Ndugu zangu CHADEMA, Kufumbatia Maji Kama Jiwe Ni Ujinga

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
11,141
20,787
Dear Comrades kwanza poleni sana kwa majukumu mazito na changamoto zilizopo mbele yetu, pia Tuendelee kumchangia Ndg yetu Tundu Lissu kwa chochote tunachobarikiwa na Mwenyezi Mungu pasi na kusahau Maombi na Dua zetu juu take.

Iko hivi, ukifuatilia kwa undani mawazo na matumaini ya wengi wetu ni kwamba HATUWEZI kushinda kiti cha urais katika uchaguzi ujao, ila wengi tunajifariji kwamba tutaongeza viti vya wawakilishi wetu pale Bungeni, na mpango-kazi ni kua tukishakua na wawakilishi wengi basi maamuzi mengi yatafanywa kutoka kwa wabunge wa upande wetu, HUU NI UPUUZI wa kiwango cha lami.

Binadamu tunatofautiana sana kwa mawazo na misimamo, Mimi binafsi siwezi kushiriki katika pambano au mtihani au kazi ambayo najua wazi kabisa kwamba SITOFAULU. Ukiangalia rekodi zilizopo utagundua kitu kimoja kwamba CCM inashinda si kwasababu inapendwa sana au inawafuasi wengi ila ni kwa MBINU CHAFU TU. Hata humu JF ukifuatilia vizuri wanaoitetea CCM Hata 50 hawafiki, wengi wanazidi kujiengua kutoka huko na asilimia kubwa waliobaki huko ni wanufaika wa mfumo.

Hatuwezi kushinda bila TUME HURU, na hatuwezi kupata Tume huru bila KATIBA MPYA ambayo Serikali iliyopo haiwezi kukubali ipatikane maana itakua ni sawa na kujichoma kisu. Tafsiri yake ni kwamba tutaendelea kubaki kuwa wapinzani labda mpaka kizazi chetu kiishe, na amini nawaambieni ndugu zangu kama 2020 kutakua na uchaguzi basibasi msishangae tubaki na majimbo matano(5) tu na tena tutayapata kwa mbinde sana.

Kila nikiwaza figisu figisu za uchaguzi uliopita ambao kwa maoni ya wengi ni uliongozwa na Mwanademokrasia Mzee wetu Jakaya sipati picha huu unaokuja utakuaje!!! Fikirieni watu kama akina Mdee, Bulaya, Lema na wengine wengine wapo bungeni kwa nguvu ya ziada siyo kwasababu TUME ilikua fair kwao achilia mbali wale waliopoteza viti vyao.

Sasa namna gani huu uongozi uliopo sasa? Ukimtazama mwenyekiti wao wa sasa na aina ya siasa anayoitaka nchini kwetu unaona kabisa kaburi letu halipo mbali. Kumbuka zile kauli zake kwamba MTU analipwa mshahara, posho, kodi, na gharama mbali mbali kutia ndani usafiri halafu anatangaza mpinzani kashinda, au nachukia wanasiasa huku akijitanabaisha kua yeye siyo mwanasiasa, unaona kabisa kua uchaguzi ujao afe beki afe kipa hakuna mpinzani kushinda.

Sasa ndiyo hapo ninapokumbuka kauli ya mhenga wa sikuzetu Mrisho Mpoto alipomwambia mjomba'ake kwamba "Kufumbatia maji kama jiwe ni ujinga". Kushiriki uchaguzi kwa mbinu zile zile huku tukijua matokeo yake ni UPUUZI wa ajabu sana. Sijui kamati kuu imejipangaje ila inahitaji AKILI na mbinu za hali ya juu sana kushinda uchaguzi ujao, kumbuka issue siyo HOJA za kuwapa wananchi, issue ni MBINU CHAFU, Hilo TU!!! Ni lazima tutengeneze mikakati madhubuti ya kupambana na hizo mbinu CHAFU ambazo na uhakika zitatumika kuliko uchaguzi wowote uliowahi kutokea Tanzania na hayumkini kuliko uchaguzi wowote utakao kuja kutokea!

" mwerevu huona dhoruba na kujificha, mpumbavu huendelea kwenda tu"(edited)
 
CCM itaondoka kivyovyote vile
Hapo ndipo tunafeli Mkuu, Mwenyekiti na Maliyamungu wanataka watawale daima-dumu... Kumbuka MAliyamungu anajua kuondoka kwa mwenyekiti ndiyo kuondoka kwake kitu ambacho hawezi kukubali.. Suala ni CCM inaondokaje??? Hilo ndilo la kuhangaikia.
 
Mkuu CCM mipango yao huwa wanapangia hapa??Ni ngumu kupangia mipango ya kuwaondoa hao madhalimu hapa jukwaani
 
Mkuu CCM mipango yao huwa wanapangia hapa??Ni ngumu kupangia mipango ya kuwaondoa hao madhalimu hapa jukwaani
Mkuu sijasema tupange humu mbinu, issue tuinvest katika mipango madhubuti, Mimi binafsi naamini 2010/2015 tulishinda kabisa ila tulizidiwa mbinu CHAFU, Mimi sio Mwanakamati sina pa kutolea mawazo yangu zaidi ya hapa ndiyo sababu nimeona tukumbushane mapema.
 
Nimekusoma mkuu hawa watu wameanza kufarakana wao kwa wao na hii hali hairudi nyuma na sisi tutachukulia point hapo
 
Hapo ndipo tunafeli Mkuu, Mwenyekiti na Maliyamungu wanataka watawale daima-dumu... Kumbuka MAliyamungu anajua kuondoka kwa mwenyekiti ndiyo kuondoka kwake kitu ambacho hawezi kukubali.. Suala ni CCM inaondokaje??? Hilo ndilo la kuhangaikia.
Mkuu huyu Maliyamungu ndio nan hahaaaa
 
Nimekusoma mkuu hawa watu wameanza kufarakana wao kwa wao na hii hali hairudi nyuma na sisi tutachukulia point hapo
Hawakuanza leo kufarakana. Wenzenu wana misimamo taabu yenu ninyi mnaanza kufarakana wakati ambao mnatakiwa kuwa wamoja. Ikifika July 2020 cdm itagawanyika kama 2015. Mark my words
 
Sawa mkuu kwa mtizamo wako

Lakini katiba hata ibadilishwe ni ndoto unayoyafikiria. Maana katiba iliyopo ni nzuri sana SEMA HAIFUATWI IPASAVYO ZAIDI YA TEUZI TU.

Kinachotakiwa nikuwa na katiba ktk VICHWANI MWETU 2020 NDIO INAAMUA ILA SI KWAHAWA WAKUBADILI GIA ANGANI AMA SAFARI wote hawa wameandaliwa na mfumo uliopo hataweza badili lolote zaidi ya kupiga dili ukabila ukanda na kudai waanzilishi wa chama.

Wengi wa wabunge wanatafuta umaarufu tu kwa mambo ambayo hayasaidii nchi wakubali wote kukatwa kodi kwenye vipato vyao na sio waongezwe posho.
 
Hapo ndipo tunafeli Mkuu, Mwenyekiti na Maliyamungu wanataka watawale daima-dumu... Kumbuka MAliyamungu anajua kuondoka kwa mwenyekiti ndiyo kuondoka kwake kitu ambacho hawezi kukubali.. Suala ni CCM inaondokaje??? Hilo ndilo la kuhangaikia.
Mgibeon na wapenda mabadiliko wote, haya mambo yana gharama sawa na kwenda peponi sharti ufe!! Na sisi WaTz tunapenda short cuts!! Wapi na wapi!!
Ukiangalia nchi za Africa magharibi(ECOEWAS), sasa hivi kidogo ziko sawa kidemocrasy, lakini ni baada ya vurugu nyingi, mapinduzi kadhaa na kuuana. Ndipo walipokubaliana kusonga mbele.
Lakini sisi, kama uhuru ulivyopatikana kwa maneno tunadhani na democracy itakuja kwa maneno Lah hasha!! Hii kitu lazima ipite mule mule, na Ndipo kizazi kijacho kitauona ufalme wa democracy!!

Kama mahakama zetu zingelikuwa independent, walau zingeliisaidia kuipokonya ccm ukiritimba, lakini uzoefu unaonyesha sivyo (ref.) Kesi za Mchungaji Mtikila ameshinda mara kadha lakini wahafidhina wanakata rufaa!! , Jaji Augustine kuchomoa kadi za ukereketwa kulikuonyesha nini?! , kuwa na kaimu jaji mpaka watu waridhike na utiifu wake!!

HAKUNA NAMNA NI KUPITA MULE MULE
 
Binafsi nasikia uchungu sana, yaani sisi tupo tupo tu! Kuna nafsi za watu zimepotea bure, kina Saanane na Mawazo hawa wote walikua wanatosha kabisa kutuamsha morali.
 
Hapo ndipo tunafeli Mkuu, Mwenyekiti na Maliyamungu wanataka watawale daima-dumu... Kumbuka MAliyamungu anajua kuondoka kwa mwenyekiti ndiyo kuondoka kwake kitu ambacho hawezi kukubali.. Suala ni CCM inaondokaje??? Hilo ndilo la kuhangaikia.
Akina mbowe wanatakiwa kutugawia kitu kama hiki Cha paddock watu tuingie mtaani?
nintchdbpict000357848215.jpg
 
Back
Top Bottom