Ndugu zangu wananichukia

Ndugu zangu wananichukia

Habari wana JF,

Mimi ni kijana wa kike mwenye umri kati ya miaka 25-30. Ninao ndugu zangu wawili ambao tangu nmekua na kujielewa nimekuwa nikiishi nao, ndugu hao ni mama yangu mzazi na dada yangu mkubwa. Mimi ni wa mwisho kuzaliwa lakini bahati mbaya nilipokuwa darasa la pili baba yangu alifariki na inasemekana baba yangu hakuwa na mtoto mwingine zaidi yangu, dada yangu yeye ana baba yake na yuko hai.

Kisa chenyewe ni kwamba hawa ndugu zangu wana maisha mazuri japokuwa dada yangu hakusoma sana kutokana na kutokuwa na akili za darasani lakini baba yake ni mtu mwenye uwezo hivyo alimpa mtaji na huwa anafanya biashara.Tangu baba yangu kufariki nilianza kupata ubaguzi kutoka kwa dada yangu huyu maana alikuwa akiletewa vitu na baba yake mimi hanigawii na tukiwa chumbani basi huniringishia,mimi nilivumilia na kuendelea na maisha.Mama yetu alikuwa akimkemea lakin hakuacha hiyo tabia,mimi nilisoma kwa bidii nikafaulu level zote hadi kufika chuo kikuu.

Baada ya kumaliza chuo na kupata kazi nilipata wazo la kutafuta mali zangu maana baba yangu hakuniachia kitu,kila tunachomiliki kama familia ni cha baba wa dada yangu hadi nyumba tunayoishi.Hivyo nikaamua kujenga kule aliko mama yangu maana mimi nafanya kazi mkoa tofauti na mama anapoishi,mara ya kwanza nikamtumia mil 3 ili anunue matofali 3000 ya block kwa ajili ya ujenzi, nikanunua na ramani kwa mkandarasi nikaituma ili ujenzi uanze.Baada ya mwezi nikaanza kluwa natuma pesa kila mwezi kwa ajili ya vifaa kama cement,mchanga,mawe na gharama za kulipa mafundi ili wajenge,nia yangu ilikua kujenga nusunusu kila mwezi hadi nimalize.

Sasa juzi baada ya kuwasiliana na mama na kuniambia nyumba imefika kwenye lenta niliamua kufanya ziara ya kushtukiza ili nikaione nyumba yangu,cha ajabu nilipofika eneo la tukio nikakuta hakuna nyumba wala msingi, hata miti ambayo niliwahi kutuma pesa ili inunuliwe ipandwe haikuwepo yaani kiwanja kilikuwa cheupe, niliishiwa nguvu na kulia kama nimefiwa, nilienda hadi kwa mama kumuuliza kilichojiri lakini hakuwa na jibu la kueleweka, mara amejnga sehemu nyingine na nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki, niliondoka siku hiyo hiyo kurudi ninakofanyia kazi lakini moyo wangu umeumia pasipo mfano,nimepigana sana kutafuta pesa zangu lakini ndugu zangu wananirudisha nyuma,

Kabla ya hapa pia nimewahi kumkopea huyu dada yangu pesa kwenye vyama kama mil 1 lakin aligoma kulipa nkadaiwa mimi, na pia wakati nasoma nlikua nafanya biashara ya nguo nachukua kariakoo natembeza kwenye hostel za chuo sasa kuna kipindi nikawa bize na research nikampa mama yangu mzigo wa nguo wa laki 8 aniwekee dukani kwake aziuze then ubize ukiisha nitaendelea na biashara lakini mzigo aliuza na pesa hakunipa akidai kuwa alikopesha na hakulipwa.

Nimeshindwa kuelewa hawa ndugu zangu kwanini wananifanyia hivyo wakati vitu vyao na mali zao mimi hawanipi na wananinyanyasia na nikitafuta vyangu wananidhulumu, kwa kweli naumia hata sijui cha kufanya.

ndio tofauti ya kusoma na kutosoma....vitabia vya ajabu kwa dada yako kunachangiwa na akili mbovu....sasa weweumesoma unajitambua cha muhimu fanya yako kwani ushaona kila kitu kimewekwa wazi sasa mambo ya kuwshirikisha yatakukost zaidi...hata mama yako kwa stage hiyo haaminiki kwa kuwa anamezwa na dada na baba wa dada yako yani mume wake mama yako...so fanya yako kabisaa wao waneachiwa mali wewe huna...yani achana nao
 
Nyakati ngumu kwenye maisha yetu...haziji kwa nia ya kutuadhibu bali huja kwa nia ya kutufunza jambo fulani muhimu....hayo wanayokutendea nduguzo ni moja ya masomo muhimu sana kwenye maisha jambo la msingi ni kumshukuru kwa kuweza kusimama mwenyewe kwenye maisha yako na kuhangaikia maisha yako....

