Ndugu zangu wananichukia

Ndugu zangu wananichukia

Miss Jay

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2013
Posts
211
Reaction score
174
Habari wana JF,

Mimi ni kijana wa kike mwenye umri kati ya miaka 25-30. Ninao ndugu zangu wawili ambao tangu nmekua na kujielewa nimekuwa nikiishi nao, ndugu hao ni mama yangu mzazi na dada yangu mkubwa. Mimi ni wa mwisho kuzaliwa lakini bahati mbaya nilipokuwa darasa la pili baba yangu alifariki na inasemekana baba yangu hakuwa na mtoto mwingine zaidi yangu, dada yangu yeye ana baba yake na yuko hai.

Kisa chenyewe ni kwamba hawa ndugu zangu wana maisha mazuri japokuwa dada yangu hakusoma sana kutokana na kutokuwa na akili za darasani lakini baba yake ni mtu mwenye uwezo hivyo alimpa mtaji na huwa anafanya biashara.Tangu baba yangu kufariki nilianza kupata ubaguzi kutoka kwa dada yangu huyu maana alikuwa akiletewa vitu na baba yake mimi hanigawii na tukiwa chumbani basi huniringishia,mimi nilivumilia na kuendelea na maisha.Mama yetu alikuwa akimkemea lakin hakuacha hiyo tabia,mimi nilisoma kwa bidii nikafaulu level zote hadi kufika chuo kikuu.

Baada ya kumaliza chuo na kupata kazi nilipata wazo la kutafuta mali zangu maana baba yangu hakuniachia kitu,kila tunachomiliki kama familia ni cha baba wa dada yangu hadi nyumba tunayoishi.Hivyo nikaamua kujenga kule aliko mama yangu maana mimi nafanya kazi mkoa tofauti na mama anapoishi,mara ya kwanza nikamtumia mil 3 ili anunue matofali 3000 ya block kwa ajili ya ujenzi, nikanunua na ramani kwa mkandarasi nikaituma ili ujenzi uanze.Baada ya mwezi nikaanza kluwa natuma pesa kila mwezi kwa ajili ya vifaa kama cement,mchanga,mawe na gharama za kulipa mafundi ili wajenge,nia yangu ilikua kujenga nusunusu kila mwezi hadi nimalize.

Sasa juzi baada ya kuwasiliana na mama na kuniambia nyumba imefika kwenye lenta niliamua kufanya ziara ya kushtukiza ili nikaione nyumba yangu,cha ajabu nilipofika eneo la tukio nikakuta hakuna nyumba wala msingi, hata miti ambayo niliwahi kutuma pesa ili inunuliwe ipandwe haikuwepo yaani kiwanja kilikuwa cheupe, niliishiwa nguvu na kulia kama nimefiwa, nilienda hadi kwa mama kumuuliza kilichojiri lakini hakuwa na jibu la kueleweka, mara amejnga sehemu nyingine na nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki, niliondoka siku hiyo hiyo kurudi ninakofanyia kazi lakini moyo wangu umeumia pasipo mfano,nimepigana sana kutafuta pesa zangu lakini ndugu zangu wananirudisha nyuma,

Kabla ya hapa pia nimewahi kumkopea huyu dada yangu pesa kwenye vyama kama mil 1 lakin aligoma kulipa nkadaiwa mimi, na pia wakati nasoma nlikua nafanya biashara ya nguo nachukua kariakoo natembeza kwenye hostel za chuo sasa kuna kipindi nikawa bize na research nikampa mama yangu mzigo wa nguo wa laki 8 aniwekee dukani kwake aziuze then ubize ukiisha nitaendelea na biashara lakini mzigo aliuza na pesa hakunipa akidai kuwa alikopesha na hakulipwa.

Nimeshindwa kuelewa hawa ndugu zangu kwanini wananifanyia hivyo wakati vitu vyao na mali zao mimi hawanipi na wananinyanyasia na nikitafuta vyangu wananidhulumu, kwa kweli naumia hata sijui cha kufanya.
 
Miss J !!
Pole, hiyo ni mitihani midogomidogo....!! Suali jee unapuma vizuri? (if yes) basi upo vizuri kbs.... its not the end of the world !! endelea na maisha...
 
Kuna jamaa mitaa ya kwetu alikua anaishi Uingereza alikua anatuma pesa wamjengee nyumba kumbe ndugu zake wanazitafuta wanamtumia picha nyumba ya jirani.Baada ya miaka kadhaa jamaa akarudi bila taarifa akakuta nyumba hakuna pesa imeliwa.Jamaa alivyoondoka hakurudi tena mpaka leo anaishi majuu
 
nimependa kiyu kimoja tu kwako..ufaiter!! yan nikimuona mdada ni fighter waaisha huwa nafarijika sana moyoni.
usijal hao ni nduguzo, jifunze sasa unaweza shirikiana na watu wengine sio lazima nduguzo....
look 4ward my sister na sio ya nyuma tena
 
Pole sana Miss Jay Mungu akutie nguvu na akupe uwezo wa kuwasamehe wote ili azidi kukufungulia baraka.

Imeshatokea Wacha ipitie kwasasa achana na mpango wa kujenga Kwenu zaidi jiimarishe wewe hapo ulipo,nunua Kiwanja sehemu ulipo Anza kujenga,jiimarishe zaidi kwa kutafuta vyanzo vingine vya pesa,mama kwa sasa achana naye msamehe tu kwa yote na usonge mbele kwa sasa focus zaidi kwenye mambo yako.
 
Last edited by a moderator:
Kuna jamaa mitaa ya kwetu alikua anaishi Uingereza alikua anatuma pesa wamjengee nyumba kumbe ndugu zake wanazitafuta wanamtumia picha nyumba ya jirani.Baada ya miaka kadhaa jamaa akarudi bila taarifa akakuta nyumba hakuna pesa imeliwa.Jamaa alivyoondoka hakurudi tena mpaka leo anaishi majuu

******&&&
aisee muda mwingine inakera kuona nduguzo hawathamin juhudi zako...ila cha msingi ni kuwa na netwok pana usiegemee kwa ndugu pekee
 
kwa wafanyakaz sio lazima ujenge kwenu jenga ukouko unakofanyia kazi kwani cku izi kambi popote
 
nimependa kiyu kimoja tu kwako..ufaiter!! yan nikimuona mdada ni fighter waaisha huwa nafarijika sana moyoni.
usijal hao ni nduguzo, jifunze sasa unaweza shirikiana na watu wengine sio lazima nduguzo....
look 4ward my sister na sio ya nyuma tena

Dogo changamka.... wife material hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harusi yako nakupa go ahead...
 
we learn through mistakes .. sasa umejifunza anza kujenga kwako na usimamie mwenyewe na ikiwezekana zaidi ya salamu kwa mama yako mzazi inatosha we kaa kimya fanya maisha yako la sivyo utakuwa wa kulalamika kila siku
 
Kuwa-address kama "ndugu", badala na mama na dada. + hiyo "kutokuwa na akili za darasani" pun kwa dada yako, na story nzima, I can only tell you this my sister. Let go of whatever it is you're holding in your heart. And you'll find peace of mind.
 
pole saana,maisha ni ELIMU endelevu yenye mitihani.....kama huo wako....kikubwa ni kujikita na mambo yako tu...ulijaribu kuwasaidia lakni hawako tayari kupokea msaada wako hivo....jitenge nao kabisa kwa mambo ya maendeleo.....udugu ubaki kama ilivyokawaida !!!!!!!maisha mema
 
Nikwambie kitu dada yangu? Hao unaoita ndugu zako sio tu wanakuchukia ila wanakuona ----, unasuluhisho moja tu la kufanya hapa, JITAMBUE UENDELEE NA MAISHA
 
Back
Top Bottom