Ndugu Mtanzania: Je unajua hili?

MM Mwanakijiji,

Jibu unalo Mwanakijiji! Kujua kwetu ni kuamsha "Cheche" za fikra na siku moja kuchukua hatua-hata kama ikiwa kuchukua sheria mikononi kwetu. At worst, it will be on the record for the future generation-who can not forever be put down by the perpetrators.
 
kujua ni kuamka,
kujua ni kujiandaa na unakoenda,
kujua ni ujasiri
kujua ndio elimu,
na kujua ni kupanga..
kujua ni ushujaa na kujipanga.......
Acha woga ambao kwa kujua kwako na kutaka wengine wasijue ni Uchoyo...weka mambo hazarani, mengi yameshawekwa hapa na yamesaidia japo si moja kwa moja lakni tunmeona mshtuko serikalini.......nipo tayari kununu kodi kwa ajiri ya wabunge wote nizipeleke....

tukikaa kimya watatuona kwa sababu hatujui na hatuna uwezo wa kujua basi watafunika kombe, lakini wakijua kwamba tunajua na tunauwezo pia wa kujua hata ikibidi kurisk maisha ya ka-nzi, hawatatuchezea tena na watakuwa makini.

tufanye hivi kwa ajiri ya nchi yetu na maslahi ya vizazi vijavyo...

lete habari,tupe raha ya uchungu wa nchi yetu...tujue tunafanya nini 2010..
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tunajua sana. Tunajua hata mambo mengine ambayo wanadhania hatujui; tunajua hata yale ambayo wao wanasema ni ya 'siri' au yaliyopigwa mihuri ile myekundi ya "Siri Kubwa". Tunajua yanayofanywa nao maofisini na hata mitaani. Kimsingi, sasa hivi tuna taifa la wanaojua sana.

Kile kinachoitwa "utitiri" wa vyombo vya habari vimetufanya tuwe na uhuru wa kupata habari nyingi na kujua mambo mengi kiasi kwamba tumefika mahali hakuna kinachotushtua tena. Tumekuwa kama tuliopigwa ganzi ya aina fulani kiasi kwamba ili tusikie maumivu inahitajika jeraha kubwa kweli, lakini haya madogo madogo tunashtuka tuna makovu tu hatukumbuki lini tuliiumia na lini tulipona.

Vyombo hivi vya habari vimepita lengo la kutoa taarifa tu na vimekuwa pia vilele vya maoni huru na malumbano ya kijamii na kisiasa. Mengine haya maoni yoyote isipokuwa kutueleza nani kala nini, wapi na kalala na nani! Wenyewe tumeyakubali na kuyaweka kwenye kundi la Udaku.

Tunajua mipango yao mingi "ya maendeleo" kwani imeandikwa kwenye vitabu na nyaraka nyingi. Mipango hiyo ambayo imepewa majina matamu matamu na ya kukumbuka inaelezea kila kitu tunachotaka kujua kuhusu ujenzi wa taifa letu. Fikiria kuna MKUKUTA, MKURABITA, na miradi mingine ya kila aina kwenye wizara na idara mbalimbali. Wakati mwingine nafikiria kuna watu wameajiriwa kuja na hii "miradi".

Tunajua jinsi kashfa mbalimbali zimeligubika taifa letu na wahusika wake wakuu; na siyo tu kujua hivi hivi tunajua kama kwa kukariri. Huwezi kwa mfano kuzungumzia Richmond bila kuzungumzia Dowans; huwezi kuzungumzia Deep Green bila kuzungumzia Meremeta na huwezi kuzungumzia Meremeta bila kugusa Tangold; huwezi kuzungumzia EPA bila ya kugusa Kagoda kama vile usivyoweza kugusa CIS halafu ukaacha kuigusa Benki Kuu. Tunajua nini kimefanyika, wapi kimefanyika, na nani amefanya nini. Na hata pale tusipojua nani amefanya nini tunajua kabisa tukitaka kujua tunaweza!

Tunajua kuwa CCM haiwezi kushinda inavyoshinda hivi sasa kama kungekuwa na kanuni huru na zenye kuweka mazingira sawa ya kiushindani katika ulingo wa kisiasa. Tunajua kuwa hatuna ujanja wa kubadili mfumo huo na hivyo tunajjikuta tunaendelea kushiriki chaguzi zile zile chini ya kanuni zile zile tukitarajia matokeo tofauti. Hata mahali ambapo ni rahisi kushinda kama kusukuma gari mteremkoni tunashuhudi ugumu wa ajabu kiasi kwamba kumsukuma mlevi inakuwa mbinde!