Mwanadamu mwenye akili timamu hujifunza kutokana na makosa...huna sababu a kujilaumu wala kunungunika kwa wakati bali unatakiwa kufungua ukuras mpya kwenye maisha yako na kuufunga ukurasa wa zamani......

Maisha yetu ni mafupi hivyo hatupaswi kuishi kwa kusononeka na kukosa raha bali tunatakuwa kuyafurahia maisha kwa kadri ya uwezo wetu.......usiwatenge nduguzo kwani hata wao hawajui walitendalo na ipo siku watajutia kile wakutendeacho pindi maruhani wa chuki watakapo waacha huru.....

DONT TRUST NO ONE...DONT EVEN TRUST YOURSELF......
 
Pole sana, ila jaribu kuufatilia kama huyo mama
ni mama yako mzazi , asije kuwa mama wa kufikia
maana kwa namna unavyoelezea , napata mashaka na
uhalisia wake kama kweli ndiye mzazi wako aliyeingia
leba kwenda kukuzaa.

Kwani mtu mwenye degedege iliyopanda kichwani
pekee ndi anaweza kutoa jibu kama alilotoa "Mama yako"
nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki

Acha kabisa kuna wamama wamepinda , Kuna mmoja mdingi kafariki ye ananza kuuza nyumba za urithi na kula maisha na dogodogo badala ya kusomesha watoto.
 
Waafrika ukitaka kukosana nao ni vitu viwili:Muhusishe na mambo ya pesa kwa kimkabidhi au wanawake/wanaume wenu wawe na ukaribu usio na mipaka!

Isha jifunza sana hivi vitu viwili,vimekosanisha watu wengi sana
 
Undugu ndio nini? Piga chini hao wote, kata mawasiliano nao, acha kuwapa hela na concentrate katika kujenga maisha yako badala ya kukaa unaulilia undugu wa kulazimisha. Swala la nyumba ungebadili mipango yake na badala yake tafuta kiwanja karibu na unapofanyia kazi au unapoishi ili uweze kusimamia ujenzi kwa urahisi. Narudia tena, achana na undugu wa kulazimisha kama hutakiwi.
 
Mungu awabariki wote mlionishauri na kunipa moyo,,asanteni sana
Mtunzi mahiri almarhum shaaban Robert anamzungumzia hasidi anasema
Hasidi ale ngano kwa samli
Na vimanda vya mayai
Awe na taa za kandili
Fanusi na karabai
Atahusudu moshi wa koroboi
Unaotoka kwa masikini
Hasidi avae silk hariri
Na mérimeri
Awe na yakuti almasi na johari
Na dhahabu tele zimejaa vidoleni
Atahusudu shaba ilioko shingoni
Mwa masikini
Hasidi umuhusudu alie mtoa tumboni.
Huu ndo ujumbe wangu kwako dada.
 
Habari wana JF,

Mimi ni kijana wa kike mwenye umri kati ya miaka 25-30. Ninao ndugu zangu wawili ambao tangu nmekua na kujielewa nimekuwa nikiishi nao, ndugu hao ni mama yangu mzazi na dada yangu mkubwa. Mimi ni wa mwisho kuzaliwa lakini bahati mbaya nilipokuwa darasa la pili baba yangu alifariki na inasemekana baba yangu hakuwa na mtoto mwingine zaidi yangu, dada yangu yeye ana baba yake na yuko hai.

Kisa chenyewe ni kwamba hawa ndugu zangu wana maisha mazuri japokuwa dada yangu hakusoma sana kutokana na kutokuwa na akili za darasani lakini baba yake ni mtu mwenye uwezo hivyo alimpa mtaji na huwa anafanya biashara.Tangu baba yangu kufariki nilianza kupata ubaguzi kutoka kwa dada yangu huyu maana alikuwa akiletewa vitu na baba yake mimi hanigawii na tukiwa chumbani basi huniringishia,mimi nilivumilia na kuendelea na maisha.Mama yetu alikuwa akimkemea lakin hakuacha hiyo tabia,mimi nilisoma kwa bidii nikafaulu level zote hadi kufika chuo kikuu.

