Ndugu zangu nisaidieni kazi, hali ni mbaya mno

Lacoste Mamba

Member
Jan 3, 2022
6
15
Habari za siku ndugu zangu pia poleni na majukumu ya ujenzi wa Taifa.....

Niende kwenye Mada binafsi mimi nikijana wakiume mwenye umri wa Miaka 26 ,pia nimuhitimu wa Chuo fulani Ngazi ya cheti katika fani ya Uongozi na usimamizi (public administration and management) mwaka 2018, Pia nina ujuzi wa na cheti pia cha Computer (Computer Applications).

Kilicho nileta kwenu ndugu zangu wakubwa kwa wadogo ni kutokana na changamoto ninazo pitia baada yakumaliza Elimu hiyo nakushindwa kujiendeleza kutokana na hali ya kiuchumi kwa wazazi kuwa mbaya, hivyo baada ya kuhitimu nilijishkiza kwenye vibarua vidogo vidogo vya hapa na pale lakini bado sikuweza kukidhi haja zangu au Mahitaji yangu ya kila siku kwakuwa hazikuwa kazi za kudumu pia ni kazi za msimu.

Kama mnavyojua hali ni mbaya mtaani nimejaribu hata kuomba nafasi mbalimbali zitolewazo zikiwemo utendaji wa vijiji, usimamizi wa kumbukumbu mahofisini lakini hali bado nimbaya kwa miaka yote hiyo..,Inafika mahali hata ndugu na wadogo zangu kufikia hatua ya kunidharau kwakuwa sina chochote chakufanya zaidi ya kula tuu nakuzunguka mtaani huku nikiwa sina ramani yeyote ya maana mtaani.

Hivyo ombi langu kwenu ndugu zangu wa JF najua huku kuna wajuzi mbalimbali hivyo naweza nikapata msaada wa kibarua chochote mkoa wowote ule nakuja hata kwa nauli yangu mradi kazi iwe ya halali na isiyo mchukiza Mungu angalau na Mimi mwaka huu 2022, nitoke hapa nyumbani.

NB. SICHAGUI KAZI HATA NIKIANZA NA KIWANGO KIDOGO CHA MSHAHARA SAWA TUU.., KIKUBWA NITOKE ENEO HILI NA NIWEZE KUJIPATIA KIPATO CHANGU.

MUNGU AWABARIKI SANA NDUGU ZANGU AHSANTENI MNO.
 
nakushauri hiyo hela ya nauli anzisha biashara yoyote ndogo na ufanye kwa bidii, mwanzo hua ni mgumu ila baada ya muda utazoea tu....
Ushauri mzuri saana mkuu umempa, lakini huwezi amini suala la biashara na uchuuzi kama halipo kwenye damu asee mtu anaweza kufa njaa na wakti anajua kuuza karanga, maji, pipi, mahindi ya kuchoma n.k yanaweza kumsaidia mtu ku survive.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom