Nebukadneza: Mbabe wa vita, muabudu sanamu aliyekula majani kama ng’ombe

Kabla ya mwaka 1947, hakukuwa na nchi ama sehemu yoyote pale Duniani ikiyoitwa Israel! Israel ilianza kuitwa mwaka 1947.

Ata Yesu kipindi yupo hakukuwa na sehemu ikiitwa Israel pale mashariki ya kati, ata kipindi Abraham yupo hakukuwa na sehemu ikiitwa Israel pale mashariki ya kati.
Hiyo sehemu inaitwa Israel Kipindi cha Yesu iliitwa jina gn?
 
Sasa najiuliza tu. Kama Waisrael hawa si wale, kwamba hawapo tena, hawa ambao Biblia imewaandika wote watarudi, ni akina nani? I don’t know.
Hapo Waisraeli wanaozungumziwa ni wale waliojuwa mateka Babiloni chini ya utawala ya Nebukadneza

Mungu aliwaahidi kuwa watarudi nchini kwao Israeli kwenda kuanza maisha mapya na kujenga upya Yerusalemu baada ya miaka 70 ya utekwani Babiloni
 
Sasa jamani mnapoona Israel anapigana vita na kuua watoto na wanawake, hakuanza leo, ilikuwa tangu miaka hiyo ya nyuma, ni vita ambayo walizoea kupigana, hakushangai kwenye Biblia, tunakuja kushangaa sasa hivi.
Tofauti na vita ya sasa kipindi kile walikuwa wanapigana chini ya kibali cha Mungu sasa hivi hawana baraka zake ni Shetani tu ndiye anayewapelekesha waue hadi watoto wasio na hatia
 
Alikubali Mungu gani mkuu? Maana Mungu wa Wayahudi wala sio Mungu unamuamini wewe Mkristo. Tazama njia zenu za kumfikia huyo Mungu mnavyotafautiana pakubwa.
Mungu ninayemuamini mimi Mkristu ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Mungu aliyegawanya bahari ya Shamu waisrael wakapita Mungu aliyenena kwa Kinywa cha Nabii Isaya kwamba fimbo ya chuma itainuka katika kabila la Yuda atakayetawala milele!
 
Kabla sijakuandikia stori ya huyu mwamba wa Babeli katika nchi ya Babiloni, ngoja nijaribu na mimi kujiuliza maswali kadhaa. Watu wanasema wale Waisrael wa zamani sio wa sasa hivi, hao wa zamani walikwenda wapi?

Wakati wa nyakati za mwisho tunaambiwa kwamba Waisrael wote duniani watarudi nchini kwao. Yaani woooote, hakutokuwa na Muisrael yeyote yule ambaye atabaki nchi nyingine. Na hii ndiyo sababu inayowafanya kuwapiga Waarabu na kuchukua sehemu ya nchi zao kwa kuwa wanajua mwisho wa siku wale wenzao zaidi ya milioni 16 lazima warudi nyumbani.

Sasa wakisharudi wote na kukosekana Muisrael mwingine nje ya taifa lao, hapo ndipo mataifa yote yatapigana na hawa majamaa. Watapigwa vibaya mno mpaka kukimbilia kwenye ule mlima aliopaa Yesu na kisha kushuka, na mwisho wa dunia ndivyo utakavyokuwa.

Sasa najiuliza tu. Kama Waisrael hawa si wale, kwamba hawapo tena, hawa ambao Biblia imewaandika wote watarudi, ni akina nani? I don’t know.

Okay! Tuje mdogo mdogo tusome mambo tupanue ubongo wetu. Unapowasikia Waisrael jua kwamba hilo taifa limekuwa likipigana vita tangu miaka ya zamani, tena zaidi ya nchi yoyote ile.

Ili Israel iwe sehemu salama ilikuwa ni lazima kupigana vita. Wamepigana vita zaidi ya elfu kumi, kuna walizoshinda na kuna walizopigwa vibaya. Hili taifa linapenda vita, yaani wakisikia watu wanataka kupigana nao, ndiyo kwanza wanafurahi.

Wamelelewa hivyo tangu kipindi cha akina Abraham. Wanapenda vita kuliko kula, yaani wakilala, wanawaza vita, wakiamka wanawaza vita. Na kubwa zaidi huwa vita vyao havichagui, wanaua wanawake na watoto, hawa hawachagui hata kidogo.