Kwa kweli tunajua sana hadi wakati mwingine inaudhi. Kuna wakati naombea tusijue vitu fulani fulani kwani wakati mwingine kutokujua kunakuzuia usiumie au kujisikia hatia. Kuna vitu binafsi nisingependa kuvijua.

- Nisingependa kujua kuwa Rais wetu anajua kuwa asilimia 30 ya bajeti inaishia mifukoni mwa maafisa wa ngazi za juu!

- Nisingependa kujua kuwa Mwendesha Mashtaka wetu Mkuu anawajua walioiba kwa kupitia Kagoda na anajua kuwa walikuwa wametumwa lakini hawezi kuwachukulia hatua kwa sababu anajua akifanya hivyo atailetea matatizo serikali yake!

- Nisingependa kujua kuwa CCM iliahidi kutafuta suluhisho la mahakama ya kadhi lakini badala ya kufanya juhudi hizo miaka 20 iliyopita inajikuta inatuburuza taifa zima na kuleta mgawanyiko. Tungekuwa na mahakama hizo wakati huo nadhani sote tunajua kuwa kusingekuwa na tishio la baadhi ya viongozi wa Waislamu dhidi ya CCM!

- Nisingependa kujua kuwa viongozi wa kanisa ambao wametoa mwongozo wa kuchagua viongozi bora ndio hao hao wanakuwa wa kwanza kuwaalika viongozi wabovu kwenye shughuli zao za kufungua na kuzindua shughuli za kanisa! Laiti nisingejua jinsi gani walivyo wanafiki!

Kwa kweli kuna wakati mambo mengine nisingependa kujua kabisa. Baada ya ziara ya ka"nzi" Costa Rica na ile ziara ambayo nusura imvunje mbawa zake kule Upanga, amekuja na kunijulisha undani wa Meremeta undani ambao naamini kabisa na kwa kiasi kikubwa naelewa kwanini Pinda ameapa kutoligusa hilo.

Laiti nami nisingejua kile anachokijua Pinda na baadhi ya watu jeshini na serikalini (wabunge hawajui kwa hiyo heri yao!). Bahati mbaya sasa nakijua na kimenifanya nikubali kweli Meremeta ni suala la usalama wa Taifa! Ninaijua Meremeta kuliko habari zote zilioandikwa katika magazeti kuhusu kampuni hiyo na sasa kichwa kinaniuma kama ni bora nijue tu yaishe. Laiti wasingefanya hicho walichofanya kwa kupitia Meremeta labda wengine tusingejua.

Lakini swali linalonisumbua zaidi ni kuwa hivi tunajua ili kiwe nini? Ujuzi wetu wa mambo yanayohusu hali ya nchi yetu, siasa zetu, viongozi wetu unatusaidia vipi? Tunajua mambo haya yote na kupeana taarifa kila baada ya sekunde halafu nini kinafuata?

Je tunajua ili kuridhisha udadisi wetu ili na sisi tuwe miongoni mwa wajuao? Tunajua ili na sisi tuoneshe kuwa tunajua na si mbumbumbu? Tunajua haya yote na mengine mengi tunayoyapata kijiweni halafu yanatubadilisha sisi tuweje? Kama katika kujua kwako hujabadilika kwa namna yoyote sasa si bora kuishi bila ya kujua?

Hili la Meremeta kwa mfano hivi likishatoka na kuwekwa hadharani na kuanikwa juani kama mahindi ya kukobolewa ambayo harufu yake hupeperushwa kwenda mbali na upepo wenye vumbi na watu wakajua halafu kitakuwa nini? Kama wabunge waliamua kutokujua na Spika akakubali wasijue na Waziri Mkuu na Sumari wote wakihakikisha watu hawajui sasa sisi tukilifanya lijulikane tunafanya hivyo kwa faida gani?

Je si bora vingine waendelee kujua hao wachache na sisi wengine tuendelee kujua vile wanavyotaka tujue tu? Na hii ndiyo sababu nyingine ya kuweka mchango kidogo kwenye suala hili ili kuchuja wale wanaotaka kujua isije kuwa tukafanya kitu tukidhania tunafanya la maana kumbe tunaendeleza kupiga watu ganzi?

Je ni lazima watu wote wajue kila kitu au wakati mwingine ni bora wachache wajue kwa niaba ya wengi? Unajua hilo?

