Ndugu yangu anauza banda lake

Chinengu

Member
Jan 20, 2019
92
85
Salaam kwenu,husika kichwa cha habari hapo juu.

Kutokana na hari halisi ya maisha yanavyokwenda,nimeona niwashirikishe hili sana jf wenzangu wa Mtwara ili tu kupata msaada wenu.

Kuna ndugu yangu amemaliza saut mwaka juzi,bahati nzuri alipata mkopo,baada ya kujibana akaamua kununua kipande cha eneo na kujenga chumba ili tu kukwepa adha ya kupanga,pia aliweka banda kwa ajiri ya kufugia kuku,baada ya kumaliza chuo amebahatika kuolewa huko tandahimba,kama mjuavyo hakuna ajira hata hizi zilizotoka sasa zinaonekana zina ugumu Katika uombaji wake.

Ameamua auze banda lake ili apate mtaji ajiajiri,kwahyo kama kuna mtu wenye kuhitaji yupp tayari hata kama watalipana kwa awamu,eneo lipo barabarani,kuna bombs la maji pia.

Bei yake ni mil 4.5 tu,mwenye kuhitaji anaweza kupiga ili muelewane 0693 183 955
Shukran.
 
Kwa kitambo iki kuuza ni kutupa pia sio rafiki kw kuanzisha biashara mpya. Nionavyo mm!
Ni kweli kwa uuzaji huu ni sawa na kutupa lakini atafanyaje na hari hii,na vile waswahili husema kimfaacho mtu chake,huko bank hukopeshwi hadi uwe na biashara ilo simama hasa.
 
Ishu ni mda kaka. Kuna Mwana yupo mtwara kw uamisho wa kikazi. Alintaka nimkopeshe m5 afanye biashara korosho kwakua nilkua na deni lake la m3 nikamtupia 4 tu. Nikamnasihi usiwekeze kwa hela ndefu ww ni mgeni apo. Mwana katumbukiza km 10m ivi. Aysee kilichomkuta ! Namuonea aibu ata kumuliza yn. Je haikua biashara?
 
Eneo gani hicho kibanda kipo, mimi niko Mtwara maeneo ya viwandani karibu na nyumba ya NGOMA.
 
Ishu ni mda kaka. Kuna Mwana yupo mtwara kw uamisho wa kikazi. Alintaka nimkopeshe m5 afanye biashara korosho kwakua nilkua na deni lake la m3 nikamtupia 4 tu. Nikamnasihi usiwekeze kwa hela ndefu ww ni mgeni apo. Mwana katumbukiza km 10m ivi. Aysee kilichomkuta ! Namuonea aibu ata kumuliza yn. Je haikua biashara?
Ni kweli,kwa biashara ya korosho kiukweli ni bahati nasibu,ila huyu yeye anataka angalau afuge kuku wa mayai na kuwekeza kwenye kilimo cha muhogo Ila mtaji ndio hasa tatizo ndio maana kaamua hivyo
 
Aha kumbe Mbae, Kupita Msijute umesema eneo liko barabarani hebu nambie karibu na wapi barabara ya Mtwara -Dar
Kwa barabara ya mtwara-Dar,ukitokea magomen ukifika kituo kinaitwa pacha ya mbae ndio unashuka hapo na kuifata hiyo Barabara ya mbae
 
Salaam kwenu,husika kichwa cha habari hapo juu.
Kutokana na hari halisi ya maisha yanavyokwenda,nimeona niwashirikishe hili sana jf wenzangu wa Mtwara ili tu kupata msaada wenu.
Kuna ndugu yangu amemaliza saut mwaka juzi,bahati nzuri alipata mkopo,baada ya kujibana akaamua kununua kipande cha eneo na kujenga chumba ili tu kukwepa adha ya kupanga,pia aliweka banda kwa ajiri ya kufugia kuku,baada ya kumaliza chuo amebahatika kuolewa huko tandahimba,kama mjuavyo hakuna ajira hata hizi zilizotoka sasa zinaonekana zina ugumu Katika uombaji wake.
Ameamua auze banda lake ili apate mtaji ajiajiri,kwahyo kama kuna mtu wenye kuhitaji yupp tayari hata kama watalipana kwa awamu,eneo lipo barabarani,kuna bombs la maji pia.
Bei yake ni mil 4.5 tu,mwenye kuhitaji anaweza kupiga ili muelewane 0693 183 955
Shukran.

Makosa ya kujieleza vizuri unaweza kukosa msaada.
Sasa eneo liko barabarani, unauzaje? au mtu atanunuaje barabarani? Yaani makusudi ukanunue barabarani!! Au eneo lipo karibu na barabara? Fafanua vizuri ueleweke. Najuwa wapo watakaonipinga kuwa mbona inaeleweka; ila sijui kivipi, lakini ukweli upo dhahiri.

Niwape mfano hai katika makosa ya matangazo: Kuna kinyozi alikuwa amepanga kwenye frame ambayo ilikuwa kwenye gorofa. Aliweka tangazo rahisi tu kwenye frame yale, yaani KINYOZI. Kwa sababu ya ujuzi wake alikuwa na wateja wengi sana. Sasa, kwa bahati mbaya sana katu katika frame moja za chini kuna jamaa mwingine alipanga akaweka mgahawa. Sasa kiafya wateja wa jamaa wa mgahawa walimshauri amwombe kinyozi apange katika baadhi ya frame za pale chini kwani wakati mwingine nywele za wateja wake zilikwa zinapeperukia ndani ya mgahawa. Basi kinyozi aliposhauriwa hakupinga, aliomba kupanga katika frame frame ya chini ambayo kwa bahati nzuri ilikwa imeachwa na mteja ambaye alihamisha duka lake, ilikuwa frame ya tatu toka ulipo mgahawa.
Sasa, ili kuwajulisha wateja wake kuwa amehama kule juu na sasa yupo pale chini, akaweka tangazo lilisomeka kama ifuatavyo: TANGAZO - "YULE KINYOZI ALIYEKUWA ANANYOA JUU SASA ANANYOA CHINI". Hapo ikawa mwanzo wa kupoteza wateja. Jua kila mtu ana namna yake ya kutafsiri maandiko.
 
Kumbe tayari ameshaolewa? nipe namba yake nimcheki mi mwenyewe nipo Tandahimba mkuu.
 
Nimekuelewa,ila nilicho maanisha ni kwamba hilo eneo linafikika kwa urahisi nikiwa na maana kuwa hata kama una gari unafika nayo bila shida
 
Back
Top Bottom