Ukisoma Biblia, zamani wafalme walikuwa wakiambiwa na mitume kwamba nendeni nchi fulani, pigeni nchi nzima, msiache mtu ama mmea wowote umesimama, hakikisha mnaua wanawake mpaka watoto. Na wakifika huko walikuwa wakiua nchi nzima, hata mtoto anayetambaa, walikuwa wanamdedisha. Yalikuwa ni maagizo kutoka juu.

Sasa jamani mnapoona Israel anapigana vita na kuua watoto na wanawake, hakuanza leo, ilikuwa tangu miaka hiyo ya nyuma, ni vita ambayo walizoea kupigana, hakushangai kwenye Biblia, tunakuja kushangaa sasa hivi.

Tuachane na hayo, kuna siku nitakuja na stori yao ndeeeefuuuuuu.

Tuje kwa huyu mwamba wa kuitwa Nebukadneza. Unapowazungumzia wafalme waliokuwa na nguvu kubwa, basi bila shaka hutoweza kulisahau jina la mwamba mmoja hivi wa kuitwa Nebukadneza.

Huyu jamaa alikuwa mtawala kipindi kile cha akina Daniel. Nenda kasome Daniel sura ya 1 mpaka ya 4, imemuelezea sana mfalme huyu kwa namna alivyokuwa na nguvu, Mungu alikuwa anamuonyesha mambo yajayo kwa kupitia ndoto, halafu Daniel ndiye akawa mtafsiri.

Tuje sasa. Huyu jamaa ametoka wapi?

Baba wa mfalme huyu aliitwa Nabopolaan. Huyu alikuwa mflame wa 65 wa nchi iitwayo Babiloni ambayo ilikuwa na mji wake uitwao Babeli. Sasa miaka hiyo mfalme huyu alikuwa kwenye mapigano makali ya Misri, kwa nini? Walikuwa wanagombania milki ya Ashuru, yaani kama leo hii Morocco na Algeria wasivyopatana kisa tu kuna maeneo Morocco anayatawala kimabavu na Algeria wakiamini hayo ni maeneo yao.

Sasa baba yake alipofariki dunia, Nebukadneza akaanza kutawala Babiloni na kuingia kwenye vita yake ya kwanza na Misri, vita hivyo vilikwenda kupiganiwa huko Eufrate katika utawala wa mwisho wa baba yake, hiyo ilikuwa ni mwaka 605 Kabla ya Kristo.

Wakati huo Misri ilikuwa na mfalme wao, Farao-Neto lakini alijikuta yeye na majeshi yake wakiangukia pua kwa kuchakazwa vibaya sana na Babiloni.

Hiyo vita haikupiganiwa Eufrate tu bali walihama na kwenda kupigania sehemu nyingine iitwayo Karkemishi katika mto Eufrate. Unaweza kusoma kitabu cha Yeremia 46:2.

Sasa hapa nakupa mambo mawili, historia kulingana na Biblia, halafu historia kulingana na vitabu vya darasani. Hapa inabidi nicheze kotekote ili muelewe vizuri.

Sasa kwa nini Babiloni iliamua kumpiga Misri? Kwanza hii ilikuwa ni adhabu ya Mungu, yaani aliona kulikuwa na maovu mengi sana Misri (Hawa jamaa wamepinda tangu zamani), akaamua kumpeleka Nebukadneza kwenda kupigana huko. Soma Yeremia kuanzia sura ya 46.

Lakini sababu ya pili ni kwamba Misri aliitaka miji ya Shamu na Palestina, kwa nini? Miji hiyo ilikuwa karibu na Babiloni na kwa sababu waliona majamaa wanaitawala dunia, basi ingekuwa kazi nyepesi sana kupambana nao kama tu wangeipata miji hiyo.

Sasa naye Babiloni hawakutaka kuona hilo linatokea. Wakapambana vilivyo mpaka kushinda vita hivyo. Wakati Nebukadneza anapambana kwenye vita ndipo akapokea taarifa kwamba mshua wake amekufa hivyo ilikuwa ni lazima kurudi nyumbani na kusimikwa kuwa mfalme.

