Upande mwingine wa Baba

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,525
14,396
Baba hawezi kubeba mimba kwa muda wa miezi tisa, lakini daima ana mimba ya mahitaji ya familia, ndoto na maono ya maisha bora ya baadaye.
Huenda baba asijue jinsi uchungu wa kuzaa unavyo kuwa, lakini uchungu wake si wa kimwili, uchungu wake ni wa kihisia-moyo, naye anapata majeraha ya kiakili mara kwa mara.
Baba anaweza asiwe na matiti ya kunyonyesha watoto, lakini kila mtu ananyonya kutoka kwa matiti yake yasiyoonekana yaani akili yake kubwa ili kulisha familia!

Huenda baba asipatwe na vipindi vya kila mwezi, lakini hutokwa na damu ndani wakati anapokosa oabisa njia ya kupata kitu kwa ajili ya familia yake, anapolaumiwa kwa kutokuwa kama wanaume wenzake, na anapothaminiwa mara chache sana kwa ajili ya mapambano Yake ya kila siku na kujitahidi ili kuweka familia pamoja.
Mungu awatie nguvu wa Baba wote wanaopambana kwa ajili ya familia zao..
 
Back
Top Bottom