Ndugu natafutiwa mke wa kuoa!

Ndugu natafutiwa mke wa kuoa!

mutahappy

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2012
Posts
529
Reaction score
188
Her ya pasaka !

Wakati nikiwa nimebakiza miez kadhaa kumaliza masomo ya degree huku nikiwa na umri wa miaka 28 kwa ujumla ndugu na jamaa zangu nimewapa jukumu la kunitaftia mwanamke wa kuoa na nimewatajia vigezo.

Mpaka sasa wapo wasichana 5 ambao wameishapatikana na wamenisubir nimalize masomo il nikachambue anae nifaa.

Katika karne hii kwel hil jambo likoje?
NB.
HII NI STORY NILIYOSIMULIWA NA RAFIK YANGU,
Sasa wakuu ni sawa kwa sasa kutaftiwa mwanamke na je madhara na faida zake ni zipi?
 
Inategemea wewe unaonaje. Sioni ubaya wake so long umetaka mwenyewe kutafutiwa.
 
makutano yapo ya aina nyingi hata hayo pia ni makutano baina ya wawili,
 
Karne hii bado kuna kutafutiana wake tu?
 
Kama mtaunda tume ya usaili naomba mnikumbuke tafadhali. Unijulishe masaburi allowance in advance.
 
Ndio uamuzi alioamua mwenyewe jamani. Ingekuwa amechaguliwa hao wanawake bila ridhaa yake hapo ndio ingekuwa ni tatizo.
kila mtu anastyl yake ya kutongoza nayeye kaamua kutongoza kwa style ya kutumia ndugu.
 
Ni nzuri zaidi kujitafutia mwenyewe ili ukija juta ujijutue au kama kujipongeza ujipongeze
 
Hii style huwa ipo sana sehemu za vijijini japo najua inaenda ikipungua kwa kasi sana kwa sasa. Maadamu anapewa sample za kutosha mfano kama alivyosema watano, then from there anahitajika mmoja anaweza kubahatisha aliye wake ama akakosa maana naye atakuwa na vigezo vyake alivyojiwekea na angependa japo vitimie kwa kiwango fulani.

Hii haina tofauti sana na wale wanaotafuta wachumba online, wanaokutana kwenye sherehe, kwenye usafiri, makazini nk, maana mwisho wa siku inabidi asimame kama yeye na kusema yaliyo moyoni mwake. Lakini kama ataishia kuchagua mmoja kati hao, then atake tena msaada wa kutongozewa, Duh hilo sasa tatizo, halikubaliki kwa sasa.
 
Mi naona hakuna ubaya wowote.Hiyo imekaa kama form 4 aliyepata zero-lazima akubaliane na hali pasi na kusingizia Mwl,Serikali,Mzazi au yeye mwenyewe kutokusoma.So at the end inabidi ukubali matokeo.Pia naomba usiwe unadanganya maana ni wewe mwenyewe then unatupia mpira kwa mwingine.
 
Back
Top Bottom