Baada ya kumaliza chuo na kupata kazi nilipata wazo la kutafuta mali zangu maana baba yangu hakuniachia kitu,kila tunachomiliki kama familia ni cha baba wa dada yangu hadi nyumba tunayoishi.Hivyo nikaamua kujenga kule aliko mama yangu maana mimi nafanya kazi mkoa tofauti na mama anapoishi,mara ya kwanza nikamtumia mil 3 ili anunue matofali 3000 ya block kwa ajili ya ujenzi, nikanunua na ramani kwa mkandarasi nikaituma ili ujenzi uanze.Baada ya mwezi nikaanza kluwa natuma pesa kila mwezi kwa ajili ya vifaa kama cement,mchanga,mawe na gharama za kulipa mafundi ili wajenge,nia yangu ilikua kujenga nusunusu kila mwezi hadi nimalize.

Sasa juzi baada ya kuwasiliana na mama na kuniambia nyumba imefika kwenye lenta niliamua kufanya ziara ya kushtukiza ili nikaione nyumba yangu,cha ajabu nilipofika eneo la tukio nikakuta hakuna nyumba wala msingi, hata miti ambayo niliwahi kutuma pesa ili inunuliwe ipandwe haikuwepo yaani kiwanja kilikuwa cheupe, niliishiwa nguvu na kulia kama nimefiwa, nilienda hadi kwa mama kumuuliza kilichojiri lakini hakuwa na jibu la kueleweka, mara amejnga sehemu nyingine na nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki, niliondoka siku hiyo hiyo kurudi ninakofanyia kazi lakini moyo wangu umeumia pasipo mfano,nimepigana sana kutafuta pesa zangu lakini ndugu zangu wananirudisha nyuma,

Kabla ya hapa pia nimewahi kumkopea huyu dada yangu pesa kwenye vyama kama mil 1 lakin aligoma kulipa nkadaiwa mimi, na pia wakati nasoma nlikua nafanya biashara ya nguo nachukua kariakoo natembeza kwenye hostel za chuo sasa kuna kipindi nikawa bize na research nikampa mama yangu mzigo wa nguo wa laki 8 aniwekee dukani kwake aziuze then ubize ukiisha nitaendelea na biashara lakini mzigo aliuza na pesa hakunipa akidai kuwa alikopesha na hakulipwa.

Nimeshindwa kuelewa hawa ndugu zangu kwanini wananifanyia hivyo wakati vitu vyao na mali zao mimi hawanipi na wananinyanyasia na nikitafuta vyangu wananidhulumu, kwa kweli naumia hata sijui cha kufanya.
UKWELI LAZIMA USEMWE UNAISHI NA WACHAWI,NA IKO SIKU WATAKUPOTEZA,JIWEKE MBALI NAO LAKINI MAMA NI MAMA USIMSAHAU KIHALI NA KIMALI.
 
mtu anapotea wakati wakwenda ila siyo wakurudi...ilitakiwa toka ulipomkopea mil 1 na hakulipa unampotezea mazima,lakini zaidi ni kuwa hata hawa wazazi wetu pia wanakuwa na ushetani ndani yake haswa inapotokea kuwa hana roho yakutamani mafanikio unaweza sema ni aina flani hivi ya uchawi...chakufanya kuanzia sasa nikufanya mambo yako bila hata kuwashirikisha au kuwaweka karibu.....hao wana undugu na shetani hakika nakuambia....fikiria kwa kutumia akili siyo moyo,utakufa maskini wakat MUNGU alikupa nafasi hiyo...
MKUU HAO NI WACHAWI HAKIKA,NA AKICHEZA WANAMUUA.UKUMBUKE ALINYANYASIKA NA MAMA ALIKUWEPO,VIGAGULA HIVYO AVIEPUKE
 
Dada usikate tamaa bado nafasi unayo! Histoshe kwa hayo mambo ni ya kawaida kwa wabongo washio uswahilini mahana wengi yanawatokea.
 
Huwezi mtenga mama ila ningekushauri nenda kauze hicho kiwanja itakupunguzia machungu tena nenda ukiwa huko happy kama walidhani utakonda wakonde wao ukifika hapo wachangamkie vizuri ila wasijue kusudi lako uza kajenge hukouliko dawa ya adui si kumchukia ni kuzidisha upendo kama ni binadamu dhamira itamsuta
 
A

SIMWACHE *****,ADUI HAPENDWAGI ANAEPUKWA SIKU MOJA OKOTA NYOKA UISHI NAE NDANI MKUU
 
Uliza vizuri pia kuhusu kiwanja wasije wakawa wameisha uza??
ulichokosea kuendelea kumuamini b mkubwa wakati alishakuliza.yeye kuwa n mama haina maana kuwa hana mapungufu na si kwamba hakupendi
 
Dah,nimewaza kwa kina saaana baada ya kumaliza kusoma huu uzi wako na comments za wadau wengine!nimeishia kushusha pumzi ndefu tu na kuisindikiza na glass ya maji baridi...pole bi dada,ndo majaribu ya maisha wengi wameshauri ya maana na yenye kujenga,fanyia kazi ushauri wao. Ahsante.
 
