Ndugu Mtanzania: Je unajua hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu Mtanzania: Je unajua hili?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 15, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji

  Tunajua sana. Tunajua hata mambo mengine ambayo wanadhania hatujui; tunajua hata yale ambayo wao wanasema ni ya 'siri' au yaliyopigwa mihuri ile myekundi ya "Siri Kubwa". Tunajua yanayofanywa nao maofisini na hata mitaani. Kimsingi, sasa hivi tuna taifa la wanaojua sana.

  Kile kinachoitwa "utitiri" wa vyombo vya habari vimetufanya tuwe na uhuru wa kupata habari nyingi na kujua mambo mengi kiasi kwamba tumefika mahali hakuna kinachotushtua tena. Tumekuwa kama tuliopigwa ganzi ya aina fulani kiasi kwamba ili tusikie maumivu inahitajika jeraha kubwa kweli, lakini haya madogo madogo tunashtuka tuna makovu tu hatukumbuki lini tuliiumia na lini tulipona.

  Vyombo hivi vya habari vimepita lengo la kutoa taarifa tu na vimekuwa pia vilele vya maoni huru na malumbano ya kijamii na kisiasa. Mengine haya maoni yoyote isipokuwa kutueleza nani kala nini, wapi na kalala na nani! Wenyewe tumeyakubali na kuyaweka kwenye kundi la Udaku.

  Tunajua mipango yao mingi "ya maendeleo" kwani imeandikwa kwenye vitabu na nyaraka nyingi. Mipango hiyo ambayo imepewa majina matamu matamu na ya kukumbuka inaelezea kila kitu tunachotaka kujua kuhusu ujenzi wa taifa letu. Fikiria kuna MKUKUTA, MKURABITA, na miradi mingine ya kila aina kwenye wizara na idara mbalimbali. Wakati mwingine nafikiria kuna watu wameajiriwa kuja na hii "miradi".

  Tunajua jinsi kashfa mbalimbali zimeligubika taifa letu na wahusika wake wakuu; na siyo tu kujua hivi hivi tunajua kama kwa kukariri. Huwezi kwa mfano kuzungumzia Richmond bila kuzungumzia Dowans; huwezi kuzungumzia Deep Green bila kuzungumzia Meremeta na huwezi kuzungumzia Meremeta bila kugusa Tangold; huwezi kuzungumzia EPA bila ya kugusa Kagoda kama vile usivyoweza kugusa CIS halafu ukaacha kuigusa Benki Kuu. Tunajua nini kimefanyika, wapi kimefanyika, na nani amefanya nini. Na hata pale tusipojua nani amefanya nini tunajua kabisa tukitaka kujua tunaweza!

  Tunajua kuwa CCM haiwezi kushinda inavyoshinda hivi sasa kama kungekuwa na kanuni huru na zenye kuweka mazingira sawa ya kiushindani katika ulingo wa kisiasa. Tunajua kuwa hatuna ujanja wa kubadili mfumo huo na hivyo tunajjikuta tunaendelea kushiriki chaguzi zile zile chini ya kanuni zile zile tukitarajia matokeo tofauti. Hata mahali ambapo ni rahisi kushinda kama kusukuma gari mteremkoni tunashuhudi ugumu wa ajabu kiasi kwamba kumsukuma mlevi inakuwa mbinde!


  Kwa kweli tunajua sana hadi wakati mwingine inaudhi. Kuna wakati naombea tusijue vitu fulani fulani kwani wakati mwingine kutokujua kunakuzuia usiumie au kujisikia hatia. Kuna vitu binafsi nisingependa kuvijua.

  - Nisingependa kujua kuwa Rais wetu anajua kuwa asilimia 30 ya bajeti inaishia mifukoni mwa maafisa wa ngazi za juu!

  - Nisingependa kujua kuwa Mwendesha Mashtaka wetu Mkuu anawajua walioiba kwa kupitia Kagoda na anajua kuwa walikuwa wametumwa lakini hawezi kuwachukulia hatua kwa sababu anajua akifanya hivyo atailetea matatizo serikali yake!

  - Nisingependa kujua kuwa CCM iliahidi kutafuta suluhisho la mahakama ya kadhi lakini badala ya kufanya juhudi hizo miaka 20 iliyopita inajikuta inatuburuza taifa zima na kuleta mgawanyiko. Tungekuwa na mahakama hizo wakati huo nadhani sote tunajua kuwa kusingekuwa na tishio la baadhi ya viongozi wa Waislamu dhidi ya CCM!

  - Nisingependa kujua kuwa viongozi wa kanisa ambao wametoa mwongozo wa kuchagua viongozi bora ndio hao hao wanakuwa wa kwanza kuwaalika viongozi wabovu kwenye shughuli zao za kufungua na kuzindua shughuli za kanisa! Laiti nisingejua jinsi gani walivyo wanafiki!

  Kwa kweli kuna wakati mambo mengine nisingependa kujua kabisa. Baada ya ziara ya ka"nzi" Costa Rica na ile ziara ambayo nusura imvunje mbawa zake kule Upanga, amekuja na kunijulisha undani wa Meremeta undani ambao naamini kabisa na kwa kiasi kikubwa naelewa kwanini Pinda ameapa kutoligusa hilo.

  Laiti nami nisingejua kile anachokijua Pinda na baadhi ya watu jeshini na serikalini (wabunge hawajui kwa hiyo heri yao!). Bahati mbaya sasa nakijua na kimenifanya nikubali kweli Meremeta ni suala la usalama wa Taifa! Ninaijua Meremeta kuliko habari zote zilioandikwa katika magazeti kuhusu kampuni hiyo na sasa kichwa kinaniuma kama ni bora nijue tu yaishe. Laiti wasingefanya hicho walichofanya kwa kupitia Meremeta labda wengine tusingejua.

  Lakini swali linalonisumbua zaidi ni kuwa hivi tunajua ili kiwe nini? Ujuzi wetu wa mambo yanayohusu hali ya nchi yetu, siasa zetu, viongozi wetu unatusaidia vipi? Tunajua mambo haya yote na kupeana taarifa kila baada ya sekunde halafu nini kinafuata?

  Je tunajua ili kuridhisha udadisi wetu ili na sisi tuwe miongoni mwa wajuao? Tunajua ili na sisi tuoneshe kuwa tunajua na si mbumbumbu? Tunajua haya yote na mengine mengi tunayoyapata kijiweni halafu yanatubadilisha sisi tuweje? Kama katika kujua kwako hujabadilika kwa namna yoyote sasa si bora kuishi bila ya kujua?

  Hili la Meremeta kwa mfano hivi likishatoka na kuwekwa hadharani na kuanikwa juani kama mahindi ya kukobolewa ambayo harufu yake hupeperushwa kwenda mbali na upepo wenye vumbi na watu wakajua halafu kitakuwa nini? Kama wabunge waliamua kutokujua na Spika akakubali wasijue na Waziri Mkuu na Sumari wote wakihakikisha watu hawajui sasa sisi tukilifanya lijulikane tunafanya hivyo kwa faida gani?

  Je si bora vingine waendelee kujua hao wachache na sisi wengine tuendelee kujua vile wanavyotaka tujue tu? Na hii ndiyo sababu nyingine ya kuweka mchango kidogo kwenye suala hili ili kuchuja wale wanaotaka kujua isije kuwa tukafanya kitu tukidhania tunafanya la maana kumbe tunaendeleza kupiga watu ganzi?

  Je ni lazima watu wote wajue kila kitu au wakati mwingine ni bora wachache wajue kwa niaba ya wengi? Unajua hilo?
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  huwezi kuzungumzia kashfa zote hizo bila kumzungumzia APSON aliyekuwa bosi wa usalama wa taifa
   
 3. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mimi nataka kujua undani wa Meremeta.... tuwasiliane kwa PM ndugu yangu!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  nilianzisha mada kula na mimi na wewe tumeshalizungumzia sana na Cheche imeshamuandika mara nyingi tu. Siyo yeye tu bali pia ubavu wa leo wa TISS chini ya RO ni muendelezo wa ubovu ule ule wa Apson.

  je unajua hilo?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  usiwe na wasiwasi tuko kwenye final touches of what I would refer as "a groundbreaking, jaw-dropping, earth-shaking exclusive report". Watakaotaka kujua watapewa namna ya kukipata. Don't worry.
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ndio maana Watanzania wengi wana matatizo ya kutoshangazwa na mambo yanavyo endeshwa na serikali zao!

  Kashfa zimekuwa nyingi kiasi ya kwamba zinaonekana kama ni jambo la kawaida tu miongoni mwa jamii... Makabwela hatushtuki tena...!

  Nina wasi wasi itakapofikia wakati kashfa za viongozi wetu na hao tunaowaita mafisadi kutokuwepo tena wananchi wanaweza kuandamana... maana tushazowea ati kupuuzwa na kudhurumiwa.
   
 7. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tusichoke kuwajuza wengine yale ya ukweli tunayoyajua, naamini kwa njia hii, hipo siku tutaipata Tanzania yetu tuitakayo!
   
 8. F

  Froida JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Nina wasi wasi itakapofikia wakati kashfa za viongozi wetu na hao tunao waita mafisadi kutokuwepo tena wananchi wanaweza kuandamana... maana tushazowea ati kupuuzwa na kudhurumiwa.
  _

  yaani inasikitisha huu umbumbu utatutoka lini
   
 9. Mtimti

  Mtimti JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 912
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  kujua kwetu ndio kunakowaumiza vichwa na kuwafanya wawe na woga na hivyo kupelekea kufanya kila aina ya hila ili wasitoke madarakani,wana hiyari ya kufa wakiwa kwenye madaraka ili kuepuka adha ya segerea/ukonga pindi watakapokubali kushindwa.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  nimeipenda hiyo!.. very deep
   
 11. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna wakati nilipokuwa nawaona viongozi wa CCM wakiapa hakuna mpinzani atakayeingia ikulu, na wala haitawezekana kamwe serikali ya mseto kuundwa Zanzibar nilidhani ni kwa sababu wamekunywa maji ya bendera ya CCM. Sasa ndio nimejua kwa nini wanaapa kwa nguvu kiasi hicho hadi povu kuwatoka midomoni. Kumbe ni sababu ya kuficha uchafu wao. Hivi hawajui kwamba iko siku kila kitu kitadhihirika hadharani? Hawafahamu kwamba siku hiyo inakuja very soon tena wote wakiwa hai? Tuliwapa dhamana wakatusaliti sasa ni zamu yetu kuwauliza na kuwasaliti mbele ya familia zao. Wezi wakubwa hawa!
   
 12. M

  Makabe Member

  #12
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kujua kwetu na kuishambulia hiyo Idara ya Usalama wa Taifa hakutoshi, tufike mahali tumsaidie RO ajue anatakiwa kufanya nini katika suala hilo la Meremeta
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kama Waziri Mkuu kaogopa kuigusa RO hana ubavu; na Kikwete ndiyo kabisa! Ndiyo sababu JK mwenyewe aliamua kusitisha shughuli za hiyo Meremeta na hiyo Triennex kujitoa..
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji sie wananchi tunajua na tunajua mpaka tumezowea kujua bila ya kuona faida ya kujua kwake.

  Tumeshajua mengi sana......sasa tunataka tuambiwe cha kufanya ili tuone faida ya kujua kwake.
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Asante, tunasubiria.
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Hapa unamtafutia RO lawama za bure, hiyo ndiyo system yetu, RO kaikuta na ataiacha, life as usual.
   
 17. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bado wananchi walio wengi hawana ufahamu na uoza wa viongozi wetu. Itachukua muda wananchi hasa wa vijijini ambao ndio wengi kujua nini haki yao katika nchi hii na nini watawala wanapaswa kuwafanyia watu wao.

  Sisi wachache wenye ufahamu tuendelee kusambaza tuyajuayo kwa wenzetu hata kama yanaumiza roho kama MMJ anavyosema lakini naamini juhudi hizi zitazaa matunda siku moja hata kama itachua miaka mingi. Tunachofanya ni kupigania vizazi vijavyo. Lazima tukumbuke maneno ya Hekima "You can fool some people for some time but you can not fool all the people all the time". Hivyo tuweke matumaini kuwa japo watu wengi bado hawajapata mwamko wa kuikomboa nchi yetu kutokana na ufinyu wa uelewa lakini siku zaja na zi karibu ambapo watu wetu wataamka kama walivyoamka kule Romania na kupigana kwa mikono dhidi ya vifaru vya Chausesco na ushindi wakaupata. Aluta continua
   
 18. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tunaisubiri kwa hamu hiyo report nasi tujue chakufanya
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Ile miaka ya bongo tambarale ndo inafikia ukingoni. Kama unavyosema MMKJ, kitu kilichowapa heshima kubwa system ni uwezo wa kukaa na ripoti kama hizo bila Taifa kujua nini kinaendelea.Leo hii mambo mengi yako wazi hadharani. Na inavyoonekana UWT ambao tuliwaheshimu, ni kama hawapo maana ukisikia EPA, Meremeta, ya kashfa nyingine nyingi ambazo zinalidhulumu Taifa kwa manufaa ya wachache zinafanikiwa unajiuliza hawa watu wanafanya nini? Ni muundo uliopo hauwapi nguvu ya kufanya kazi independently au ni kujisahau kunakotokana na heshima hii kubwa Watanzania waliowapa wakaona kama wako above them?

  Kwa vyovyote ilivyo, role yao ni muhimu. Kama hawafanyi kazi zao kama inavyotakiwa inasikitisha sana. Hatuwezi kumudu kashikashi za ushindani wa miaka hii tulionayo.
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mbaya zaidi hata wale wanaoonekana kuwa ni MASHUJAA wetu na JUKWAA la kusemea wanalo tena lenye KINGA imara kabisa, BUNGE letu, nao wameamua kukaa kimya. Nawaongelea akina Zitto, Dr Slaa, Mama Kilango,....Wamebaki sasa kukimbizana na VIMACHINGA vya ufisadi kama meno ya tembo, sahihi ya Buzwagi kule London, mradi wa maji Shinyanga,...
  Makubwa wanayasema kwa tahadhari kubwa utadhani hawana ushahidi au wameomba ushahidi kwa "tunaojua" tukawanyima. Imefika mahala nadhani tusameheane, tuanze upya na tusonge mbele kama NCHI?
   
Loading...