Nebukadneza alikuwa mjanja sana. Yaani alikuwa akipambana na Wamisri ili wasichukue Palestina na Shamu lakini wakati huohuo alikuwa akipigana na watu wa mji huo ili awatawale.

Alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, na baada ya hapo, sasa akaamua kwenda huko Yuda ili kupigana na mfalme Yehoyakimu. Unaposema taifa la Yuda, inamaana ya Israel. Akaona hiyo haitoshi, akaufuata mji wa Siria (Syria) na kuupiga na miaka minne baadaye akarudi kupigana na Wamisri.

Hii ita hakushinda, na hata Wamisri hawakushinda. Sasa hilo likawapa viburi watu wengine na kuona mbona kama na sisi tunamuweza jamaa? Kwa nini tusmfuate na kumkung’uta?

Mtu wa kwanza kuwa kimbelembele na kuonyeshwa mfano alikuwa Yuda (Israel) alipoleta kukukakara zake, akapigwa vibaya mno na wakamteka mfalme Yehoyakini, halafu pale akampandikiza mfalme aliyemtaka yeye aliyeitwa Sedekia. Najua kwa Wakristo haya majina si mageni kwenu.

Miaka ilikwenda mbele, mataifa yalitaka kujitoa katika utawala wa Babeli lakini walishindwa kwa sababu majamaa walikuwa hatari wa vita.

Watu wakapitisha ndogondogo kwa mfalme wa Yuda, Sedekia na kumwambia mbona alijisahau mbaba? Kwa nini ulipe ushuru mkubwa kwa Babeli na wakati hata wewe unaweza kujinasua, alienda kupigana na Misri, ngoma droo, wewe unamshindwaje? Mpige umuondoe nchini kwako! Sedekia akaona poa, acha nimtwange, kuingia vitani tu, akapigwa yeye.

Mji wa Yerusalemu ukawa under attack, jamaa akaingia hekaluni, akachukua vyombo vya dhahabu vya humo ambavyo Wayuda walikuwa wakivitumia kwenye ibada zao (Hivi vyombo vilimletea shida sana mfalme Belshaza ambaye ni mtoto wa Nebukadneza). Akawateka watu, akamuua Sedekia, halafu nchi ya Yuda akaifanya kuwa mkoa na si nchi tena.

Sasa miongoni mwa mateka waliochukuliwa ndiyo walikuwepo akina Daniel, Shadraki na Abedenego

Sijui unapata picha hapo.

Yaani ukisoma Bible, halafu ukasoma na haya masomo ya darasani ya historia, unaanza kupata mambo mengi zaidi.

Itaendelea.
Unajitahi kuelezea vizuri. Naaamini baada ya hapo utasogea mbele zaidi ya Daniel 4 uende hadi Daniel 12.

Nikupe Nyongeza kidogo ili ubaki njia kuu.

1. Babilon ndio nchi ya Iraq kwa sasa.
2. Nebkadneza ndio aliuhurusuru/ Aliuteka Yuda na kuwachukua hao vijana -
3. Nebkadneza ndio alichukua vyombo vya hekalu.
4. Sababu ya kuuteka Yuda ni kibali toka kwa Mungu, yaani Yuda walifanya maasi na kuuwa watu wengi sana, ndio Mungu akampa maelekezo Nebakneza kuuteka huo mji ili kuponya watu wake. Kiufupi Nebkadneza alimpendeza Mungu kwenye utawala wake. Hadi alipokuja kumkosea Mungu hapo badae.
 
Jina la mfalme wa Babylonia ambaye alitawala katika karne ya 6 KK ni Nebukadneza.

Hilo jina Nebukadreza labda ni kutokana na kukosea matamshi tu
Siyo makosa ya kimatamshi ila huyo, nimetoka kusoma hapa Wikipedia anaelezwa kuwa alikuwa mfalme bora sana wa babeli katika karne ya 6 KK.

So nazani ni watu wawili tofauti 🤒😎
 
Hapo Waisraeli wanaozungumziwa ni wale waliojuwa mateka Babiloni chini ya utawala ya Nebukadneza

Mungu aliwaahidi kuwa watarudi nchini kwao Israeli kwenda kuanza maisha mapya na kujenga upya Yerusalemu baada ya miaka 70 ya utekwani Babiloni
Jamani eeeh kama aliwaahidi watarudi kwao lakini kipindi hicho Israel ilijulikana kama koo tu sio kwamba ilikuwa sehemu fulani inaitwa Israel, hakuna sehemu iliyokuwa inaitwa Israel na ndiyo maana ata Abraham hakuambiwa aende Israel ila Canaani akitoka Hulu yawakalidayo.