Ndio maana kuna rafiki yangu mmoja tulikuwa naye Chuo tunasoma wote aliwahi kuniambia kuwa Wamarekani wanafunzi asilimia kubwa huwa hawapendi kutazama Habari kwasababu huwa inaleta hasira hata mwili kuwa tress kubwa sana, Kujua mara nyingi inaleta shida sana na ndio hata vita hasira, chuki kubwa katika Jamii yetu
 
usiwe na wasiwasi tuko kwenye final touches of what I would refer as "a groundbreaking, jaw-dropping, earth-shaking exclusive report". Watakaotaka kujua watapewa namna ya kukipata. Don't worry.
Tunajua na tunapenda kujua zaidi na bahati ya wale waliopo mijini kubahatika kwa upataji wa habari kwa njia nyingi zaidi (ikiwemo internet kama JF) ila bado muamko wa kweli haujatutikisaa...

heri yao vijijini kuelewaa kwa haraka dhana na umuhimu wa uongozi mbadala kutokana na mahubiri ya mikutano ya upinzanii.

nawapongeza karatu, tarime, kigoma kaskazini, moshi mjini, mpanda mashariki,pemba na busanda, biharamulo na mbeya vijijini (nguvu ya kulazimisha asiyeshinda ashinde kutumika) wameonyesha njia.

dar kama kitovu cha taarifa na mapokeo ya taarifaa sijaelewaa tunahitaji nn ili kuamka vemaa na kuenda katika njia ya hawa wapenda mabadiliko wa maeneo niliyotaja hapo juu..
 
Bado wananchi walio wengi hawana ufahamu na uoza wa viongozi wetu. Itachukua muda wananchi hasa wa vijijini ambao ndio wengi kujua nini haki yao katika nchi hii na nini watawala wanapaswa kuwafanyia watu wao.

Sisi wachache wenye ufahamu tuendelee kusambaza tuyajuayo kwa wenzetu hata kama yanaumiza roho kama MMJ anavyosema lakini naamini juhudi hizi zitazaa matunda siku moja hata kama itachua miaka mingi. Tunachofanya ni kupigania vizazi vijavyo. Lazima tukumbuke maneno ya Hekima "You can fool some people for some time but you can not fool all the people all the time". Hivyo tuweke matumaini kuwa japo watu wengi bado hawajapata mwamko wa kuikomboa nchi yetu kutokana na ufinyu wa uelewa lakini siku zaja na zi karibu ambapo watu wetu wataamka kama walivyoamka kule Romania na kupigana kwa mikono dhidi ya vifaru vya Chausesco na ushindi wakaupata. Aluta continua

Mimi nakubaliana na PJ kuwa tuwavue nguo hadharani kwa kuweka wazi yale yote maovu waliotenda na umma wa watanzania ujue hizo siri za viongozi ni nini.Nijuavyo mimi kuna watu ambao hawana subira watachukua hatua mara moja .Kama ni kuandamana na kuishinikiza serikali ing'oke madarakani wapo tayari na watafanya hivyo.

Lakini kuna wale waendao kwa staili ya kuzomea viongozi mafisadi na hili limekuwa likiwanyima sana usingizi.Kwa mfano zaira za wabunge hivi karibuni kukagua madhara ya mgodi wa North Mara kuna maeneo walizomewa na hawakusimama kuendesha vikao,na hata kwenye yalemaeneo waliyoendesha vikao hawakua na confidence ya kujibu kwa ufasaha maswali ya wananchi.Hii kitu inafanya kazi wandugu.

Nashauri kuwa kile tunachokijua tuwafahamishe watanzania wenzetu tena wale wa vijijini ili kwa umoja tufanye jambo la maana kwa kusema IT IS ENOUGH WITH THIS RUBISH.

MJJ bila kuwajulisha wengi kile tunachofahamu hatutaweza kupata critical mass ya kuleta mageuzi Tanzania.Tuweke mambo hadharani na wajue tumejua ili watembee wakiwa uchi na wakijua kuwa watanzania wote tunajua kuwa wako uchi tena wa mnyama.

