dikteta2020
JF-Expert Member
- Aug 14, 2018
- 595
- 3,990
Hizi siasa za kuchafuana utu kwa mambo ya kipuuzi, kumshushia mwenzako hadhi ya ubinadamu wake na huku ukijua alikotokea ni jambo la kipuuzi na linapaswa kukemewa hadharani.
Hii inanifanya niamini kuwa hukumu za jana ndani ya mahakama ya Kisutu zilikusudiwa kupangwa kisiasa.
Watanzania tunajua kuwa Tundu Lissu hakupenda kwenda kuishi huko Ulaya ambapo mnasema ana uraia. Kilichompeleka huko ni gharama za siasa zetu mufilisi za kuwa tayari kuua pale mnapokuwa hamkubaliani kwa hoja. Hivyo ni lazima tuwe na hofu ya Mungu maana Karma ni kweli!
Kitendo cha Polepole kumpakazia Tundu Lissu ushoga hadharani kwa kweli hakikubaliki. Alienda Ulaya kutibiwa baada ya kuumizwa na wasiopenda ushindani wa kisiasa! Kusema hivyo ni kukosa hoja mbadala za ushindani wa kisiasa na kutapelekea matatizo zaidi.
Nakuona unaongea kwa ukali kuhusu kada wenu aliyeuawa huko Njombe, kama wewe ulivyoumia basi kila mmoja wetu linapomfika tatizo anapata kipimo hicho hicho cha maumivu. Lazima tuheshimu uhai wa kila mmoja wetu! Nchi hii siyo ya bata na kuku! Ni ya watu wenye miili sawa, na kila mmoja wetu linapomfika tatizo huumia kwa kiwango kile kile kilichokuumiza wewe! Tafadhali sana!
Mtaanza kuja na ujinga wa kudhalilisha utu wa watu kwakuwa tu mnataka madaraka. Hilo kamwe halikubaliki. Tufanye siasa za hoja zikitolewa tuhuma zijibiwe bila kudhalilishana kwa kiwango unachopanga kufanya. Hiyo ndiyo maana halisi ya siasa.
Polepole, unakoelekea siko!