Ndugu zangu wananichukia

Ndugu zangu wananichukia

Nadhani unajua moja ya sifa za asset ni depreciation, nyumba ina sifa hiyo wakati ardhi alipoiweka inapanda thamani with time. Mtoa mada hajasema ni nyumba ya nini. Sijasoma biashara/uhasibu ila najua nyumba ni asset (non - current asset) ndo maana huwekwa dhamana akapata mkopo /mtaji.

Nyumba sio asset wala non-current asset. Non-current asset ni asset ambayo inatumika kusaidia uzalishaji wa kitu fulani kama vile mashine, gari n.k.
 
Kaunga naitaji msaada kwa ilo pliz
 
Last edited by a moderator:
Mmh huyo ni mama ako aliekubeba tumbon mwenyew?! au ulibambikwa kwake!? maana hainiingii akilin aisee!
 
Habari wana JF,

Mimi ni kijana wa kike mwenye umri kati ya miaka 25-30.Ninao ndugu zangu wawili ambao tangu nmekua na kujielewa nimekuwa nikiishi nao, ndugu hao ni mama yangu mzazi na dada yangu mkubwa.Mimi ni wa mwisho kuzaliwa lakini bahati mbaya nilipokuwa darasa la pili baba yangu alifariki na inasemekana baba yangu hakuwa na mtoto mwingine zaidi yangu,dada yangu yeye ana baba yake na yuko hai.

Kisa chenyewe ni kwamba hawa ndugu zangu wana maisha mazuri japokuwa dada yangu hakusoma sana kutokana na kutokuwa na akili za darasani lakini baba yake ni mtu mwenye uwezo hivyo alimpa mtaji na huwa anafanya biashara.Tangu baba yangu kufariki nilianza kupata ubaguzi kutoka kwa dada yangu huyu maana alikuwa akiletewa vitu na baba yake mimi hanigawii na tukiwa chumbani basi huniringishia,mimi nilivumilia na kuendelea na maisha.Mama yetu alikuwa akimkemea lakin hakuacha hiyo tabia,mimi nilisoma kwa bidii nikafaulu level zote hadi kufika chuo kikuu.

Baada ya kumaliza chuo na kupata kazi nilipata wazo la kutafuta mali zangu maana baba yangu hakuniachia kitu,kila tunachomiliki kama familia ni cha baba wa dada yangu hadi nyumba tunayoishi.Hivyo nikaamua kujenga kule aliko mama yangu maana mimi nafanya kazi mkoa tofauti na mama anapoishi,mara ya kwanza nikamtumia mil 3 ili anunue matofali 3000 ya block kwa ajili ya ujenzi, nikanunua na ramani kwa mkandarasi nikaituma ili ujenzi uanze.Baada ya mwezi nikaanza kluwa natuma pesa kila mwezi kwa ajili ya vifaa kama cement,mchanga,mawe na gharama za kulipa mafundi ili wajenge,nia yangu ilikua kujenga nusunusu kila mwezi hadi nimalize.

Sasa juzi baada ya kuwasiliana na mama na kuniambia nyumba imefika kwenye lenta niliamua kufanya ziara ya kushtukiza ili nikaione nyumba yangu,cha ajabu nilipofika eneo la tukio nikakuta hakuna nyumba wala msingi, hata miti ambayo niliwahi kutuma pesa ili inunuliwe ipandwe haikuwepo yaani kiwanja kilikuwa cheupe, niliishiwa nguvu na kulia kama nimefiwa, nilienda hadi kwa mama kumuuliza kilichojiri lakini hakuwa na jibu la kueleweka, mara amejnga sehemu nyingine na nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki, niliondoka siku hiyo hiyo kurudi ninakofanyia kazi lakini moyo wangu umeumia pasipo mfano,nimepigana sana kutafuta pesa zangu lakini ndugu zangu wananirudisha nyuma,

Kabla ya hapa pia nimewahi kumkopea huyu dada yangu pesa kwenye vyama kama mil 1 lakin aligoma kulipa nkadaiwa mimi,na pia wakati nasoma nlikua nafanya biashara ya nguo nachukua kariakoo natembeza kwenye hostel za chuo sasa kuna kipindi nikawa bize na research nikampa mama yangu mzigo wa nguo wa laki 8 aniwekee dukani kwake aziuze then ubize ukiisha nitaendelea na biashara lakini mzigo aliuza na pesa hakunipa akidai kuwa alikopesha na hakulipwa.Nimeshindwa kuelewa hawa ndugu zangu kwanini wananifanyia hivyo wakati vitu vyao na mali zao mimi hawanipi na wananinyanyasia na nikitafuta vyangu wananidhulumu, kwa kweli naumia hata sijui cha kufanya.

Pole sana, ila jaribu kuufatilia kama huyo mama
ni mama yako mzazi , asije kuwa mama wa kufikia
maana kwa namna unavyoelezea , napata mashaka na
uhalisia wake kama kweli ndiye mzazi wako aliyeingia
leba kwenda kukuzaa.

