afande kifimbo
JF-Expert Member
- Aug 31, 2015
- 6,303
- 2,779
Habari wana JF,
Mimi ni kijana wa kike mwenye umri kati ya miaka 25-30. Ninao ndugu zangu wawili ambao tangu nmekua na kujielewa nimekuwa nikiishi nao, ndugu hao ni mama yangu mzazi na dada yangu mkubwa. Mimi ni wa mwisho kuzaliwa lakini bahati mbaya nilipokuwa darasa la pili baba yangu alifariki na inasemekana baba yangu hakuwa na mtoto mwingine zaidi yangu, dada yangu yeye ana baba yake na yuko hai.
Kisa chenyewe ni kwamba hawa ndugu zangu wana maisha mazuri japokuwa dada yangu hakusoma sana kutokana na kutokuwa na akili za darasani lakini baba yake ni mtu mwenye uwezo hivyo alimpa mtaji na huwa anafanya biashara.Tangu baba yangu kufariki nilianza kupata ubaguzi kutoka kwa dada yangu huyu maana alikuwa akiletewa vitu na baba yake mimi hanigawii na tukiwa chumbani basi huniringishia,mimi nilivumilia na kuendelea na maisha.Mama yetu alikuwa akimkemea lakin hakuacha hiyo tabia,mimi nilisoma kwa bidii nikafaulu level zote hadi kufika chuo kikuu.
Baada ya kumaliza chuo na kupata kazi nilipata wazo la kutafuta mali zangu maana baba yangu hakuniachia kitu,kila tunachomiliki kama familia ni cha baba wa dada yangu hadi nyumba tunayoishi.Hivyo nikaamua kujenga kule aliko mama yangu maana mimi nafanya kazi mkoa tofauti na mama anapoishi,mara ya kwanza nikamtumia mil 3 ili anunue matofali 3000 ya block kwa ajili ya ujenzi, nikanunua na ramani kwa mkandarasi nikaituma ili ujenzi uanze.Baada ya mwezi nikaanza kluwa natuma pesa kila mwezi kwa ajili ya vifaa kama cement,mchanga,mawe na gharama za kulipa mafundi ili wajenge,nia yangu ilikua kujenga nusunusu kila mwezi hadi nimalize.
Sasa juzi baada ya kuwasiliana na mama na kuniambia nyumba imefika kwenye lenta niliamua kufanya ziara ya kushtukiza ili nikaione nyumba yangu,cha ajabu nilipofika eneo la tukio nikakuta hakuna nyumba wala msingi, hata miti ambayo niliwahi kutuma pesa ili inunuliwe ipandwe haikuwepo yaani kiwanja kilikuwa cheupe, niliishiwa nguvu na kulia kama nimefiwa, nilienda hadi kwa mama kumuuliza kilichojiri lakini hakuwa na jibu la kueleweka, mara amejnga sehemu nyingine na nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki, niliondoka siku hiyo hiyo kurudi ninakofanyia kazi lakini moyo wangu umeumia pasipo mfano,nimepigana sana kutafuta pesa zangu lakini ndugu zangu wananirudisha nyuma,
Kabla ya hapa pia nimewahi kumkopea huyu dada yangu pesa kwenye vyama kama mil 1 lakin aligoma kulipa nkadaiwa mimi, na pia wakati nasoma nlikua nafanya biashara ya nguo nachukua kariakoo natembeza kwenye hostel za chuo sasa kuna kipindi nikawa bize na research nikampa mama yangu mzigo wa nguo wa laki 8 aniwekee dukani kwake aziuze then ubize ukiisha nitaendelea na biashara lakini mzigo aliuza na pesa hakunipa akidai kuwa alikopesha na hakulipwa.
Nimeshindwa kuelewa hawa ndugu zangu kwanini wananifanyia hivyo wakati vitu vyao na mali zao mimi hawanipi na wananinyanyasia na nikitafuta vyangu wananidhulumu, kwa kweli naumia hata sijui cha kufanya.
Teh! Teh! Jamaa kaona Fursa ambayo wewe hujaionaToa ushauri jukwaani PM ya nini tena?
Pole sana, ila jaribu kuufatilia kama huyo mama
ni mama yako mzazi , asije kuwa mama wa kufikia
maana kwa namna unavyoelezea , napata mashaka na
uhalisia wake kama kweli ndiye mzazi wako aliyeingia
leba kwenda kukuzaa.
Kwani mtu mwenye degedege iliyopanda kichwani
pekee ndi anaweza kutoa jibu kama alilotoa "Mama yako"
nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki
Hah hah hah hah umenichekesha sana kwenye vyooote icho tu ndo ulipoguswa duuh hii.kiboko shikamooUmeolewa?
Mtunzi mahiri almarhum shaaban Robert anamzungumzia hasidi anasemaMungu awabariki wote mlionishauri na kunipa moyo,,asanteni sana
UKWELI LAZIMA USEMWE UNAISHI NA WACHAWI,NA IKO SIKU WATAKUPOTEZA,JIWEKE MBALI NAO LAKINI MAMA NI MAMA USIMSAHAU KIHALI NA KIMALI.Habari wana JF,
Mimi ni kijana wa kike mwenye umri kati ya miaka 25-30. Ninao ndugu zangu wawili ambao tangu nmekua na kujielewa nimekuwa nikiishi nao, ndugu hao ni mama yangu mzazi na dada yangu mkubwa. Mimi ni wa mwisho kuzaliwa lakini bahati mbaya nilipokuwa darasa la pili baba yangu alifariki na inasemekana baba yangu hakuwa na mtoto mwingine zaidi yangu, dada yangu yeye ana baba yake na yuko hai.