Jina Israel limekuja kuchomekwa kwenye version mpya hizi kama mnavyoambiwa leo kuwa Musa ni (Moses) wakati Wayahudi wenyewe wanaitwa (Moshe) sasa jiulizeni hizi pronounce zenu zimetoka wapi ilihali mnaambiwa manabii hawa ni wayahudi?
 
Ilikuwepo na mipaka ilikuwepo mjii wao mkuu uliitwa Yuda
 
Kabla sijakuandikia stori ya huyu mwamba wa Babeli katika nchi ya Babiloni, ngoja nijaribu na mimi kujiuliza maswali kadhaa. Watu wanasema wale Waisrael wa zamani sio wa sasa hivi, hao wa zamani walikwenda wapi?

Wakati wa nyakati za mwisho tunaambiwa kwamba Waisrael wote duniani watarudi nchini kwao. Yaani woooote, hakutokuwa na Muisrael yeyote yule ambaye atabaki nchi nyingine. Na hii ndiyo sababu inayowafanya kuwapiga Waarabu na kuchukua sehemu ya nchi zao kwa kuwa wanajua mwisho wa siku wale wenzao zaidi ya milioni 16 lazima warudi nyumbani.

Sasa wakisharudi wote na kukosekana Muisrael mwingine nje ya taifa lao, hapo ndipo mataifa yote yatapigana na hawa majamaa. Watapigwa vibaya mno mpaka kukimbilia kwenye ule mlima aliopaa Yesu na kisha kushuka, na mwisho wa dunia ndivyo utakavyokuwa.

Sasa najiuliza tu. Kama Waisrael hawa si wale, kwamba hawapo tena, hawa ambao Biblia imewaandika wote watarudi, ni akina nani? I don’t know.

Okay! Tuje mdogo mdogo tusome mambo tupanue ubongo wetu. Unapowasikia Waisrael jua kwamba hilo taifa limekuwa likipigana vita tangu miaka ya zamani, tena zaidi ya nchi yoyote ile.

Ili Israel iwe sehemu salama ilikuwa ni lazima kupigana vita. Wamepigana vita zaidi ya elfu kumi, kuna walizoshinda na kuna walizopigwa vibaya. Hili taifa linapenda vita, yaani wakisikia watu wanataka kupigana nao, ndiyo kwanza wanafurahi.

Wamelelewa hivyo tangu kipindi cha akina Abraham. Wanapenda vita kuliko kula, yaani wakilala, wanawaza vita, wakiamka wanawaza vita. Na kubwa zaidi huwa vita vyao havichagui, wanaua wanawake na watoto, hawa hawachagui hata kidogo.

Ukisoma Biblia, zamani wafalme walikuwa wakiambiwa na mitume kwamba nendeni nchi fulani, pigeni nchi nzima, msiache mtu ama mmea wowote umesimama, hakikisha mnaua wanawake mpaka watoto. Na wakifika huko walikuwa wakiua nchi nzima, hata mtoto anayetambaa, walikuwa wanamdedisha. Yalikuwa ni maagizo kutoka juu.

Sasa jamani mnapoona Israel anapigana vita na kuua watoto na wanawake, hakuanza leo, ilikuwa tangu miaka hiyo ya nyuma, ni vita ambayo walizoea kupigana, hakushangai kwenye Biblia, tunakuja kushangaa sasa hivi.

Tuachane na hayo, kuna siku nitakuja na stori yao ndeeeefuuuuuu.

Tuje kwa huyu mwamba wa kuitwa Nebukadneza. Unapowazungumzia wafalme waliokuwa na nguvu kubwa, basi bila shaka hutoweza kulisahau jina la mwamba mmoja hivi wa kuitwa Nebukadneza.

Huyu jamaa alikuwa mtawala kipindi kile cha akina Daniel. Nenda kasome Daniel sura ya 1 mpaka ya 4, imemuelezea sana mfalme huyu kwa namna alivyokuwa na nguvu, Mungu alikuwa anamuonyesha mambo yajayo kwa kupitia ndoto, halafu Daniel ndiye akawa mtafsiri.

Tuje sasa. Huyu jamaa ametoka wapi?

Baba wa mfalme huyu aliitwa Nabopolaan. Huyu alikuwa mflame wa 65 wa nchi iitwayo Babiloni ambayo ilikuwa na mji wake uitwao Babeli. Sasa miaka hiyo mfalme huyu alikuwa kwenye mapigano makali ya Misri, kwa nini? Walikuwa wanagombania milki ya Ashuru, yaani kama leo hii Morocco na Algeria wasivyopatana kisa tu kuna maeneo Morocco anayatawala kimabavu na Algeria wakiamini hayo ni maeneo yao.

Sasa baba yake alipofariki dunia, Nebukadneza akaanza kutawala Babiloni na kuingia kwenye vita yake ya kwanza na Misri, vita hivyo vilikwenda kupiganiwa huko Eufrate katika utawala wa mwisho wa baba yake, hiyo ilikuwa ni mwaka 605 Kabla ya Kristo.

Wakati huo Misri ilikuwa na mfalme wao, Farao-Neto lakini alijikuta yeye na majeshi yake wakiangukia pua kwa kuchakazwa vibaya sana na Babiloni.

Hiyo vita haikupiganiwa Eufrate tu bali walihama na kwenda kupigania sehemu nyingine iitwayo Karkemishi katika mto Eufrate. Unaweza kusoma kitabu cha Yeremia 46:2.

Sasa hapa nakupa mambo mawili, historia kulingana na Biblia, halafu historia kulingana na vitabu vya darasani. Hapa inabidi nicheze kotekote ili muelewe vizuri.

Sasa kwa nini Babiloni iliamua kumpiga Misri? Kwanza hii ilikuwa ni adhabu ya Mungu, yaani aliona kulikuwa na maovu mengi sana Misri (Hawa jamaa wamepinda tangu zamani), akaamua kumpeleka Nebukadneza kwenda kupigana huko. Soma Yeremia kuanzia sura ya 46.

Lakini sababu ya pili ni kwamba Misri aliitaka miji ya Shamu na Palestina, kwa nini? Miji hiyo ilikuwa karibu na Babiloni na kwa sababu waliona majamaa wanaitawala dunia, basi ingekuwa kazi nyepesi sana kupambana nao kama tu wangeipata miji hiyo.

Sasa naye Babiloni hawakutaka kuona hilo linatokea. Wakapambana vilivyo mpaka kushinda vita hivyo. Wakati Nebukadneza anapambana kwenye vita ndipo akapokea taarifa kwamba mshua wake amekufa hivyo ilikuwa ni lazima kurudi nyumbani na kusimikwa kuwa mfalme.

Nebukadneza alikuwa mjanja sana. Yaani alikuwa akipambana na Wamisri ili wasichukue Palestina na Shamu lakini wakati huohuo alikuwa akipigana na watu wa mji huo ili awatawale.

Alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, na baada ya hapo, sasa akaamua kwenda huko Yuda ili kupigana na mfalme Yehoyakimu. Unaposema taifa la Yuda, inamaana ya Israel. Akaona hiyo haitoshi, akaufuata mji wa Siria (Syria) na kuupiga na miaka minne baadaye akarudi kupigana na Wamisri.

Hii ita hakushinda, na hata Wamisri hawakushinda. Sasa hilo likawapa viburi watu wengine na kuona mbona kama na sisi tunamuweza jamaa? Kwa nini tusmfuate na kumkung’uta?

Mtu wa kwanza kuwa kimbelembele na kuonyeshwa mfano alikuwa Yuda (Israel) alipoleta kukukakara zake, akapigwa vibaya mno na wakamteka mfalme Yehoyakini, halafu pale akampandikiza mfalme aliyemtaka yeye aliyeitwa Sedekia. Najua kwa Wakristo haya majina si mageni kwenu.

Miaka ilikwenda mbele, mataifa yalitaka kujitoa katika utawala wa Babeli lakini walishindwa kwa sababu majamaa walikuwa hatari wa vita.