Kwani mtu mwenye degedege iliyopanda kichwani
pekee ndi anaweza kutoa jibu kama alilotoa "Mama yako"
nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki
 
Hasira nimepata mimi.....dah
Wasamehe lakini kamwe usisahau iwe kama funzo kwako. Wewe ni mtu mzima, tafuta kiwanja unapopataka wewe hata huko mkoani Ulipo , jenga taratibu kwa kusimamia mwenyewe. Inshaallah mwenyezi Mungu atakusimamia na kukuneemesha zaidi ya hapo
 
Mmh huyo ni mama ako aliekubeba tumbon mwenyew?! au ulibambikwa kwake!? maana hainiingii akilin aisee!

ni mama yangu mzazi,kama nilibambikwa pia siwezi kujua maana nimekua namuona yeye tu cjawahi muona mama mwingine
 
Pole sana, ila jaribu kuufatilia kama huyo mama
ni mama yako mzazi , asije kuwa mama wa kufikia
maana kwa namna unavyoelezea , napata mashaka na
uhalisia wake kama kweli ndiye mzazi wako aliyeingia
leba kwenda kukuzaa.

Kwani mtu mwenye degedege iliyopanda kichwani
pekee ndi anaweza kutoa jibu kama alilotoa "Mama yako"
nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki

nashindwa nifuatilie kwa nani kwa sababu ndugu wa baba yangu cwafahamu maana baba yangu hakuwa mtu wa nchi hii na ndugu wa mama huwa wananiambia huyu ni mama yangu
 
nisaidie babu kunibembelezea maana fighters wakikaa meza moja lazima kodi ya bandarini ionekane

Anza mdogomdogo kwankubembeleza PM. Then unijulishe ulipokwama kwa ajili ya msaada. Together we can.

Usimpoteze huyu mjasiriamali mpambanaji
 
we kweli kunguru unauliza nn sasa!! ulicho uliza kinaendana na mada???

---- kweli wewe si uache ajibu kwani wewe ndo Imetoa Mada bata nini shauri yako utaolewa
 
Pole Kwa kutopewa ushauri na wazee waliokuzidi umri hapo kazini...
Mie wazee niliowakuta kazini ambao wana umri wa kumzd baba yangu waliniambia maneno ya usiha mazuri na ambayo nilipoyapima nikajua kweli wananisaidia maana wao walisema wananamnia nisikosee kama wao..

Jenga kwanza nyumba yako mahali unapoishi na sio kwenu maana hutoishi kwenu ila utaishi palipo ofisi yako.

Wazazi saidia ukiweza ila wao si jukumu lako sana maana wao wanaishia ila ww una kizazi chako kinakuja na kitakushangaa kikikuta hujawaandalia mazingira mazuri kisa ulikuwa busy na wazazi wako. Huu ni ulimwengu wa everyman for himself, ila usiache kusaidia matatizo ya kwenu ambayo yana ulazima.

Usihangaike na magari,life style na anasa. Tafta kujiweka sawa kimaisha kwanza na hayo mambo utayakuta tuu maana yapo,yalikuepo na yatakuepo.

Mtumaini sana mungu na uheshimu kila mtu bila ubaguzi, usiwe mjuaji na nyenyekea sana hata wakikukosea.

Ukiwa na kwako ndio anza kusaidia na wengine kama uwezo unaruhusu na uweke akiba ya badae na kiendesha maisha ya familia yako.



*wanadamu tuna maudhi ila jifunze kupuuza mana hata ww unaudhi wengine pia
 
Achana na ndugu zako hao. una miaka mingapi? Mimi nina 32, nipo tayari kukuoa. unipate ndugu wa maana.
 
Yaliyopita si ndwele, sasa umeshajua ni ndugu wa aina gani wamekuzunguka hilo lenyewe tu ni jambo chanya.

Sasa kinachofuata ni wewe kufanya yale ambayo wewe kwa nafasi yako utaweza kuyasimamia.

Tumeumbwa tofauti sana mkuu hilo pia uishi ukilifahamu.
 
Pole sana dada angu!huo ndio ushindi wako!vumilia kwa mawazo uliyonayo saizi,kemea roho ya chuki itakayojitokeza kwa mama,lamsingi ni kuhesabu kuwa unaanza upya dada angu simama kama wewe pasipo kumchukia mama na nduguyo neno linasema shinda ubaya kwa wema
 
Miss Jay Wewe ni mtu mzima sasa jaribu kufanya maendeleo mwenyewe pia jenga mahali(mkoa) unapofanyia kazi hii itasaidia kusimamia wewe mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
nashindwa nifuatilie kwa nani kwa sababu ndugu wa baba yangu cwafahamu maana baba yangu hakuwa mtu wa nchi hii na ndugu wa mama huwa wananiambia huyu ni mama yangu

Jitahidi ufanye utafiti flani juu ya hicho nilichosema
kwani kama ni mama yako mzazi kungekuwa kuna
kitu flani cha kuwavuteni "pamoja". Kumbuka
the blood is much more thicker than water.
 
Pole sana miss jay hayo yote yametokea ili mtu asikulaumu tena, pamoja na kuchukua vyote hivyo, lakini hawajachukua akili yako, huyo aliyekuwezesha kupata hivyo bado yupo atakuwezesha kupata vingine usikatetamaa kabisa,sasa umemfahamu mama Yako na dada yako usiache kuwa penda sisi wakristo ktk warumi 12 :19 kisasi ni cha mungu
 
Back
Top Bottom