Je itakuwa ni aibu ilioje kwa viongozi ambao kwa sasa wanaviburi vilivyopindukia ambao hawataki tujue ubadhirifu walioufanya kuwa ndio chanzo cha utajiri wao uliokufuru wakijua tumejua wasichotaka tujue tena kwa idadi kubwa ya watu si aibu hiyo?
 
mzee Mwanakijiji sijui Tanzania tunakoipeleka ebu sasa tujaribu Chama kingine tuone mambo yatakuwaje.
Let us be risk takers
 
mzee Mwanakijiji sijui Tanzania tunakoipeleka ebu sasa tujaribu Chama kingine tuone mambo yatakuwaje.
Let us be risk takers

Audrey na MKJJ tafadhari msitupeleke huko. Kumbe ni ninyi?? Mimi nilifikiri ni mafisadi ndiyo wanatupeleka kubaya!!! Taratibu!!!

Anyway, hii artcle ya MMKJJ imenigusa. May be ni bora kutokujua kinachoendela kuliko kujua halafu huna uwezo wa kubadilisha mambo au kuwyafanyia kazi kama PG wetu!!!!!
 
Audrey na MKJJ tafadhari msitupeleke huko. Kumbe ni ninyi?? Mimi nilifikiri ni mafisadi ndiyo wanatupeleka kubaya!!! Taratibu!!!

Anyway, hii artcle ya MMKJJ imenigusa. May be ni bora kutokujua kinachoendela kuliko kujua halafu huna uwezo wa kubadilisha mambo au kuwyafanyia kazi kama PG wetu!!!!!

Hawahitaji kutupeleka huko... kudharau yale tuyajuayo, umbumbumbu au kutokujua kabisa kote kwaweza kutupeleka huko unakokuogopa. Hili Taifa letu kwa sasa jinsi lilivyo linajipeleka lenyewe!
 
Ninachokiona mimi kuna haja ya sisi tunaopata habari hizi kuwahamasisha wengine hasa wale ambao wanaamini kuwa siasa ni jambo baya wanasahau kuwa ndo inayoleta mustakabari wa nchi.

Hapa ndo penye kazi maana kama tutafanikiwa kuwahamasisha ndugu zetu basi hawa mafisidi lazima tutawashinda tu.

Kwani hamjasikia huko Malawi?mawaziri wote mafisadi hasa waliokuwepo kipindi cha Bakili Muluzu wako na hali mbaya maana wameanza kujaa rumande.

Wito wangu basi tukipata habari hakikisha walioko kwenye mailbox yako wanapata taarifa hiyo.hapo tutakuwa tunamultiply effect ya habari hizo zenye hamasa.
 
Baada ya kusoma post hii, nilikuwa naona, tungefungua Forum ya UFISADI. Hii ingewekwa kwa ajili ya kumbukumbu ya ufisadi mbalimbali uliokwisha fanyika na kwa waliohusika. Tatizo nililoliona, ni sisi wananchi tunakuwa busy sana katika kujihusisha na shughuli zetu binafsi, kiasi kwamba ufisadi unapoandikwa katika magazeti, ni rahisi kusoma na kusahau. Kama ingewekwa forum decicated to UFISADI, tungeweza kupitia kila siku na kujikumbusha ujinga unaondelea katika serikali yetu. Yani ingewekwa na ya quotation ovyo ovyo, ingekuwa fresh kabisa.
 
Ndio maana Watanzania wengi wana matatizo ya kutoshangazwa na mambo yanavyo endeshwa na serikali zao!

Kashfa zimekuwa nyingi kiasi ya kwamba zinaonekana kama ni jambo la kawaida tu miongoni mwa jamii... Makabwela hatushtuki tena...!

Nina wasi wasi itakapofikia wakati kashfa za viongozi wetu na hao tunaowaita mafisadi kutokuwepo tena wananchi wanaweza kuandamana... maana tushazowea ati kupuuzwa na kudhurumiwa.
Ni kweli tusije kushangaa ikatokea hivyo;siunajua tena mazoea hujenga tabia.
 
Thanks MKJJ, THE POST HAS MOTIVATED ME and 100% i would like to know what is albout kuhusu Meremeta na vikinda vyake, halafu vipi hatujapata Cheche kwa muda kidogo.

