Ndugu zangu CHADEMA, Kufumbatia Maji Kama Jiwe Ni Ujinga

Dear Comrades kwanza poleni sana kwa majukumu mazito na changamoto zilizopo mbele yetu, pia Tuendelee kumchangia Ndg yetu Tundu Lissu kwa chochote tunachobarikiwa na Mwenyezi Mungu pasi na kusahau Maombi na Dua zetu juu take.

Iko hivi, ukifuatilia kwa undani mawazo na matumaini ya wengi wetu ni kwamba HATUWEZI kushinda kiti cha urais katika uchaguzi ujao, ila wengi tunajifariji kwamba tutaongeza viti vya wawakilishi wetu pale Bungeni, na mpango-kazi ni kua tukishakua na wawakilishi wengi basi maamuzi mengi yatafanywa kutoka kwa wabunge wa upande wetu, HUU NI UPUUZI wa kiwango cha lami.

Binadamu tunatofautiana sana kwa mawazo na misimamo, Mimi binafsi siwezi kushiriki katika pambano au mtihani au kazi ambayo najua wazi kabisa kwamba SITOFAULU. Ukiangalia rekodi zilizopo utagundua kitu kimoja kwamba CCM inashinda si kwasababu inapendwa sana au inawafuasi wengi ila ni kwa MBINU CHAFU TU. Hata humu JF ukifuatilia vizuri wanaoitetea CCM Hata 50 hawafiki, wengi wanazidi kujiengua kutoka huko na asilimia kubwa waliobaki huko ni wanufaika wa mfumo.

Hatuwezi kushinda bila TUME HURU, na hatuwezi kupata Tume huru bila KATIBA MPYA ambayo Serikali iliyopo haiwezi kukubali ipatikane maana itakua ni sawa na kujichoma kisu. Tafsiri yake ni kwamba tutaendelea kubaki kuwa wapinzani labda mpaka kizazi chetu kiishe, na amini nawaambieni ndugu zangu kama 2020 kutakua na uchaguzi basibasi msishangae tubaki na majimbo matano(5) tu na tena tutayapata kwa mbinde sana.

Kila nikiwaza figisu figisu za uchaguzi uliopita ambao kwa maoni ya wengi ni uliongozwa na Mwanademokrasia Mzee wetu Jakaya sipati picha huu unaokuja utakuaje!!! Fikirieni watu kama akina Mdee, Bulaya, Lema na wengine wengine wapo bungeni kwa nguvu ya ziada siyo kwasababu TUME ilikua fair kwao achilia mbali wale waliopoteza viti vyao.

Sasa namna gani huu uongozi uliopo sasa? Ukimtazama mwenyekiti wao wa sasa na aina ya siasa anayoitaka nchini kwetu unaona kabisa kaburi letu halipo mbali. Kumbuka zile kauli zake kwamba MTU analipwa mshahara, posho, kodi, na gharama mbali mbali kutia ndani usafiri halafu anatangaza mpinzani kashinda, au nachukia wanasiasa huku akijitanabaisha kua yeye siyo mwanasiasa, unaona kabisa kua uchaguzi ujao afe beki afe kipa hakuna mpinzani kushinda.

Sasa ndiyo hapo ninapokumbuka kauli ya mhenga wa sikuzetu Mrisho Mpoto alipomwambia mjomba'ake kwamba "Kufumbatia maji kama jiwe ni ujinga". Kushiriki uchaguzi kwa mbinu zile zile huku tukijua matokeo yake ni UPUUZI wa ajabu sana. Sijui kamati kuu imejipangaje ila inahitaji AKILI na mbinu za hali ya juu sana kushinda uchaguzi ujao, kumbuka issue siyo HOJA za kuwapa wananchi, issue ni MBINU CHAFU, Hilo TU!!! Ni lazima tutengeneze mikakati madhubuti ya kupambana na hizo mbinu CHAFU ambazo na uhakika zitatumika kuliko uchaguzi wowote uliowahi kutokea Tanzania na hayumkini kuliko uchaguzi wowote utakao kuja kutokea!

" mwerevu huona dhoruba na kujificha, mpumbavu huendelea kwenda tu"(edited)
Mkuu umeeleweka sana tunaomba uongozi wetu wa chama kuliangalia hili jambo kwa uzito unao takiwa
 
Hapo ndipo tunafeli Mkuu, Mwenyekiti na Maliyamungu wanataka watawale daima-dumu... Kumbuka MAliyamungu anajua kuondoka kwa mwenyekiti ndiyo kuondoka kwake kitu ambacho hawezi kukubali.. Suala ni CCM inaondokaje??? Hilo ndilo la kuhangaikia.
Pamoja na hili jukumu ni la kimkakati hasa kwa uongozi lkn pia nasi wanachama na watanzania wapenda mabadiliko kujiandaa
 
Dear Comrades kwanza poleni sana kwa majukumu mazito na changamoto zilizopo mbele yetu, pia Tuendelee kumchangia Ndg yetu Tundu Lissu kwa chochote tunachobarikiwa na Mwenyezi Mungu pasi na kusahau Maombi na Dua zetu juu take.

Iko hivi, ukifuatilia kwa undani mawazo na matumaini ya wengi wetu ni kwamba HATUWEZI kushinda kiti cha urais katika uchaguzi ujao, ila wengi tunajifariji kwamba tutaongeza viti vya wawakilishi wetu pale Bungeni, na mpango-kazi ni kua tukishakua na wawakilishi wengi basi maamuzi mengi yatafanywa kutoka kwa wabunge wa upande wetu, HUU NI UPUUZI wa kiwango cha lami.

Binadamu tunatofautiana sana kwa mawazo na misimamo, Mimi binafsi siwezi kushiriki katika pambano au mtihani au kazi ambayo najua wazi kabisa kwamba SITOFAULU. Ukiangalia rekodi zilizopo utagundua kitu kimoja kwamba CCM inashinda si kwasababu inapendwa sana au inawafuasi wengi ila ni kwa MBINU CHAFU TU. Hata humu JF ukifuatilia vizuri wanaoitetea CCM Hata 50 hawafiki, wengi wanazidi kujiengua kutoka huko na asilimia kubwa waliobaki huko ni wanufaika wa mfumo.

Hatuwezi kushinda bila TUME HURU, na hatuwezi kupata Tume huru bila KATIBA MPYA ambayo Serikali iliyopo haiwezi kukubali ipatikane maana itakua ni sawa na kujichoma kisu. Tafsiri yake ni kwamba tutaendelea kubaki kuwa wapinzani labda mpaka kizazi chetu kiishe, na amini nawaambieni ndugu zangu kama 2020 kutakua na uchaguzi basibasi msishangae tubaki na majimbo matano(5) tu na tena tutayapata kwa mbinde sana.

Kila nikiwaza figisu figisu za uchaguzi uliopita ambao kwa maoni ya wengi ni uliongozwa na Mwanademokrasia Mzee wetu Jakaya sipati picha huu unaokuja utakuaje!!! Fikirieni watu kama akina Mdee, Bulaya, Lema na wengine wengine wapo bungeni kwa nguvu ya ziada siyo kwasababu TUME ilikua fair kwao achilia mbali wale waliopoteza viti vyao.

Sasa namna gani huu uongozi uliopo sasa? Ukimtazama mwenyekiti wao wa sasa na aina ya siasa anayoitaka nchini kwetu unaona kabisa kaburi letu halipo mbali. Kumbuka zile kauli zake kwamba MTU analipwa mshahara, posho, kodi, na gharama mbali mbali kutia ndani usafiri halafu anatangaza mpinzani kashinda, au nachukia wanasiasa huku akijitanabaisha kua yeye siyo mwanasiasa, unaona kabisa kua uchaguzi ujao afe beki afe kipa hakuna mpinzani kushinda.