Kisa chenyewe ni kwamba hawa ndugu zangu wana maisha mazuri japokuwa dada yangu hakusoma sana kutokana na kutokuwa na akili za darasani lakini baba yake ni mtu mwenye uwezo hivyo alimpa mtaji na huwa anafanya biashara.Tangu baba yangu kufariki nilianza kupata ubaguzi kutoka kwa dada yangu huyu maana alikuwa akiletewa vitu na baba yake mimi hanigawii na tukiwa chumbani basi huniringishia,mimi nilivumilia na kuendelea na maisha.Mama yetu alikuwa akimkemea lakin hakuacha hiyo tabia,mimi nilisoma kwa bidii nikafaulu level zote hadi kufika chuo kikuu.
Baada ya kumaliza chuo na kupata kazi nilipata wazo la kutafuta mali zangu maana baba yangu hakuniachia kitu,kila tunachomiliki kama familia ni cha baba wa dada yangu hadi nyumba tunayoishi.Hivyo nikaamua kujenga kule aliko mama yangu maana mimi nafanya kazi mkoa tofauti na mama anapoishi,mara ya kwanza nikamtumia mil 3 ili anunue matofali 3000 ya block kwa ajili ya ujenzi, nikanunua na ramani kwa mkandarasi nikaituma ili ujenzi uanze.Baada ya mwezi nikaanza kluwa natuma pesa kila mwezi kwa ajili ya vifaa kama cement,mchanga,mawe na gharama za kulipa mafundi ili wajenge,nia yangu ilikua kujenga nusunusu kila mwezi hadi nimalize.
Sasa juzi baada ya kuwasiliana na mama na kuniambia nyumba imefika kwenye lenta niliamua kufanya ziara ya kushtukiza ili nikaione nyumba yangu,cha ajabu nilipofika eneo la tukio nikakuta hakuna nyumba wala msingi, hata miti ambayo niliwahi kutuma pesa ili inunuliwe ipandwe haikuwepo yaani kiwanja kilikuwa cheupe, niliishiwa nguvu na kulia kama nimefiwa, nilienda hadi kwa mama kumuuliza kilichojiri lakini hakuwa na jibu la kueleweka, mara amejnga sehemu nyingine na nilipomuambia anipeleke akasema amepasahau hapakumbuki, niliondoka siku hiyo hiyo kurudi ninakofanyia kazi lakini moyo wangu umeumia pasipo mfano,nimepigana sana kutafuta pesa zangu lakini ndugu zangu wananirudisha nyuma,
Kabla ya hapa pia nimewahi kumkopea huyu dada yangu pesa kwenye vyama kama mil 1 lakin aligoma kulipa nkadaiwa mimi, na pia wakati nasoma nlikua nafanya biashara ya nguo nachukua kariakoo natembeza kwenye hostel za chuo sasa kuna kipindi nikawa bize na research nikampa mama yangu mzigo wa nguo wa laki 8 aniwekee dukani kwake aziuze then ubize ukiisha nitaendelea na biashara lakini mzigo aliuza na pesa hakunipa akidai kuwa alikopesha na hakulipwa.
Nimeshindwa kuelewa hawa ndugu zangu kwanini wananifanyia hivyo wakati vitu vyao na mali zao mimi hawanipi na wananinyanyasia na nikitafuta vyangu wananidhulumu, kwa kweli naumia hata sijui cha kufanya.
MKUU HAO NI WACHAWI HAKIKA,NA AKICHEZA WANAMUUA.UKUMBUKE ALINYANYASIKA NA MAMA ALIKUWEPO,VIGAGULA HIVYO AVIEPUKEmtu anapotea wakati wakwenda ila siyo wakurudi...ilitakiwa toka ulipomkopea mil 1 na hakulipa unampotezea mazima,lakini zaidi ni kuwa hata hawa wazazi wetu pia wanakuwa na ushetani ndani yake haswa inapotokea kuwa hana roho yakutamani mafanikio unaweza sema ni aina flani hivi ya uchawi...chakufanya kuanzia sasa nikufanya mambo yako bila hata kuwashirikisha au kuwaweka karibu.....hao wana undugu na shetani hakika nakuambia....fikiria kwa kutumia akili siyo moyo,utakufa maskini wakat MUNGU alikupa nafasi hiyo...
MHam single
SIMWACHE *****,ADUI HAPENDWAGI ANAEPUKWA SIKU MOJA OKOTA NYOKA UISHI NAE NDANI MKUUHuwezi mtenga mama ila ningekushauri nenda kauze hicho kiwanja itakupunguzia machungu tena nenda ukiwa huko happy kama walidhani utakonda wakonde wao ukifika hapo wachangamkie vizuri ila wasijue kusudi lako uza kajenge hukouliko dawa ya adui si kumchukia ni kuzidisha upendo kama ni binadamu dhamira itamsuta
Wakati naandika uzi huu nilikuwa na huzuni iliyochanganyika na akili kuruka,nilikuwa sijui pa kuanzia wala kumalizia,,ila asante kwa Mungu anaenitia ujasiri na nguvu hadi dakika hii,asanteni pia wana jukwaa wote mnaoendelea kunishauri na kunifanya niendelee kupata ahueni ya majeraha haya,Mungu akijalia nikikaa sawa kiakili nitaanza kujijenga tena upya kiuchumi, I hope cku moja nitaleta mrejesho wa mafanikio humu.MUNGU awabariki sana.Habari wana JF,