Halafu jamaa aliekeza jinsi ya kupata hiyo doc ya Meremeta, would you please assist on how i can find the bomb!
 
mimi nachoweza kusema ni kwamba sisi wenyewe vijana wa Kitanzania ndo tumeamua hawa jamaa i mean CCM waendelee kutubuluza, ukisoma ile hotuba ya Obama ailpokuwa Ghana aliongelea kuhusu nguvu kazi ya Vijana katika maendeleo ya bara la Afrika na aliipongeza sana Ghana kwa Vijana wamemonyesha Mwamko KATIKA KULETA MABADILIKO katika utawala wa nchi yao. mimi naamini kuwa pasipo vijana Kitanzania kuamka na kuingia kwenye siasa za Tanzania tutabaki kila siku kulalamika kwamba these guys are doing blunders, jamani twendeni tushiriki kaitka kuchagua Viongozi wetu, Tanzania Vijana ni zaidi ya asilimia 20, guys we can CHANGE the corrupted system na kuwa na Taifa lenye mwelekeo, lenye FURSA SAWA KWA WOTE na baadaye tukaenjoy matunda ya nchi yetu TAJIRI. Tusipokubali kuwa siasa ni sehemu ya MAMISHA YETU basi tutaendelea kulalamika tu, letts join the TASK FORCES za CHADEMA.

Mimi kama MTANZANIA kama watanzania wengine naona fursa niliyonayo ni kuhakikisha nashiriki 100% kwenye Siasa na kufanya hivo nilipokuwa Tanzania nilikuwa kwenye tASK FORCE kuhakikisha CHADEMA tunapata MAJIMBO YOTE YA GEITA.

NAWAOMBENI JAMANI TUSHIRIKI KWENYE SIASA, na tuifanye siasa kama shughuli zetu tunazofanya kutingizia viapato vyetu. Tuatafanikiwa tu.


Zidumu Fikra za Kimapinduzi.
 
mbona katika haya hujataja Mwananchi Gold? au umesamehe?

kama mnakumbuka Waziri Mkuu alisema suala la Meremeta haliwezi kujadiliwa hadharani. Sisi (Cheche) tumeamua kuliweka hadharani. Sasa hapa tunapima kwanza legal ramifications za kitendo chetu hicho ambacho kimsingi kinaendana na dhana muhimu katika nchi ya kidemokrasia yaani public intergrity.

Kwa vyovyote vile ilivyo by the end of next week.. kila kitu kitakuwa kimekamilika; yaani, njia ya malipo, delivery, conditions za mtu kupatia (siyo kwa sababu mtu amelipa tumehamisha haki zetu kwake)n.k Na kubwa zaidi ni la kuhakikisha kuwa kutokana na kazi ngumu timu yetu imefanya ili kulijulisha taifa "uozo wa hatari" wa siri hii watu wengine wasije kuanza kuchapa na kusambaza kana kwamba ni za kwao. Hivyo.. hii report kama zile mbili za nyuma (On Tanzania's Role's in Arms Trafficking and Open Letter to the British Gvt that was partly read in the House of Commons) zitakuwa zinalindwa na Haki Miliki.

Sisi wenyewe tuko matumbo joto... pressure inapanda, pressure inashuka.. kijasho chatiririka..
 
Baada ya kusoma post hii, nilikuwa naona, tungefungua Forum ya UFISADI. Hii ingewekwa kwa ajili ya kumbukumbu ya ufisadi mbalimbali uliokwisha fanyika na kwa waliohusika. Tatizo nililoliona, ni sisi wananchi tunakuwa busy sana katika kujihusisha na shughuli zetu binafsi, kiasi kwamba ufisadi unapoandikwa katika magazeti, ni rahisi kusoma na kusahau. Kama ingewekwa forum decicated to UFISADI, tungeweza kupitia kila siku na kujikumbusha ujinga unaondelea katika serikali yetu. Yani ingewekwa na ya quotation ovyo ovyo, ingekuwa fresh kabisa.


Hili limeshafanyiwa kazi. Unakaribishwa.

Tanzania Corruption Tracker - Home
 
Mbona unatufanya tunakosa amani katika mioyo yetu. Hili linalokuja linaogopesha ni hivi unapenda kujua lakini unajua labda ukijua litakuumiza utabaki kusema nafuu nisingejua.
Kwa maana hiyo hakuna suluhu ya swala la meremeta hata tukijua maana inaonekana tanzania kuna watu walio karibu sana na mungu huwezi kuwagusa kwa lolote kazi ipo kweli kweli
 
Mwanakijiji sie wananchi tunajua na tunajua mpaka tumezowea kujua bila ya kuona faida ya kujua kwake.

Tumeshajua mengi sana......sasa tunataka tuambiwe cha kufanya ili tuone faida ya kujua kwake.

It will not be fair enough that 'someone' has to do everything for me and you.it is time for me and you to 'think and think' what do we do,because this country is for me and you!this country is for OUR GENERATIONS!...me and you.as for me am still brainstorming what do we do

ni mtizamo tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom