Ndugu zangu wananichukia

Ndugu zangu wananichukia

aisee pole sana miss jay story yako ikotofaut kdg na yng ila umekosea sana kiwanja umenunua lkn hakuwepo mby zaid swala la ujenzi ni swala nyeti sana hutakiwi kukabithi mtu pesa kbs usimazi ulitakiwa uwe wako na sio ndugu yako kbs pesa mwanaharam sana kilichopotea huwezi kueudisha rekebisha makosa yako jipange upya uwe na uchaga kdg kujua unafutilia kazi na kias cha pesa unachotoa kila la kheri
 
usjal dadaangu. kikubwa shukuru Mungu una kitu cha kukupatia kipato. hivyo fanya uanze 1, nunua kiwanja mbali na huko walipo mama na dada, jenga mdo mdo utatusua.
 
Ndugu zako hawakuchukii
ila hawana discipline na pesa
usiwakopeshe wala kuwashirikisha tena ishu za pesa
mama yako unaweza kuta pia sio timam sawasawa
ukimchukia unamuonea bure
 
Pole sana dada, Trust in God, jaribu kusimama wewe kama wewe sasa
 
mtu anapotea wakati wakwenda ila siyo wakurudi...ilitakiwa toka ulipomkopea mil 1 na hakulipa unampotezea mazima,lakini zaidi ni kuwa hata hawa wazazi wetu pia wanakuwa na ushetani ndani yake haswa inapotokea kuwa hana roho yakutamani mafanikio unaweza sema ni aina flani hivi ya uchawi...chakufanya kuanzia sasa nikufanya mambo yako bila hata kuwashirikisha au kuwaweka karibu.....hao wana undugu na shetani hakika nakuambia....fikiria kwa kutumia akili siyo moyo,utakufa maskini wakat MUNGU alikupa nafasi hiyo...
 
Kuna siku Yesu Mnazareti alimwambia "Ondoka kwangu shetani". Mtu mwenye kuzuia Malengo makubwa uliyojiwekea tena kwa makusudi huna jina la kumuita zaidi ya shetani.

Kwa kuwa umetambua ndugu zako (Mama & dada yako) hawapo upande wako ni vzr ukawaepuka. Huna namna zaidi ya kukubaliana na ukweli huu.

Mungu ni mwema mtumaini yeye ili akuinue na kukupa "Hekima & maarifa" ya kushinda vita ulivyonavyo.
 
Cha msingi. Piga moyo konde. Wasamehe. Jipange upya usirudie makosa tena. Simama mwenyewe kwa miguu yako mungu atakusaidia.
 
Habari wana JF,

Mimi ni kijana wa kike mwenye umri kati ya miaka 25-30.Ninao ndugu zangu wawili ambao tangu nmekua na kujielewa nimekuwa nikiishi nao, ndugu hao ni mama yangu mzazi na dada yangu mkubwa.Mimi ni wa mwisho kuzaliwa lakini bahati mbaya nilipokuwa darasa la pili baba yangu alifariki na inasemekana baba yangu hakuwa na mtoto mwingine zaidi yangu,dada yangu yeye ana baba yake na yuko hai.

Kisa chenyewe ni kwamba hawa ndugu zangu wana maisha mazuri japokuwa dada yangu hakusoma sana kutokana na kutokuwa na akili za darasani lakini baba yake ni mtu mwenye uwezo hivyo alimpa mtaji na huwa anafanya biashara.Tangu baba yangu kufariki nilianza kupata ubaguzi kutoka kwa dada yangu huyu maana alikuwa akiletewa vitu na baba yake mimi hanigawii na tukiwa chumbani basi huniringishia,mimi nilivumilia na kuendelea na maisha.Mama yetu alikuwa akimkemea lakin hakuacha hiyo tabia,mimi nilisoma kwa bidii nikafaulu level zote hadi kufika chuo kikuu.

Baada ya kumaliza chuo na kupata kazi nilipata wazo la kutafuta mali zangu maana baba yangu hakuniachia kitu,kila tunachomiliki kama familia ni cha baba wa dada yangu hadi nyumba tunayoishi.Hivyo nikaamua kujenga kule aliko mama yangu maana mimi nafanya kazi mkoa tofauti na mama anapoishi,mara ya kwanza nikamtumia mil 3 ili anunue matofali 3000 ya block kwa ajili ya ujenzi, nikanunua na ramani kwa mkandarasi nikaituma ili ujenzi uanze.Baada ya mwezi nikaanza kluwa natuma pesa kila mwezi kwa ajili ya vifaa kama cement,mchanga,mawe na gharama za kulipa mafundi ili wajenge,nia yangu ilikua kujenga nusunusu kila mwezi hadi nimalize.

