi na mara nyingi hukumbwa na mikosi mbalimbali kwenye utawala wake.