Elekeza nguvu zako kwenye kujipanga mwenyewe. Wasiopenda/taka maendeleo yako kua nao makini
 
Habari wana JF,

Mimi ni kijana wa kike mwenye umri kati ya miaka 25-30. Ninao ndugu zangu wawili ambao tangu nmekua na kujielewa nimekuwa nikiishi nao, ndugu hao ni mama yangu mzazi na dada yangu mkubwa. Mimi ni wa mwisho kuzaliwa lakini bahati mbaya nilipokuwa darasa la pili baba yangu alifariki na inasemekana baba yangu hakuwa na mtoto mwingine zaidi yangu, dada yangu yeye ana baba yake na yuko hai.

Kisa chenyewe ni kwamba hawa ndugu zangu wana maisha mazuri japokuwa dada yangu hakusoma sana kutokana na kutokuwa na akili za darasani lakini baba yake ni mtu mwenye uwezo hivyo alimpa mtaji na huwa anafanya biashara.Tangu baba yangu kufariki nilianza kupata ubaguzi kutoka kwa dada yangu huyu maana alikuwa akiletewa vitu na baba yake mimi hanigawii na tukiwa chumbani basi huniringishia,mimi nilivumilia na kuendelea na maisha.Mama yetu alikuwa akimkemea lakin hakuacha hiyo tabia,mimi nilisoma kwa bidii nikafaulu level zote hadi kufika chuo kikuu.

Baada ya kumaliza chuo na kupata kazi nilipata wazo la kutafuta mali zangu maana baba yangu hakuniachia kitu,kila tunachomiliki kama familia ni cha baba wa dada yangu hadi nyumba tunayoishi.Hivyo nikaamua kujenga kule aliko mama yangu maana mimi nafanya kazi mkoa tofauti na mama anapoishi,mara ya kwanza nikamtumia mil 3 ili anunue matofali 3000 ya block kwa ajili ya ujenzi, nikanunua na ramani kwa mkandarasi nikaituma ili ujenzi uanze.Baada ya mwezi nikaanza kluwa natuma pesa kila mwezi kwa ajili ya vifaa kama cement,mchanga,mawe na gharama za kulipa mafundi ili wajenge,nia yangu ilikua kujenga nusunusu kila mwezi hadi nimalize.

Sasa juzi baada ya kuwasiliana na mama na kuniambia nyumba imefika kwenye lenta niliamua kufanya ziara ya kushtukiza ili nikaione nyumba yangu,cha ajabu nilipofika eneo la tukio nikakuta hakuna nyumba wala msingi, hata miti ambayo niliwahi kutuma pesa ili inunuliwe ipandwe haikuwepo yaani kiwanja kilikuwa cheupe, niliishiwa nguvu na kulia kama nimefiwa, nilienda hadi kwa mama kumuuliza kilichojiri lakini hakuwa na jibu la kueleweka, mara amejnga sehemu nyingine na nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki, niliondoka siku hiyo hiyo kurudi ninakofanyia kazi lakini moyo wangu umeumia pasipo mfano,nimepigana sana kutafuta pesa zangu lakini ndugu zangu wananirudisha nyuma,

Kabla ya hapa pia nimewahi kumkopea huyu dada yangu pesa kwenye vyama kama mil 1 lakin aligoma kulipa nkadaiwa mimi, na pia wakati nasoma nlikua nafanya biashara ya nguo nachukua kariakoo natembeza kwenye hostel za chuo sasa kuna kipindi nikawa bize na research nikampa mama yangu mzigo wa nguo wa laki 8 aniwekee dukani kwake aziuze then ubize ukiisha nitaendelea na biashara lakini mzigo aliuza na pesa hakunipa akidai kuwa alikopesha na hakulipwa.

Nimeshindwa kuelewa hawa ndugu zangu kwanini wananifanyia hivyo wakati vitu vyao na mali zao mimi hawanipi na wananinyanyasia na nikitafuta vyangu wananidhulumu, kwa kweli naumia hata sijui cha kufanya.
Wakati naandika uzi huu nilikuwa na huzuni iliyochanganyika na akili kuruka,nilikuwa sijui pa kuanzia wala kumalizia,,ila asante kwa Mungu anaenitia ujasiri na nguvu hadi dakika hii,asanteni pia wana jukwaa wote mnaoendelea kunishauri na kunifanya niendelee kupata ahueni ya majeraha haya,Mungu akijalia nikikaa sawa kiakili nitaanza kujijenga tena upya kiuchumi, I hope cku moja nitaleta mrejesho wa mafanikio humu.MUNGU awabariki sana.
 
Back
Top Bottom