Sasa juzi baada ya kuwasiliana na mama na kuniambia nyumba imefika kwenye lenta niliamua kufanya ziara ya kushtukiza ili nikaione nyumba yangu,cha ajabu nilipofika eneo la tukio nikakuta hakuna nyumba wala msingi, hata miti ambayo niliwahi kutuma pesa ili inunuliwe ipandwe haikuwepo yaani kiwanja kilikuwa cheupe, niliishiwa nguvu na kulia kama nimefiwa, nilienda hadi kwa mama kumuuliza kilichojiri lakini hakuwa na jibu la kueleweka, mara amejnga sehemu nyingine na nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki, niliondoka siku hiyo hiyo kurudi ninakofanyia kazi lakini moyo wangu umeumia pasipo mfano,nimepigana sana kutafuta pesa zangu lakini ndugu zangu wananirudisha nyuma,

Kabla ya hapa pia nimewahi kumkopea huyu dada yangu pesa kwenye vyama kama mil 1 lakin aligoma kulipa nkadaiwa mimi,na pia wakati nasoma nlikua nafanya biashara ya nguo nachukua kariakoo natembeza kwenye hostel za chuo sasa kuna kipindi nikawa bize na research nikampa mama yangu mzigo wa nguo wa laki 8 aniwekee dukani kwake aziuze then ubize ukiisha nitaendelea na biashara lakini mzigo aliuza na pesa hakunipa akidai kuwa alikopesha na hakulipwa.Nimeshindwa kuelewa hawa ndugu zangu kwanini wananifanyia hivyo wakati vitu vyao na mali zao mimi hawanipi na wananinyanyasia na nikitafuta vyangu wananidhulumu, kwa kweli naumia hata sijui cha kufanya.

Fanya yako na achana na watu wasiobebeka,kwanza walikunyanyasa afu unawabembeleza nini sasa?piga chini tafuta maisha yako na familia yako!
 
Acha ubwege ndugu zako hawana nia ya kusaidia zaidi ya kukuumiza fanya mambo yako kimya kimya
 
Wewe ni mtu mzima unalia lia na ndugu ya nini?
Duniani hapa anayekushika mkono ndio ndugu yako........
Chakufanya nunua kiwanja unapoishi....mbali nao kabisa (cha huko kiuze) anza ujenzi.

Mawasiliano nao yawe ni ya kawaida yasihusishe pesa....na ikitokea issue ya pesa ujue kusema "sina hela" unless iwe ni ugonjwa.
 
Pole sana bi dada. Umewajua rang zao, sasa amua kufanya mwenyewe! Mungu atakufungulia milango, na najua watakuja kukuomba msamaha siku moja & uwasamehe tu. Binadamu kwa sasa tumepoteza uaminifu & upendo, hata mnyama hawezi kumfanyia hivi mwanae wa kuzaa, no way. Imeniuma!
 
muda mwingine waweza waza hadi ukakufuru kwa maana kuna ndugu hawafadhiliki na pia hufikiri msaada wako ni jukumu lako kwao..watu kama hawa wanaoutumia undugu kama udhaifu wako ili wakufilisi sio wakuwachekea kila mara maana kwao ni fursa ila kwako ni maumivu.Fanya unachoweza kutoa kama msaada kwao ili uishi maisha yako maana ndugu ni wa muhimu lakini future yako INA umaana zaidi kwako na kizazi chako.
 
Peleleza hata jina lake na ukoo wake kama si wa nchi hii sazi mitandao inasaidia sana unaweza search jina hiko la ukoo ukapata mwanga!kikubwa pigania kutafuta majina yake tuu
 
Katika maisha, kila mtu ana nafasi ya kukuangusha mara moja. Kuangushwa mara mbili ni uzembe uliokithiri.

Ulifanya vyema kuanza kujikwamua na umaskini. Sasa umeshagundua kuwa mama hawezi kusimamia shughuli zako, jitegemee. Nunua kiwanja na uanze ujenzi mahali pengine. Weka pesa zako miezi kadhaa na uchukue likizo ya wiki moja tu full time site usimamie ujenzi. Hakuna anaekuchukia, ndio walivyo na tamaa ya pesa za kusquander. Usiwakasirikie wala kuwanunia, fanya yako bila kuwashirikisha.
 
Comment zenu zinanitia moyo na kunipa mwanga wa kipi cha kufanya,asanteni na Mungu awabariki
 
Back
Top Bottom