Sasa ndiyo hapo ninapokumbuka kauli ya mhenga wa sikuzetu Mrisho Mpoto alipomwambia mjomba'ake kwamba "Kufumbatia maji kama jiwe ni ujinga". Kushiriki uchaguzi kwa mbinu zile zile huku tukijua matokeo yake ni UPUUZI wa ajabu sana. Sijui kamati kuu imejipangaje ila inahitaji AKILI na mbinu za hali ya juu sana kushinda uchaguzi ujao, kumbuka issue siyo HOJA za kuwapa wananchi, issue ni MBINU CHAFU, Hilo TU!!! Ni lazima tutengeneze mikakati madhubuti ya kupambana na hizo mbinu CHAFU ambazo na uhakika zitatumika kuliko uchaguzi wowote uliowahi kutokea Tanzania na hayumkini kuliko uchaguzi wowote utakao kuja kutokea!

" mwerevu huona dhoruba na kujificha, mpumbavu huendelea kwenda tu"(edited)

uliposema habari ya tume huru tu nimekuona una akili!!, uko sahihi sana

habari ya ukuta, sangara, kumtukana rais, sijui nini havina maana yeyote kama basics ambayo ni kuwa na tume huru haipo

matusi huwa hayawapati wenye hela na vyeo
 
Usiogope mkuu tutatoa nyoka pangoni hata kwa upanga.
Mh shehe mponda amesema tuikemee hii serikal hata kwa upanga.2020 huyu Mugabe wa bongo tunatoa nje

Swissme
Wahenga walisema na hawakukosea:
A barking dog seldom bites! Unfortunately, chadema never bites.
 
mleteni dereva wa lissu

mtoeni mbowe uenyekiti

stop kubadili gia angani.

ova.
 
uliposema habari ya tume huru tu nimekuona una akili!!, uko sahihi sana

habari ya ukuta, sangara, kumtukana rais, sijui nini havina maana yeyote kama basics ambayo ni kuwa na tume huru haipo

matusi huwa hayawapati wenye hela na vyeo
Yes, ifike mahali tuangalie maslahi ya nchi, uchama ndiyo unaangusha taifa letu.
 
Pamoja na hili jukumu ni la kimkakati hasa kwa uongozi lkn pia nasi wanachama na watanzania wapenda mabadiliko kujiandaa
Kabisa kabisa Mkuu, tatizo wengi wetu tuko nyuma ya keyboard tu.
 
Wewe unaota ndoto ccm inamiziz pandezote kama nikuomba micngo msaidiwe ombeni ila msiwadaganye watu eti ccm hapendwi inapendwa sana ngoma za watoto mtuzima hachezi na hazikeshi
 
Huna lolote wewe keyboard warrior .
Ulitaka niandikeje?! Kwamba democracy halisi (fair kwa wote) itapatikana kwa hisani ya ccm au kwa hisani ya Maghufuli?! No. Kuwa warrior ni pamoja na kuwa na mawazo huru!! Siyo kama wewe uliyejifungia na hautoi alternative. Kwa sababu democracy tunahitaji wote wapinzani na pro government. Ili kuifanya nchi yetu kuwa sehemu nzuri kwa binaadamu .

Lazima kuwe na pressure amani ya ndani au nje . Lakini yoote hayo yatategemea wanaoidai democracy watachukua mrengo gani!!
 
True, but HOW? Thats the question possed.

Swali liaipojibiwa kimkakati basi 'kufumbatia maji kama jiwe' kutaendelea na ndio upuuzi unaoongelewa na mleta mada.
They have guns we have better guns tunaisubiri 2020 ogopa people with nothing to loose.
 
Wewe unaota ndoto ccm inamiziz pandezote kama nikuomba micngo msaidiwe ombeni ila msiwadaganye watu eti ccm hapendwi inapendwa sana ngoma za watoto mtuzima hachezi na hazikeshi
Hebu wekeni tume huru tuone upendo unaozungumzia hapa Mkuu. Au siku Magu ahutubie Dar Lissu Mwanza tuone attention iatakua wapi.
 
Bado tuna safari ndefu sana km sisi ambao tunapaswa kusimama na kusimamia kile tunachokiamini bado tunawaza juu ya "MBINU CHAFU" za chama tawala nadhani 2020 bado tutapiga hatua 10 mbele na kurudi hatua 8 nyuma.

[HASHTAG]#FIKRAMGANDO[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom