Mathias Byabato
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,020
- 691
Akihojiwa na kituo cha redio Kagera Community Radio(KCR FM) leo asubuhi Ofisa elimu kwa umma kutoka Tume ya uchaguzi (NEC Bw Titus Mwanzalila amesema kigezo kilichotumika ni urejeshwaji wa fomu za wagombea Urais ambapo mgombea wa Urais kupitia CCM John Magufuli alirejesha fomu akiwa wa kwanza na Tundu Lissu alirejesha akiwa wa mwisho.
Ameongeza kuwa kwa ngazi za ubunge na udiwani wagombea walipangwa katika karatasi za kura kwa maelekezo ya Tume
Hata hivyo amesema hiyo si sababu ya mpiga kura kutompigia kura mgombea anayemtaka.
Katika hatua nyingine amesema tume imejipanga kikamilifu kuondoa changamoto katika mchakato huu wa uchaguzi.
Nikipata nafasi nitawawekea audio clip
mbarikiwe
Byabato
Bukoba.