Watu wakapitisha ndogondogo kwa mfalme wa Yuda, Sedekia na kumwambia mbona alijisahau mbaba? Kwa nini ulipe ushuru mkubwa kwa Babeli na wakati hata wewe unaweza kujinasua, alienda kupigana na Misri, ngoma droo, wewe unamshindwaje? Mpige umuondoe nchini kwako! Sedekia akaona poa, acha nimtwange, kuingia vitani tu, akapigwa yeye.

Mji wa Yerusalemu ukawa under attack, jamaa akaingia hekaluni, akachukua vyombo vya dhahabu vya humo ambavyo Wayuda walikuwa wakivitumia kwenye ibada zao (Hivi vyombo vilimletea shida sana mfalme Belshaza ambaye ni mtoto wa Nebukadneza). Akawateka watu, akamuua Sedekia, halafu nchi ya Yuda akaifanya kuwa mkoa na si nchi tena.

Sasa miongoni mwa mateka waliochukuliwa ndiyo walikuwepo akina Daniel, Shadraki na Abedenego

Sijui unapata picha hapo.

Yaani ukisoma Bible, halafu ukasoma na haya masomo ya darasani ya historia, unaanza kupata mambo mengi zaidi.

Itaendelea.
Ukiendelea naomba uni-tag
 
Swala sio kutofautiana kwa sababu hata wakristo wenyewe wanatofautiana kumfikia Mungu... Mroma na Mpentekoste wanasali tofauti kabisa ila wote ni wakristo.

Wakristo wanaamini wayahudi ni bloodline ya mitume, na Yesu alikuwa myahudi. Sasa wewe unataka kulazimisha unachokiamini wewe na wakristo wakiamini.
Hivi miaka hiyo wahaya mlikuwepo?
 
Kijana usipotoshe, hakuna sehemu Mungu alipowaagiza Waisraeli kukata miti yote kwenye nchi ya adui wakati wa vita.
Ukisoma kumbukumbu la torati 20:19 Mungu anawakataza Waisraeli kukata miti wakati wa vita.
Ni vyema kuchuja maneno kwa umakini na kuzingatia ukweli pale unapotaka kumhusisha Mungu katika madai yoyote.
 
Jamani eeeh kama aliwaahidi watarudi kwao lakini kipindi hicho Israel ilijulikana kama koo tu sio kwamba ilikuwa sehemu fulani inaitwa Israel,

Jina Israel limekuja kuchomekwa kwenye version mpya hizi kama mnavyoambiwa leo kuwa Musa ni (Moses) wakati Wayahudi wenyewe wanaitwa (Moshe) sasa jiulizeni hizi pronounce zenu zimetoka wapi ilihali mnaambiwa manabii hawa ni wayahudi?
Jina la Israel limetokana na Yakobo kwahiyo kabla ya Yakobo hilo jina halikuwepo.
Waisraeli walipotoka utumwani Misri waliingia nchi ya Kanaani na kuanzisha Taifa la Israeli ambalo mipaka yake ilipangwa na Mungu mwenyewe, Kutoka 23:31
Kuhusu tofauti ya majina ya Mitume na Manabii, ni jambo la kawaida jina moja kutamkwa na kuandikwa tofauti kutoka lugha moja kwenda nyingine lakini maana inabaki vilevile.Mfano, John na Yohana, England na Uingereza.
Kama nchi ya Israel haijawahi kuwepo je Wafalme Daudi na Suleimani walitawala nchi gani.
 
Kuhusu kula majani ni lugha ya picha...
Kimsingi jamaa alikuwa anavuta bangi....ndio majani ya kondeni...
Usifikiri kila mtu hapa ni MPUMBAVU mwenzio.
Biblia imeweka wazi kuwa Nebukadneza alikula majani kama ng'ombe halafu wewe unakuja kutuletea stori za vijiweni hapa.
Jiheshimu.
 
Haidhuru si kitu
Bangi ndio iliyomsaidia kuwa na busara ya kuhifadhi vyombo alivyoteka toka hakalu la Sulaiman Salalah aleeii wasalaam..tofauti na alivyofanya mwanae....
Na majani hayohayo ya kondeni(bangi)ndio iliyompa kibri na hakutaka kutubu ndani ya mwaka mmoja baada ya ile ndoto.
Na kwa nyongeza ninajiheshimu sababu ki umri mie ni baba yako au mke wa mama yako...Asante na karibu.
 
Back
Top Bottom